CUF yalaani mashambulizi dhidi ya wanachama wake yaliyofanywa na CHADEMA Arusha

Huyu ni mwanachama wa CUF aliyepigwa jiwe na wafuasi wa CHADEMA katika soko la Kilomero, Kata ya Levolosi, Arusha, akiwa anafanya matangazo ya mkutano wa hadhara utakaofanyika Jumapili tarehe 30 Septemba 2012. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na kuhutubiwa na Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba, na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad. Mashambulizi hayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kati, Rashid Shubeti.

Chama cha Wanachi (CUF) kimelaani kitendo cha watu wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA kuwashambulia kwa mawe wafuasi wa CUF, wakati (wafuasi hao wa CUF) walipokuwa wakiendelea na shughuli za kutangaza mikutano ya chama hicho inayoendelea Arusha.

Katika taarifa yake kwa umma mapema leo kupitia mitandao ya kijamii, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro, amesema:

“INASIKITISHA SANA – VIONGOZI WETU WAMEJERUHIWA VIBAYA ARUSHA. Pamoja na kutoa tahadhari kubwa kwa viongozi wa polisi Arusha, kuwa wenzetu wa CHADEMA wanapanga kwa nguvu zote kuwaogopesha wananchi wa ARusha wasihudhurie mikutano yetu kwa kupanga kuwapiga na kuwaumiza viongozi na wafuasi wetu, jeshi la polisi halikuchukua hatua yoyote.

“Hatimaye dakika chache zilizopita, viongozi na wafuasi wetu wamevamiwa na KUPIGWA SANA KWA MAWE na wafuasi wa CHADEMA walioandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo.

“Zahma hii imewakuta viongozi na wafuasi wetu waliotangulia Katika eneo la SOKO LA KILOMBERO kwa ajili ya kuendelea na matangazo ya mkutano wa Jumapili.

“Mawe yalirushwa kama mvua kuelekea kwa wafuasi wetu bila sababu. Ni marundo ya mawe yaliyokuwa yameandaliwa mahsusi kwa ajili hiyo. Cha kushangaza zaidi ni kuwa HAYA yametendeka mbele ya polisi.”

Naibu Katibu Mkuu Mtatiro amesema kwamba majeruhi waliwahi kukimbizwa hospitalini.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Haki za Binadamu wa CUF, Abdul Kambaya ametoa taarifa kwa umma akisema kwamba chama chake “kinasikitishwa na kulaani kitendo cha viongozi wa CHADEMA mkoani Arusha kuwashawishi wafuasi wao kuwaponda kwa mawe wanachama wa CUF wanaoendelea na mikutano ya kisiasa inayofanywa na CUF tangu mwanzo wa wiki hii.”

“Hii medhihirishwa na maneno ya Godbless Lema juzi alipokuwa anawahutubia wafuasi wa Chadema kwenye viwanja vya Stendi ya Nduruma alisema kwamba “CUF wametuvamia” na kuwasihi ile ‘slogan’ ya “kamata mwizi men” sasa ianze. Na ushahidi tunao.

“Hata hivyo, wameshawishi vijana kugawa kiwanja vya Levorosistendi ya Nduruma kwa kisingizio kwamba wanataka kuweka meza za biashara kiwanja ambacho CUF tunategemea kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumapili.

“Leo asubuhi wanachama wa CUF wamepondwa mawe walipokuwa mtaa wa Kilombero kata ya Levorosi. Kutokana na vurugu hizo gari la matangazo la CUF limepondwa mawe na mwanachama mmoja aitwaye Athumani Abdulrahman alipigwa jiwe jichoni na taarifa zimefika polisi.

“CUF inaiona Chadema kama chama kisichoweza siasa za ustahimilivu, hawajiamini na bado ni wachanga kisiasa. Hii inadhirishwa na kutoelewa maana ya demokrasia na uhuru wa Mtanzania kuamua kujiunga na chama chochote atakacho.

“Bado hawajakomaa kisiasa kama jinsi CUF ilivyokomaa. Hatukudhuru chama chochote wanapofanya siasa maeneo mbali mbali hapa nchini.CUF inatoa onyo kali kwa viongozi wa Chadema kwamba hali hii ikiendelea wajue hawataweza kufanya shughuli yoyote Tanzania kwani uwezo wakuwafanya tutakavyo tunao na kwa sababu wameanza tuanaweza kumaliza.

“Ile NGANGARI kwa polisi tunaweza kuwahamishia wao wakose pa kukaa, ila hatupendi tufikie huko na kama wana busara na ni wanasia sawa kweli wenye nia ya kutumia hoja badala ya vurugu kumkomboa Mtanzania watafakari hilo.

“CUF inaendelea kusisitiza tutaendelea na shughuli za kisiasa mkoani Arusha hakuna wa kutuzuia na tutaendelea Oparesheni MCHAKA MCHAKA na mikutano itaendelea kufanyika na kama wao ni wababe kweli na wanatumia hoja ya vurugu, waendelee na mipango yao ya hujuma na tutawafundisha siasa kwani bado hawajakomaa.”

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s