Hamad Masoud kujiuzulu ni hatua kubwa kisiasa – JUVICUF

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

PONGEZI ZA JUVICUF KWA WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO KWA UWAMUZI WAKE MAKINI WA KUWAJIBIKA KISIASA

JUVICUF inatoa pongezi za dhati kwa Mhe Hamad Masoud kwa uwamuzi wake wa kujiuzulu ili kuonyesha spirit ya dhati ya kuwajibika kisiasa.

Tunaamini alikuwa mmoja wa mawaziri waliofanya makubwa ili kuleta mabadiliko katika sekta ya mawasiliano na miundombinu Zanzibar. Tulikuwa tunamshuhudia alivyokua Mbioni Ulaya kutafuta misaada kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa Barabara na vitega uchumi vya Bandari na viwanja vya ndege. Uwanja wa ndege wa Zanzibar hapo awali ulikua ni vurugu tupu hujui nani aningia na nani anatoka au nini kinaingia na nini kinatoka. Tunafahamu alikabidhiwa uoza uliokuwemo katika wizara hiyo iliyojaa Ubinafsi, rushwa, upendeleo na Ubadhirifu. Hata hivyo hakujali alijikaza na kufanya mabadiliko makubwa. Huu Ndio uungwana na uwajibikaji, vijana wa CUF na Wazanzibari wote tutakua nae akiwa ndani ya Serikali au Nje na daima tutazithamini jitihada zake.
Kujiuzulu kwa Mheshimiwa Hamad Masoud ni ishara tosha kwamba viongozi wa CUF si waroho wa madaraka bali wapo kuwatumikia watu. Hii ni heshma kubwa kwa chama chetu na picha kamili ya kuwaonyesha wazanzibari na watanzania kwamba CUF haipo serikalini kwa ajili ya kupata vyeo bali kuwatumukia wananchi.
Kutokana na dosari kadhaa wa kadhaa zifuatazo zilizofungamana na maafa haya tunawashauri viongozi wengine wa kisiasa waliohusika wajiuzulu kama alivyofanya mwenzao ili na wao kuonyesha dhati yao ya kuwajibika kisiasa.
1. Vikosi vya ulinzi vilikosa kutimiza wajibu wao kwa wakati. Kwa mfano kikosi cha KMKM kilifika katika eneo la tukio saa 12 jioni wakati kikosi cha wanamaji cha JWTZ kilifika katika eneo la tukio siku ya pili yake. Kwa kuwa ajali ilitokea kiasi cha saa 7.30 mchana, Jambo hili limepelekea watu wengi kukosa msaada wa kuokolewa.
2. Kikosi cha Wanamaji cha JWTZ kilipaswa kuwa na jukumu la uokozi wa meli hiyo lakini hata hivyo halikufanyika mapema kutokana na kutokuwepo na kikosi imara cha dharura (standby unit) pamoja na kukosa vifaa vya kutosha vya uokozi kama vile rubber boats na fibre boats. Badala yake vifaa hivi vilifika katika eneo la tukio na kuanza kutumika siku ya pili yake wakati watu tayari wameshafariki.
3. Pamoja na Tume ya Maafa na Mwenyekiti wake kufika katika eneo la tukio haikuweza kutoa msaada wa kutosha kutokana na kuwa haikuwa na wataalamu wa masuala ya maafa. Wengi wa waokoaji waliofika walikuwa ni raia wa kawaida. Aidha katika zoezi hilo hakukuwa na Kikosi cha Uokozi na kamanda wake jambo ambalo lilikuwa dosari kubwa na kusababisha zoezi hilo kukosa muongozo.

Kwa kuwa dosari hizo ziliongeza ukali wa tatizo tunamshauri sana Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais, Mheshimiwa Mohd Aboud ambaye anasimamia masuala ya maafa ajiuzulu kwa kushindwa kufanikisha zoezi la uokozi kwa wakati na kwa ufanisi pamoja na kwamba miezi kumi tu iliyopita kitengo hicho cha maafa kilipata funzo na msaada mkubwa wa kifedha kufuatia kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander.

HAKI SAWA KWA WOTE

Khalifa Abdalla Ali
Katibu wa Jumuiya ya Vijana CUF – Taifa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s