Taarifa kwa vyombo vya habari

Kama ilivyobainika kwa umma wa Wazanzibari, Chama cha Wananchi, CUF, kimepokea kwa moyo mmoja Hatua ya Kamati Teule ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, tokea kuteuliwa kwake hadi Ripoti yake Rasmi, juu ya namna ambavyo Serikali inawajibika kunusuru hali mbaya ya Uchumi wa Visiwa vya Unguja na Pemba, unaoendelea kudhoofika kutokana na ufisadi wa viongozi wachache.

Hii ni kutokana na imani kwamba Serikali ya Zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa bila shaka inayo azma ya kuamua kwa makusudi kupiga vita na kuzuia moja kwa moja, tabia ya matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya mali ya wananchi pasi na kujali maslahi ya umma.

Azma hiyo njema ya Baraza la Wawakilishi na Serikali kwa ujumla, haikubainika tu kutokana na hatua ya kuuundwa na kupewa mamlaka kamati hiyo, bali pia ile ahadi kwamba Dola ya Nchi hii itatekeleza wajibu wake kutokana na Ripoti ya ufisadi huo, kwa kujali maoni na mapendekezo, kama ilivyoshauriwa na Wajumbe.

Heko Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi namna walivyosimama kidete kuchangia na kuunga mkono hoja za Ripoti hiyo, zilizotokana na ushahidi wa wazi juu ya namna ambavyo Uchumi na Maendeleo ya Zanzibar yanadhoofishwa na ufisadi wa watu wachache.

Chama cha CUF kinaamini kwamba sauti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ndiyo kauli hasa ya wananchi wote wapenda haki wa Visiwa vya Unguja na Pemba, na ambayo katu haitokuwa busara wala haitovumilika kuipuuza tu kwa misingi ya kujuana au kulindana huku nchi hii na watu wake, ikiendelea kudhoofika.

Chama cha Wananchi, CUF, kinaamini kuwa Serikali ya Awamu ya Saba inayo azma ya kuwajali, kuwasikiliza, na kuwakomboa wananchi, kama ilivyodhihiri katika Ripoti ya Kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islander, na hatua zilizofuata.

Ni wito na tahadhari ya Chama cha CUF, kwamba Serikali itatekeleza ahadi ya kuwachukulia hatua haraka iwezekanavyo, wote waliohusika na ufisadi huo, bila ubaguzi wala upendeleo pasi na kuwapo misingi ya uonevu na ubabaishaji, ili Dola iweze kutoa funzo na pia kujenga imani ya Wazanzibari wote, kwa mamlaka waliyoipa madaraka ya kutawala.

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………….
Salim Bimani,
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari, Uenezi, na Mawasiliano na Umma, CUF

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s