Taarifa kwa vyombo vya Habari

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI- MACHI 8, 2012

Umekuwepo usemi kwamba ukombozi wa jamii au nchi yeyote unategemea kwa kiasi kikubwa ukombozi katika uzalishaji, na zaidi katika kustawisha maendeleo yaliyokamilika, ambapo kwa ujumla wanawake ndio wahusika wakuu.

Ni kweli ustawi bora wa jamii unategemea pia ustawi bora wa akina mama, wakubwa kwa wadogo, na katika nyanja zote za maisha.

Chama cha Wananchi, CUF, kinaamini kwamba wanawake ni sehemu muhimu sana ya jamii na katika maendeleo ya nchi kwa ujumla, kwani bila uhusika wa akinamama si rahisi kuyafikia maendeleo ya kweli.

CUF, tunaamini kwamba maendeleo ya kweli na ujenzi imara wa Taifa, yatawezekana pale ambapo wanawake watashiriki kikamilifu kama inavyostahiki, na hili linategemea nguvu za makusudi za kuwawezesha kiuchumi, kielimu, kiafya, kijamii, na kimaisha.

Aidha, Chama cha CUF kinaamini kwamba wanawake wanaweza kutekeleza wajibu wao wa kuhamasisha maendeleo na ujenzi kamili wa Taifa, pale ambapo kwa makusudi wataweza kuepukana na madhila yanayowakabili katika ulimwengu wa sasa yakiwemo ya udhalilishaji wa kijinsia, ubakaji, ukandamizaji, dhulma, na kila aina ya mateso.

Chama cha CUF hakiwezi kuridhia hata kidogo dhulma dhidi ya wanawake hata iwapo ni matumizi mabaya ya shakhsia ya mwanamke kama inavyoshuhudiwa sasa kuona kwamba sehemu hiyo ya jamii ni kiwakilishi cha burudani na mapambo, kisichokuwa na thamani yeyote katika maendeleo.

Ulimwengu unashuhudia sasa hilaki inayowakabili wanawake kuanzia ngazi ya familia, jamii, utekelezaji wa majukumu yao, sehemu za kazi na hata katika utendaji kama watumishi wa umma; kuanzia vipigo na kila aina ya ufedhuli, hali ambayo inathibitisha wazi kwamba ile huruma ya asili na ya uungwana, dhidi ya wanawake, imetoweka.

Hivyo, Chama cha CUF, kinatoa wito kwa mamlaka zote kuanzia Familia hadi ngazi ya Taifa, kuheshimu na kuhamasisha haki za msingi kwa wanawake, ambazo ni pamoja na huduma muhimu za kijamii, zikiwamo elimu, afya, na heshima yao kwa ujumla.

Mwisho, Chama cha CUF kinasema HEKO WANAWAKE! HEKO AKINAMA! HEKO KWA UJASIRI WENU! NDIYO MNAWEZA PINDIPO MKIWEZESHWA!

HAKI SAWA KWA WOTE!

_______________________________________________________________

Salim A. Bimani,
Mkurugenzi, H/B/H/U/Mahusiano ya Umma

Headquaters: P.O.Box 3637, Zanzibar, Tanzania. Tel.: 024 22 37446 Fax.: 024 22 37445
Main Office: PO. Box 10979, Dar-es-Salaam, Tanzania. Tel. 022 861009 Fax.: 022 861010

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s