CUF yaifunika Uzi

  • Vijana 142 wajiunga na CUF
  • Shangwe, nderemo mji mzima

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Sheria na Mahusiano na Umma, Salim Bimani (katikati) akizungumza na watu wa Uzi.

Na Said Hamad Kombo, CUF Makao Makuu

Nianze kwa kuelezea ‘uwezo wa kukubali’ kwa kiumbe kiitwacho binaadamu. Uwezo huu hutofautiana sana katika jamii za watu, na pengine hata kupelekea kuwa ni sehemu ya tabia za binadamu huyo.

Lakini kiujumla uwezo wa binadamu wa kukubali fikra mpya au kuwa mgumu kuzikubali, husababishwa na hali mbali mbali ambazo kiudhati si miongoni mwa ila ama tabia mbaya kwa binadamu, bali ni utofauti unaoweza kututofautisha kimawazo, kimtazamo na kushindana kifikra.
Moyo umenisukuma kutoa ufafanuzi huo baada ya kuona upepo wa kisiasa katika visiwa vya Unguja umebadilika sana.

Msomaji anaweza kujiuliza ni kwa nini sikuitaja Pemba!!? Ni kwa sababu tokea awali kilipoasisiwa Chama Cha Wananchi- CUF hapo mwaka 1992, Pemba imekuwa ng’ome imara ya Chama hiki jambo ambalo Chama Tawala (CCM), licha ya nguvu za dola walizokuwa wanazitumia, ikiwemo  kufanya fujo na ghasiya katika chaguzi za 1995, 2000 na 2005, wameshindwa kupata ushindi hata katika jimbo moja.
Inaonekana wazi sasa wakati wa CUF kuzibomoa ngome za CCM kisiwani Unguja umewadia. Hii ni kwa sababu kipindi kirefu CUF ilikuwa ikizuiwa kwa nguvu za dola kuingia katika ngome za CCM.

Hivi karibuni, kwa mara ya kwanza tokea kuasisiwa kwa vyama vingi vya siasa Tanzania, CUF imefanikiwa kuingia katika jimbo la Donge, Kaskazini Unguja, na kufungua matawi yake huku kikipokelewa kwa shangwe kubwa.

Kabla ya Maridhiano na kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, CUF ilikua ikisambaratishwa kwa kutumia mabomu na risasi za moto, kila pale ambapo inapanga kufanya mkutano wake katika jimbo hilo la Donge.

Siku ya Jumanne,  tarehe 20 Disemba 2011, CUF iliinia na ‘kuiteka’ Uzi, kisiwa ambacho kipo katika vijiji vinavyodaiwa ni ngome za CCM. Hali imedhihirika wakati vijana na wazee wapatao 142 walipochukua kadi za uanachama na kujiunga na Chama hiki.

Ziara hii iliongozwa na Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari na Uenezi, Mhe. Salim Bimani, pamoja na Mlezi wa Vikundi vya Utamaduni vya CUF, Bi Khadija Salum Ali.
Katika ziara hii kulikua na vifijo, nderemo na kila aina ya shangwe vilivyofanya mji mzima wa Uzi kutetemeka kwa hamasa na furaha. Ilianza na maonyesho ya vikundi vya sanaa na kuhitimishwa kwa kukabidhiwa vifaa vya michezo (jezi pea mbili na mipira) kwa vilabu viwili vya mpira wa miguu baada ya mchezo wa kirafiki uliochezwa mbele ya mgeni rasmi.
Wananchi wa Uzi wametoa ujumbe wao kwa mgeni rasmi, Salim Bimani, aufikishe kwa Katibu Mkuu Taifa, Maalim Seif Sharif, kuwa wao wamechoshwa na ahadi za CCM za kila mwaka na sasa watahakikisha kuwa wana-Uzi wote pasi na kubakia hata mmoja, wanajiunga na CUF. Haya yalisemwa katika utenzi maalum wa watu wa Uzi uliosomwa na Ustadh Omar, msanii mwenye kipaji cha kughani kwa ghibu.

Watu wa Uzi waliongeza kusema kuwa CUF ndio Chama pekee chenye mwelekeo wa kuikomboa Zanzibar kutokana na hali ngumu ya maisha. Kwa taarifa nilizozipata ni kuwa vijiji jirani ya Uzi, ambavyo vinadaiwa kuwa na wafuasi wengi wa CCM, tayari vimeshapeleka maombi kwa CUF ili wafanyiwe mkutano wa hadhara na mgeni rasmi awe Katibu Mkuu wa CUF Taifa na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif.
Hali hii inadhihirisha wazi kuwa Wazanzibari, karibu wote, sasa wameshaujua ukweli kuwa CUF ndio chama kinachostahiki kuiongoza nchi yetu, licha ya kuwepo kwa CCM ambao siku hadi siku imani yao inaelekea kwa CUF. Ni wazi hili linatokana na uongozi makini wa Maalim Seif unaolenga kuwaunganisha Wazanzibari wote.

_____________________________________________________
HAKI SAWA KWA WOTE

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s