Haki ya misaada ya mafuriko iwe kwa wote

Na Julius Mtatiro

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro

Jana (29 Disemba 2011) tumeimaliza siku nzima kwa kazi ya kuzungukia kambi za wahanga wa mafuriko Dar es Salaam. Nimeongoza ujumbe wa viongozi waandamizi wa chama taifa na wilaya na tumepita katika kambi mbilimbili katika kila wilaya ya Dar es salaam.

Zoezi hili limekuja baada ya kupita kwa mara ya kwanza mara baada ya mafuriko. Leo tulikuwa na kazi moja kubwa, KUTOA MISAADA KWA WAHANGA. Katika kila kambi tuliyopita tumewafariji wahanga na kutoa misaada ya UNGA, MCHELE,  SUKARI, MAFUTA YA KULA, DAGAA, SABUNI, MAJANI YA CHAI, NGUO, MAHARAGE, n.k.

Wahanga wengi wamechanganyikiwa na hawajui namna gani wataanza maisha mapya ya umasikini mkuu.

Tumeieleza ofisi ya waziri mkuu kwa barua kuwa ni lazima haki itendeke kwa kila mhanga bila kujali alikuwa mwenye nyumba au mpangaji.

Ikiwa wenye nyumba watahamishiwa maeneo mengine na kupewa viwanja na fedha za kujengea na kujikimu lazima pia wapangaji wapewe haki hiyo kwa ”status” yao.
Hii ina maana kuwa lazima wapangaji wote pia wapewe fedha za kuwawezesha kupanga mahali pengine na fedha za kuanzisha maisha mapya.

Ikiwa serikali itajaribu kuwakwepa wapangaji itafanya ukatili mkubwa na usiomithilika. Ikumbukwe kuwa katika ulipaji wa kodi mpangaji analipa sawa na mwenye nyumba. Hii ni kwa sababu wote wananunua bidhaa madukani na kulipa kodi ileile kila siku.

Serikali inapoingilia majanga ya namna hii kama wajibu wake lazima ihakikishe haibagui watanzania hawa wasiojua kesho yao.

Jambo la pili ambalo tumeitaka serikali ilifanyie kazi ni kuwa – makambi mengi yako maeneo ya shule n.k. Na januari imefika inabidi watoto warudi madarasani.
Tunatambua serikali hii hulipuka kila mara na mambo yake kutoka usingizini. Tunajua watakurupuka na kutaka kuondoa wahanga kwa nguvu ili shule zifunguliwe. Tumeitahadharisha ofisi ya waziri mkuu izimgatie haki za watu wote na kuwa serikali iandae makambi yasiyo shule mapema ili wahanga wahamie huko kupisha huduma kwa wanafunzi ziendelee.

Jambo la tatu, kwa mtizamo wa chama chetu, masuala haya ya wakazi waishio bondeni ni matatizo ya udhaifu wa serikali ambayo haijiamini.

Ikumbukwe kuwa nyumba nyingi katika mabonde zimejengwa baada ya mwaka 1961. Hii ina maana kuwa wakati zinajengwa serikali ilikuwepo, lakini serikali hii isiyo na mipango hadi leo haikiwa na mipango tangu enzi za uhuru.

Leo wananchi wanajenga kila kona na serikali inawatizama tu, inajidai haioni. Yakitokea masuala kama haya mazito ndo serikali inatoka na kubweka kidogo. Baadaye inakaa kimya na kwenda kugawa kanga na vilemba ili ipigiwe kura na wakazi walewale wa mabondeni – uchuro!

Ikiwa tutaendelea na mzaha, siku moja tutaamka na kukuta tumekufa wote – kifo cha kijinga tu!

Mji kama dar hauna ”security” hata kidogo. Miaka 50 ya uhuru bado dar haina mfumo wa maji unaoeleweka, dar bado haijitambui. Watu wanajenga kila kona, hadi barabarani! Serikali ipo, imelala fo fo fo, haina meno!

Hawa waliojenga mabondeni wasilaumiwe, serikali lazima ibebe msalaba, wakati wanajenga mabondeni serikali ilikuwa likizo? Mbona tunafanya masihara katika masuala makubwa kama haya?

Mbona serikali ina uwezo mkubwa wa kujua majambazi wamejificha pori fulani, wako kadhaa? Mbona serikali inajua upesi wananchi wa kiji fulani wataandamana kesho kudai haki zao na ikatuma haraka polisi wawapige mabomu? Mbona serikali inajua mtu fulani siyo raia n.k ?
Kwa nini serikali hiyohiyo haielewi nani anajenga wapi na kwa nini anajenga hapo?

Taifa hili litafika ukingoni siku moja, kama hatutajirekebisha, siku moja tutakuta maji ya bahari ya mejaa miji muhimu kama dar, hatatoka mtu – hata helikopta zitakuwa ndani ya maji – na pale iku hata ghorofa hakuna – hadi mkuu wa nchi atakwenda!

Masikini nchi yangu tanzania, tuchukue hatua.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s