CUF yailainisha Donge

Siku ya Jumatano ya tarehe 15/08/2012 tukiwa katika mfululizo wa ziara ya mkurugenzi wa Habari, uenezi, haki za binadamu, katiba, sheria na mahusiano ya umma, Mhe Salim Bimani tulifika katika jimbo la Donge. Ziara hizi ni mfululizo wa ziara elimishi kwa wanachama wetu wa CUF majimboni kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba ndani ya mkoa wa kaskazini Unguja.

Jambo ambalo binafsi lilinishangaza ni mapokezi tuliyopata na mahudhurio makubwa ya wanachama katika kikao cha kutoa elimu iliyokusudiwa. Nilishangaa kwa sababu mimi binafsi nimekuwa nikishiriki ziara hizi za mkurugenzi tokea zoezi la utowaji wa maoni juu ya mabadiliko ya katiba halijaanza rasmi huko katika mkoa wa kusini Unguja. Kwa kweli sikupata kuona mapokezi na mahudhurio makubwa tuliyoyapata Donge.

Jambo hili pamoja na ninavyolinganisha na matokeo ya utowaji wa maoni yalivyokuwa huko mkoa wa kusini Unguja, nililazimika niamini kuwa pamoja na uwepo wa wakorofi wachache sasa hakuna tena ngome ya wahafidhina hapa Unguja. Wazanzibari wote kwa ujumla wao wameamka wanadai mabadiliko katika mfumo na muundo wa muungano kwa kuwa wamechoka kukandamizwa na kunyimwa haki zao ndani ya muungano huu.

Jambo ambalo hata wewe unaesoma post hii utashangaa ni ushiriki wa sheha wa shehia tuliyofikia katika kikao kilichokusudiwa nae akishiriki upokeaji wa elimu. Hatukuwahi kuona jambo hili huko nyuma, ni jambo geni kabisa. Tulichozoea huko kuona huko nyuma kwa watu kama hawa waitwao masheha ni vitendo vyao vya kuita polisi na kuvisambaratisha hata vikao vya ndani vya CUF na sio kushiriki kwa umakini na kwa nia njema katika vikao hivyo vya kisiasa vya CUF. Sisi kama wageni tulishangaa sana kumkuta sheha hapo, kiongozi wa serikali na kada mpevu wa CCM jambo ambalo lililazimisha tubadilishe staili yetu ya kujiachia katika vikao vyetu tuliyozoea kusema lolote ambalo linawatia hamasa wanachama wetu na badala yake sasa tutumie staili ya kidiplomasia ya kutomuudhi Mhe sheha.

Wawasilishaji mada, Mhe. mkurugenzi, kamanda mkuu wa blueguard, mkuu wa protokali, afisa wa utafiti na sera na mimi binafsi, katibu wa naibu katibu mkuu, ambae niliwasilisha ujumbe maalum kwa vijana ilibidi tujipange upya katika uwasilishaji. Sio tu kwa lengo la kutomuudhi kiongozi wa serikali ambae ana misimamo na sera tofauti na zetu na hasimu wetu wa kudumu, lakini pia kwa lengo la kujenga ushawishi wa kutosha ili avutike katika agenda zetu kupitia mada zitakazowasilishwa.
Wawasilishaji wote waliwasilisha na kumaliza. Baadae walipewa nafasi wanachama waulize maswali na kujibiwa. Baada ya hapo Mhe Sheha nae alipewa nafasi kuuliza maswali na kutoa nasaha zake. Swali lake lilikuwa hivi “ndugu mkurugenzi hivi hii tume itakuja kiwilaya, kijimbo au kishehia” aliuliza. Baada ya mkurugenzi kujibu swali lake ndipo alipotakiwa sasa atowe nasaha zake kama kiongozi wa serikali. Hapo ndipo Sheha aliponishangaza mno. Ikumbukwe kuwa ni baada ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa tu ndipo chama chetu cha CUF kilifanikiwa kufungua tawi la mwanzo katika jimbo la Donge tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi1992. Mara zote ilipopangwa ratiba hatana tume ya uchaguzi kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni jimboni humo, mwakilishi wa jibo hilo abae amekuwa waziri muda mrefu hutumia vikosi vya polisi kuwashabulia wanachama wa CUF kwa risasi za moto na kuvunja ratiba hizo.

Kwa kuwa hotuba zetu wakati wa uwasilishaji zilipambwa na hoja za wazi ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa seriakali kutoka CCM jinsi Zanzibar inavyokandamizwa ndani ya muungano basi sheha alivutiwa sana na kukiona kikao kizima kuwa ni cha maana na agenda zake ni ukweli mtupu unaohitaji kufanyiwa kazi kikweli. “Mhe mkurugenzi mimi niseme tu hayo mliyoyaeleza yote ni ukweli mtupu, kwa hiyo wazanzibari tume ikija tuseme kuwa Zanzibar inahitaji madaraka yake na heshma yake maana hivi sasa kuna matatizo mengi” alisema.

Amka mzanzibari hata waliojifunza kutokutusikiza wanatusikiliza na wanatusikia. Na pia wanaunga mkono hoja za CUF ya muungano wa haki baina ya nchi mbili ikiwa ni pamoja na kurejeshwa jamhuri ya Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani ya muungano.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s