Maalim Seif atoa ovyo kwa wachafuaji chama.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara na wachangiaji wakuu wa Chama hicho katika hala ya chakula cha usiku iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza wachangiaji hao huko hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaa

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF)Maalim Seif Sharif Hamad amesema Chama hicho kiko imara na kimejipanga kukabiliana na mtu yoyote atakayejaribu kukichafua. Amesema licha ya Chama hicho kuandamwa na kusemwa vibaya kupitia vyombo mbali mbali vya habari katika siku za hivi karibuni, lakini bado hakijayumba na kinaendelea kuimarika siku hadi siku.

Maalim Seif alieleza hayo katika hoteli ya Lamada Jijini Dar es Salaam wakati akijumuika na baadhi ya wafanyabiashara na wachangiaji wa Chama Cha CUF kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza wachangiaji hao kwa michango yao iliyosaidia sana kufanikisha uchaguzi mkuu wa 2010 kwa chama hicho.
Chama hicho amesema kinategemea zaidi michango ya wahisani ikizingatiwa kuwa kinajiendesha kwa kutegemea zaidi ruzuku kutoka serikalini, na kuwaomba wasichoke katika kukichangia chama hicho ili kiweze kutimiza malengo yake.
“Bila ya michango yenu tusingefikia hatua hii na tunathamini sana michango yenu muendelee kukiunga mkono chama chetu”, Maalim Seif aliwaasa wafanyabiashara hao, na kuongeza “uchaguzi ni gharamana hivyo lazima tukubali kugharamika, na maandalizi yake ni vyema yakaaza sasa kidogo kidogo kwa ajili ya chaguzi zijazo”, alisema.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyabiashara na wachangiaji hao, mmoja kati ya wafanyabiashara hao Bw. Juma Ahmed Juma amekiomba Chama hicho kubuni miradi zaidi ya kiuchumi ili kiweze kujiongezea kipato na kuendesha shughuli zake vizuri.
Mfanyabiashara huo amemuhakikishia Maalim Seif kuwa bado wafanyabiashara hawajachoka kukichangia chama hicho na wataendelea kufanya hivyo kadiri uwezo utakavyoruhusu.

“Tunafahamu kuwa wafanyabiashara ni chachu ya kukichangia chama na tutaendelea kufanya hivyo kwa kadiri ya uwezo utakavyoturuhusu” alisema Mfanyabiashara huyo ambaye aliwawakilisha wenzake katika hafla hiyo.
Bw Juma pia alitumia fursa hiyo kuelezea juu ya kero mbali mbali zinazowakabili wafanyabiashara wa bara na visiwani na kuomba zitafutiwe ufumbuzi kwani kuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara kutamnufaisha kila mtu wakiwemo wafanyabiashara wenyewe na wananchi kwa jumla.

_________________________________________________________________
Habari na Hassan Hamad

Picha na Salmin Said (OMKR).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s