Taarifa kwa vyombo vya Habari -CUF

Our Ref: CUF/HQ/KR/U/01/012/042 Date:28/03/2012

 

Chama cha Wananchi,CUF, kimepokea kwa moyo mmoja Hatua ya Serikali ya Zanzibar, yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa, kunusuru mazingira na haiba ya Visiwa vya Unguja na Pemba, kwa kuamua kupiga vita na kuzuia moja kwa moja matumizi ya misumeno ya moto, bila kuwapo kibali maalumu.

Huu ni uamuzi muhimu wa kuokoa tabianchi, hasa wakati huu ambapo Zanzibar, kama ilivyo katika nchi nyengine ulimwenguni, inakabiliwa na tishio kubwa la janga la mmonyoko wa ardhi, litokanalo na uharibifu wa mazingira.

Hapana ubishi kwamba misitu ni uhai na sehemu muhimu ya maisha ya watu wa nchi hii; hivyo kuitunza ni jambo la lazima, ili kuokoa kiasi ya hekta 950 zinazoteketea kila mwaka kupitia matumizi ya misumeno ya moto.

Ni busara kuamini kwamba mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe; hivyo ni wajibu kwa kila upande, kuanzia Serikali iliyochukua hatua hiyo hadi wananchi wa kawaida, kutekeleza kwa vitendo agizo hilo muhimu.

Pamoja na Serikali kuweka bayana adhabu kali ya Faini ya Shilingi 300,000 au Kifungo cha Miezi Sita Jela, kwa kila atakayekaidi agizo hilo kwa mujibu wa Kifungu cha 8 (1) (2) cha Sheria ya Zanzibar ya Mwaka 1996; Wito wa CUF ni kuwepo udhati wa utekelezaji na usimamizi wake, pasi na misingi ya ubaguzi, upendeleo, dhulma, ukandamizaji, wala ubabaishaji wa namna yoyote.

Pamoja na hayo, Chama cha CUF, kinatoa wito pia kwa Serikali, kutafuta njia mbadala za wananchi kujipatia ajira na riziki zao za halali, ambazo zinajali uhai na utunzaji wa mazingira.

Chama cha CUF, kinatoa wito huo kikiamini kwamba Serikali inao uwezo kamili wa kusimamia hatua na sheria zake, na hii ya Kuzuia Matumizi ya Misumeno ya Moto ikiwa mojawapo; ingawa la msingi zaidi ni Serikali yenyewe kuwa kigezo katika utekelezaji, ili kuweza kujenga tabia ya utiifu, bila usumbufu, kwa wananchi ambao pia ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa kanuni na maagizo.

Chama cha CUF, kinaamini “inawezekana iwapo kila mmoja atatekeleza wajibu wake”, kupitia azma njema, haki, utaratibu wa busara, kwa maslahi ya maendeleo na uhai wa nchi yetu kwa ujumla.

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………….

Salim Bimani,

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari, Uenezi, na Mawasiliano na Umma, CUF

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s