Tusitegemee Kutetewa Zanzibar na viongozi wa Zanzibar walioko kwenye Muungano, kwao sio Uzalendo ni uchumi wakujilimbikizia mali.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibr, Balozi Seif Ali Idd

Hakuna shaka kuwa kuna mtandao mkubwa wa connection za vigogo hawa vinara wa wa tumiao Muungano kama kigezo cha kujitajirisha nafsi zao huku kutokushindwa kutunisha misuli yao kwa kutetea maslahi ya Zanzibar katika Muungano.
Wako wengi wenye kuiona Zanzibar inayayuka lakini maslahi yao binafsi yalindwe, Kinara namba wani ni Mh Gharibu Bilali huyu ndio baba wa hawa watatu Mh Samia Suluh na Makamo wapili wa Zanzibar Seif Ali Idd na Kificho Spika wa BLW Zanzibar.
Hawa wenyewe wana connection kubwa ya kuiangamiza Zanzibar katika giza totoro la Muungano, kutokana na nafasi zao walizopewa, hakuna hata mmoja wa hawa pelelezeni mwenye kutunisha misuli kwa kuyatetea maslahi ya Zanzibar.
Hutumia vyeo vyao hawa bada ya kutetea maslahi ya Zanzibar huzidi kuwarahisishia maaduwi wa Zanzibar njia za kupita kutokana na uwakilishaji wao mbele ya Zanzibar.
Hawa hujiona kuwa Zanzibar ni miliki yao na wakishaamua au kukinga chochote basi hakuna yoyote tena mwenye uwezo wa kuvunja ukuta, lakini cha kushangaza ni kuwa kinga yao haiji pale penye kuona kuwa Zanzibar inahujumiwa, bali hutowa mwanya na kurahisisha kazi ya aduwi kuihujumu Zanzibar.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mh; Pandu Ameir Kificho

Iko mifano mingi tu kuwa viongozi wetu ndio maaduwi wetu wa kuinakamiza Zanzibar na kuidhoofisha katika kodi za Muungano, Viongozi wenzetu wa Serikali ya Tanganyika wajiitao viongozi wa Serikali ya Muungano, wanapo vunja katiba hufyata ndimi zao.
Lakini Wazanzibari wanaponung’unika na kutetea haki zao katika Muungano viongozi wa Muungano Bara huwa ndio wa mwanzo kubweka na kuisulubu Zanzibar kuwa imevunja katiba na Sheria za Muungano na hapo Watanganyika, hasa wale wasiopenda kusikia kuwapokwa Unguja na na Pemba, wote huwa na itikadi moja kuwa Zanzibar imevunja katiba.
Sasa tujiulize Wazanzibar hizi kero za Muungano ziko Zanzibar tu Bara hakuna? Na kama Bara ziko ni zipi na zipi ili zifanyiwe kazi? .

Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Mohammed Gharib Bilal

Kwa mtazamo wangu nikuwa ikiwa tutachukuwa kero za Muungano za pande zote mbili basi ni kusema hakuna Muungano bali kuna ubabaishaji wa makundi Fulani kutoka CCM kutumia Muungano na kero za Muungano ili kuendeleza maisha yao binafsi ya kujilimbikizia mali.
Kwa upande wangu mimi nasema hakuna kero za Muungano bali kuna kuvunja Muungano wenyewe katika system na style hii isiyokubalika, kama kuna kero za Mungano basi kero kubwa ni kufa kwa Tanganyika, Kuchukuwa Mambo yasiyo ya Muungano kuingizwa kuwa ya Muungano, mfano mfupi tumeona juzi tu Waziri asiyehusika na mambo ya ya Muungano kuvaa Joho na kuingilia mambo yasiyo muhusu.
Ikiwa yeye ni Waziri Wa Ardhi ,Jee Ali Juma Shamuhuna ni Naibu Waziri wake? Hii ndio Zanzibar kuonekana kuwa sio nchi wala haikuwahi kuwa nchi yenye kuungana na nchi nyingine kupatikana na huo Muungano.
Wenzetu wamezowea kutudhoofisha na kujifanya wao ndio top na supper power, hii inachangiwa pakubwa na viongozi wetu wanaoshughulikia mambo ya Muungano na yasio ya Muungano kuto kukemea na kutunisha misuli yao wakati wanapobaini maslahi ya Zanzibar yanakanyagwa.

Mh Samia Suluh Hassan, Waziri anaeshughulikia Mambo ya Muungano.

Bali hawapo kwa Uzalendo na utetezi wa Zanzibar wapo katika maslahi yao binafsi ya kidunia, kama Wazanzibari hawajapiga kelele au Baraza la Wawalilishi kupelekwa hoja Binafsi na Mjumbe, basi wao hukaa kimya na huyo muhusika mkuu makamo wa Raisi wa Muungano hujibweteka kwa kupewa kazi ya kukata utepe na ziara za vijijini Bara.
Hivi sasa yuko katika kampeni za kupinga nafasi ya Raisi wa Zanzibar kuwa ndio makamo wa Raisi , hii ndio kichwa kinamuuma hivi sasa na yuko tayari kuitowa Zanzibar ili yeye tu asalimike na Umakamo wake.
Mungu ibariki Zanzibar na madudu haya yenye kujitakia wenyewe Wazanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s