Vyama vingi sio ugomvi – Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Njinjo kaskazni mwa wilaya ya Kilwa akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne katika Mkoa wa Lindi.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema mfumo wa vyama vingi haukuja kwa lengo la kuwagombanisha wananchi bali kushindanisha sera ambazo zinalenga kuwaletea wananchi maendeleo.

Amesema vyama vyote vya siasa vina lengo moja la kuleta maendeleo kwa wananchi na hivyo hakuna sababu kwa wananchi kugombana kutokana na itikadi za vyama, isipokuwa kupima sera za vyama ili kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua chama chenye mwelekeo wa kujali maslahi ya wananchi.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ametoa changamoto hiyo leo katika kijiji cha Njinjo kilichoko kaskazini mwa Wilaya ya Kilwa alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara uliowajumuisha viongozi wa Mkoa wa Lindi na vyama vya CCM na CUF.
Amesema Wilaya ya Kilwa yenye majimbo mawili ya uchaguzi moja likiwa chini ya CCM na jengine CUF, inaweza kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa upande wa Tanzania Bara kutokana na mashirikiano mazuri yanayooneshwa na viongozi wa kisiasa katika Wilaya hiyo.
“Siasa si ugomvi bali ni maendeleo” alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa wakati siasa za malumbano sasa umekwisha na yeyote mwenye lengo la kuleta vurugu atafute nchi nyengine aende kwani Tanzania inajivunia amani iliyopo, ambayo imekuwa mfano kwa nchi za Afrika.
Amefahamisha kuwa upo uwezekano wa kupingana bila kupigana ikiwa vyama vya siasa vitaweka mbele maslahi ya taifa na kuondokana na tama binafsi zisizojali maslahi ya raia.
“Wapo wenzetu wanasema eti CUF ni CCM ‘B’ kwa kuwa kule Zanzibar tumeshirikiana kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wao walitaka siku zote wazanzibari tuendelee kuuwana? Alihoji.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais amesema katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Zanzibar inatarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kuwawezesha zaidi ya nusu ya vijana wa Zanzibar kupata ajira katika serikali na taasisi binafsi.
Amesema ndani ya kipindi hicho Serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa barabara zote za vijijini sambamba na kuliondoa kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote ya Zanzibar.

 

Kabla ya mkutano huo Maalim Seif aliweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji cha Kipindimbi Wilaya Kilwa na kuahidi kuchangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia umalizaji wa jengo hilo ambalo tayari limeshaezekwa.
Amesema wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu kufuata huduma za afya zaidi ya kilomita kumi (10), hali ambayo imekuwa ikisababisha vifo hasa kwa akina mama na watoto, na kutaka jengo hilo limalizwe haraka ili liweze kutoa huduma.
Viongozi mbali mbali wameahidi kuchangia ujenzi wa jengo hilo akiwemo Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM) Mheshimiwa Mumtadha Mangungu ambaye ameahidi kuchangia tani tatu za saruji ambapo Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF) Mhe. Suleiman Bungala (Bwege) ameahidi kuchangia tani mbili za saruji, huku halmashauri ya Wilaya hiyo ikiahidi kukamilisha kabisa jengo hilo na kulikabidhi kwa wananchi mwaka ujao.
___________________________________________________
Habari na Hassan Hamad,

Picha na Salmin Said

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s