CUF wamtaka JK kutimuwa mawaziri.

Nd Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakati mgomo wa madaktari leo ukiingia siku ya pili, chama cha Wananchi (CUF), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete,kumuwajibisha Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Dk, Hadji Mponda , Naibu wake Dkt Lucy Nkya, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi blandina Nyoni na Mganga wa Serikali Dkt. Deo Mtasiwa kwa kuchelewa kufanyia kazi madai ya Madaktari hao.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho kwa vyombo vya habari Dar-es-Salaam jana, inasema, chama hicho kinamtaka Rais Kikwete kukutana na Madaktari hao na kuwasihi warudi makazini.
“Pamoja na kuwarudisha kazini, Serikali inapaswa kuhakikisha madai yao yanafanyiwa kazi kwani madaktari wanadhamana kubwa ya uhai wa Watanzania ambao ndio wapiga kura waliomchagua katika nafasi aliyonayo,” imesema taarifa hiyo.
Chama hicho kimesema , madai yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya muda ya Jumuia ya Madaktari, dkt. Stephen Ulimboka ni pamoja na kuitaka serikali iwawekee mazingira bora ya kazi kwa kupeleka vifaa vya kazi kwenye hospitali na vituo vya Afya.
Madai mengine ni kuboresha malipo ya posho na kuwapatia stahili zote, kuwapatia nyumba za kuishi au kuongezwa asilimia 30 ya mshahara wao na kuongezwa mishahara kwa asilimia 30 badala ya 10 wanayolipwa sasa.
“Sisi tuaamini viongozi katika waizara hii, wanafanya kazi kwa dharau, hii inatokana na ukweli kwamba familia zao hazitibiwi na hawa madaktari, bali wanatumia kodi za Wananchi kwenda nchini India na Ulaya kwa matibabu,” alisema.

Pr. Ibrahim Haroun Lipumba, Mwenyekiti wa CUF Taifa

Wakati huhuo, chama hicho leo kinafanya maandamano ya amani kumpongeza mwenye kiti wake Profesa Ibarahim Lipumba kwa kuchaguliwa kuwa miongoni mwa Wachumi wanaoshughulikia uchumi wa dunia.
Katika taarifa yake aliyotoa jana kwa vyombo vya habari, Naibu Mkurugenzi wa Mipango, uchaguzi na Siasa wa chama hicho, Bw. Sheweji Mketto, alisema maandamano hayo yatafanyika saa saba mchana Mbagala Wilayani Temeke.
Alisema Profesa Lipumba ameanza kazi hio nchini Marekani kwa miezi mitano sasa ambapo maandamano hayo yatauganishwa na Kumbukumbu ya tukio la Mwenyekiti huyo kuvunjwa mkoo na Polisi na wanachama wengine kujeruhiwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi.
Aliongeza kuwa tukio hilo lilitokea January 25,2001 kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na aliekuwa mbunge wa Kigamboni Bw.Frank Magoba ili kuhimiza maandamano yaliyopangwa kufanyika January 27,2001.
Bw. Mketo alisema maandamano hayo yalikuwa na lengo la kudai mabadiliko ya katiba mpya. Tume huru ya Uchaguzi, kutomtambua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume kama Rais, kushinikiza kurudiwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar na kupinga kauli ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Bw. Benjamin Mkapa kukataza maandamano na mikutano ya hadhara ya kisiasa.
Maandamano hayo yataanzia Mbagala Sabasaba kwa Mpili kwenda viwanja vya Zakhem ambapo viongozi mbalimbali wa CUF, watahutubia.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s