Taarifa kwa Vyombo vya habari

Misiba ni sehemu ya majaribu yanayotufika wanadamu huku tukiamini kwamba kila msiba una ukubwa na uzito wake kwa jamii, serekali, na taifa kwa jumla.

Lakini hakuna binadamu yeyote anaependa kufikwa na majaribu haya ya Mungu kwa kupata msiba, hii ni kwa sababu hakuna msiba mdogo; na kila msiba huwa unaziumiza nyoyo zetu na kututia huzuni kubwa sana.
Chama Cha Wananchi-CUF, kimestushwa na kuipokea kwa huzuni kubwa sana taarifa ya ajali ya gari ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliyotokea jana majira ya saa saba na robo (7:15 mchana) katika maeneo ya Fuoni.

Ajali hii imeripotiwa kuuwa mwanajeshi mmoja aliejulikana kwa jina la Yassin Mohammed Yassin kutoka Tanzania Bara, na kujeruhi wanajeshi ishirini na nne (24).
Chama Cha Wananchi-CUF, kwa huzuni kubwa; kinapenda kutoa mkono wa pole kwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi, ambaye ni Rais wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete.
Pia kinatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania Adam David Mamuyange, Briged Kamanda wa Zanzibar, wanafamilia na watanzania wote kwa ujumla.

Tunamuombea maisha mema peponi kwa yule alifariki, na pia tunawatakia afya njema na kupona kwa haraka wale waliopata majaraha, Mungu atawasaidia.
Aidha, Chama Cha Wananchi-CUF, kinatoa mkono wa pole na salamu za rambi rambi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kifo cha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Balozi Athumani Mhina.
Pia kinatoa mkono wa pole kwa Katibu Mkuu CCM Taifa, Bw.Wilson Mukama, wanafamilia ya marehemu, na wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi. Tunaamini kifo chake ni pengo kubwa si kwa familia tu, bali hata kwa nafasi yake aliyokua ameishikilia katika CCM.
Mwisho, Chama Cha Wananchi-CUF, kinawaombea marehemu wote makaazi mema peponi, na kuwatakia mioyo ya subira na uvumilivu wanafamilia za marehemu.
_________________________________________

HAKI SAWA KWA WOTE.
…………………………………….
MKURUGENZI WA HAKI ZA BINADAMU NA MAHUSIANO YA UMMA, CUF.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s