“Taifa lapitia kipindi kigumu cha maafa”

Ni dhahiri kwamba huu ni wakati ambao nchi imekuwa ikikabiliwa na mfululizo wa misiba katika ngazi mbali mbali kuanzia familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Hii ni hali ambayo kwa namna moja au nyingine imekuwa ikihitaji tafakari ya kina, juhudi za makusudi, na ikibidi hatua za dharura, ili kukabiliana na athari za matukio hayo au kuweza kuyaepuka kabisa pale inapowezekana.

Kwa wakati huu, bado umma umekuwa ukikumbuka majeraha ya kuondokewa na ndugu na jamaa zao kutokana na masaibu hayo yakiwamo ya Ajali mbali mbali, Mafuriko, na hata Kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islanders, iliyochukua sura ya kihistoria na isiyosahaulika.

Chama cha Wananchi, CUF, kimepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa ya Vifo vya Watu 7, wakiwamo Watoto 6 na Mzee 1, huku wengine kadhaa wakiugua na kuendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

Msiba huo unatokana na kile kilichoelezwa, kitendo cha watu hao kutumia kitoweleo cha Nyama na Kasa, katika Kijiji cha Tumbe, Wilaya ya Michewni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

La kusikitisha zaidi maafa hayo yametokea ambapo kulishakuwapo na marufuku ya kutumia aina hiyo ya viumbe, kama kitoweleo, ingawa zipo taarifa kwamba baadhi ya wananchi huvua kasa hao na kisha kuwauza wengine kwa siri.

Chama cha CUF kinatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu na pia walioathiriwa katika tukio hilo.

Pamoja na hatua hiyo, Chama cha CUF kimekuwa kikitafakari na kinaamini kwamba mazingira hayo yanatokana pia na uchache wa taaluma au taarifa za tahadhari juu ya viumbe hao.

Kutokana na hali hiyo Chama cha CUF kinatoa wito kwa Mamlaka zinazohusika, zikiwamo Wizara ya Afya, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na pia Mamlaka zote za Maliasili nchini, kuchukua hatua za makusudi, ili kukabiliana na mazingira ya namna hiyo.

Pia, Chama cha CUF kinatoa wito kwa Mamlaka zote husika, kuongeza kiwango cha taaluma kwa wananchi juu ya madhara yanayoweza kujitokeza kwa jamii na kwa Taifa, endapo watu wataendelea kuwatumia kwa ajili ya chakula, viumbe hao.

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………………..
Salim Bimani,
MKURUGENZI WA HAKI ZA BINAADAMU NA MAHUSIANO YA UMMA, CUF

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s