CUF yapokewa kwa shangwe; Mafia

Naibu Katibu Mkuu (Bara) Julius Mtatiro

Jana tarehe 22 desemba 2011 nilifika kisiwa cha mafia(wilaya) salama, niliendelea na ziara ya kichama mkoa wa pwani ambayo inamalizika leo.
Tulipokelewa kutokea uwanja wa ndege wa mafia na mamia ya wafuasi wetu na kisha nikapelekwa ofisi ya mkuu wa wilaya kusaini kitabu cha wageni then nikaenda ofisi ya wilaya na kufanya kikao cha ndani na kina mama halafu kikao cha pili na wazee ukumbini kikifuat…iwa na mkutano mkubwa wa hadhara ulohudhuriwa na wananchi mbalimbali.

Baada ya mkutano tulipumzika kidogo kabla ya kuingia kwenye kikao cha ndani na vijana wa mafia. Asubuhi hii naongea na kamati ya utendaji ya wilaya kwa kikao maalum kisha nitarudi dar tuje kuzikawenzetu waliopoteza maisha kwenye mafuriko na kuathirika.

Hapa mafia serikali ilibomoa uwanja wa ndege mwaka 1982 kwa ahadi za kujenga mwingine haraka, cha ajabu ni kuwa hadi leo mwaka 2011 serikali imeshindwa kujenga uwanja. Pana kijibarabara cha vumvi tu ambapo ndege hutua. Timesubutu, timeweza na tinasonga mbele!

Hapa mafia fedha za kujenga gati zilitengwa lakini kwa sababu ya wizi mtupu zikaliwa, hadi leo hii gati limewashinda kujenga wakati hiki ni kisiwa(gati ni bandari) – timesubutu, timeweza…….

Hapa mafia sehemu kubwa ya wananchi wanategemea uvuvi ili kuendesha maisha yao, cha ajabu ni kuwa, serikali imewafukuza wavuvi wasivue katika maeneo yenye samaki wengi, inawalazimisha wakavue kwenye high sea wakati hawana vitendea kazi vya hali ya juu.
Kinachotokea ni kwamba wengi wao wanakosa samaki na wamekata tamaa, uvuvi sasa ni shughuli pevu.
Nimekutana na mvuvi mmoja jana anaitwa masud omar, akawa analia kama mtoto, nami machozi kidogo yanitoke.

Anasema wiki ilopita alinyang’anywa kila kitu na askari wa hifadhi na hivi sasa hajui aanzie wapi – eti kisa alikutwa akivua katika maeneo ambayo yamekatazwa.

Swali la kujiuliza, ni kwa nini wawekezaji wakubwa wanaruhusiwa kuvua katika maeneo yaliyokatazwa kwa vipindi maalum huku wazawa wakipigwa marufuku ya milele?

Leo katika nchi hii kuna ubaguzi wa wazi, mtu alizaliwa akakuta mababu na mababu zake wanavua, naye anaanza kuvua kwa sababu serikali imeshindwa kumpa elimu ya maana, mwisho wa siku hata huu uvuvi – the only tool to run his life- nayo inachukuliwa kwa nguvu. Je watu wajinyonge kama masud omar wa mafia.

Tunawekeza juhudi za dhati katika jimbo hili, mwaka jana CUF tulizidiwa kura 1200 na CCM kwenye ubunge, nina jukumu la kuongeza nguvu na mikakati ili kuwakomboa wananchi hawa 2015.

Nitarudi dar baadaye na kwa wale ambao hatukuwa tumetakiana krisimasi njema basi nitumie fursa hii kuwa-wish MARRY CHRISTIMAS!!!!
Japo wenzetu mafia wanasheherekea krisimasi wakiwa na hali mbaya mno!
_______________________________________________
By Julius Mtatiro,
Naibu katibu Mkuu wa CUF (Bara)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s