Mfumo tenganishi hauna nafasi tena Zanzibar -Maalim Seif

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad jana alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) imedhamiria kumaliza mfumo wa siasa tenganishi visiwani humo.
Alisema serikali iliyopo madarakani sasa ni shirikirikishi na kwamba mfumo huo ndio njia pekee ya kuimarisha umoja miongoni mwa wananchi visiwani humo.
Maalimu Seif alikuwa anafungua mkutano wa pili juu ya hali ya siasa, ambapo ajenda yake kuu ni uimarishaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar .
Aliwaambia washiriki wapatao 250 wa mkutano huo ulioandaliwa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet) kuwa mfumo wa siasa tengenishi haina nafasi tena Zanzibar kwa sababu wananchi wameuchoka.
Maalim Seif alisema chini ya GNU wananchi wako karibu sana na pia wanashirikiana sana na viongozi katika juhudi za kujiletea maendeleo bila kujali itikadi zao.
“Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeondoa ushindani usiokuwa na tija katika siasa na sasa chini ya serikali shirikishi wananchi wako karibu sana sasa katika kusirikiana na viongozi wao kujiletea maendeleo,” alisema.
Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF aliwaomba wasomi nchini na taasisi za kimataifa kuendelea kusaidia juhudi inayochukuliwa na serikali ya Zanzibar kuimarisha mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo, ikiwa ni hatua ya kudumisha utulivu uliopatikana baada ya mfumo huo kuanza mwaka huu.
Alisema hali ya utulivu na amani uliopo sasa Zanzibar unatoa fursa kwa wananchi na viongozi kufanyakazi za maendeleo badala ya kushughulikia masuala ya migogoro.
Juu ya mchango uliowezesha kupatika GNU, Maalim Seif alisema ingawa kupatikana kwa mfumo huo ni juhudi ya Wazanzibari wenye, ushauri wa wasomi kupitia taasisi yao Redet umesaidia sana kuleta mafanikio.
Hata hivyo alisema mchango wa taasisi hiyo bado unahitajika ili kufanikisha chngamoto zinazoikabili Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutokana na kuendelea kuwepo kwa viongozi wachache wasioridhika na uwepo wa serikali hiyo visiwani.
Juu ya mchakato wa Katiba ya Tanzania , Maalim Seif alisema utekelezaji wa suala hilo ulenge zaidi katika kuondoa sura inayosababisha pande bmili za Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar kufungana kikatiba.
Alisema sura ya Muungano iliyopo inadumisha migogoro badala ya kuimarisha muungano.
Mkutano uliofunguliwa na Maali Seif unatarajiwa kufungwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

Bonyeza hapa kusoma Hotuba ya makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s