Afya ni kipaumbele katika serikali yetu – Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Hoteli Tatu wilayani Kilwa maara baada ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji hicho. Aliyekaa ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Ludovick Mwananzila

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya afya kutokana na umuhimu wake kwa jamii katika kuchangia maendeleo ya wananchi na taifa kwa jumla. Kauli hiyo imetolwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akingumza na wananchi wa kijiji cha Hoteli tatu Wilaya ya Kilwa, mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji hicho.

 
Amesema taifa lenye maendeleo linategemea sana afya ya watu wake ambao ndio nguvu kazi, na ndio maana serikali imeandaa mpango maalum wa kuisogeza huduma hiyo kwa jamii kwa kujenga vituo vya afya karibu na makazi ya wananchi ili kuwaondoshea usumbufu.

Maalim Seif ameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupeleka madaktari na wa uguzi wenye sifa mara kituo hicho kitakapokamilika ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi wa eneo hilo ambao wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu kutokana na kufuata huduma hiyo masafa marefu.

Aidha amewaasa wananchi wa kijiji hicho kuvitumia vituo vya afya kwa kupata matibabu sahihi, badala ya kuendelea kuwatumia waganga wa kienyeji ambao wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwa kujaribu kuwapatia matibabu bila ya kutumia vipimo vyovyote.

“Wakati wa kwenda kwa mganga ukapiga bao (yaani ramli) umepita sasa, huu ni wakati wa sayansi na teknolojia, tafadhalini tumieni vituo vyenu vya afya kujitafutia matibabu”, aliasa Maalim Seif ambaye aliahidi kuchangia shilingi milioni moja kusaidia zahanati hiyo iweze kukamilika kwa haraka na kutoa huduma kwa wananchi.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Bwana Noordin Hassan Babu amewapongeza wananchi wa kijiji cha Hoteli tatu kwa kubuni mradi wa kujenga zahati hiyo ambao ni muhimu kwa maendeleo yao.

Amesema serikali inaunga mkono juhudi hizo zinazoanzishwa na wananchi ikiwa na lengo la kujenga zahanati katika kila kijiji, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa wananchi.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Hoteli Tatu wilayani Kilwa baada ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji hicho. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Ludovick Mwananzila na kulia ni mfuasi wa CUF na mfuasi wa CCM.

Wakati huo huo Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye yuko Wilayani Kilwa kwa ziara ya siku nne alitembelea shughuli za Chama hicho na kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya CUF kata ya Kipatimu na kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Chumo.

Akizungumza na wanachama na wananchi wa vijiji hivyo, Katibu huyo Mkuu wa Chama Cha CUF amesema Chama hicho bado ni chama cha upinzani bara na visiwani, tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya watu kuwa kimekuwa CCM ‘B’.

Amesema kuingia katika serikali kwa chama hicho haina maana kuwa kimegeuka kuwa CCM na kufafanua kuwa kila chama kina sera zake.

“Hatujaunganisha vyama, kila chama kina sera zake, nataka mfahamu wananchi wa Chumo kuwa CUF imeamua kuingia katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kwa lengo la kunusuru maisha ya wanachi, na huu ndio mfumo unaotumika katika nchi mbali mbali sasa kwa vya kushirikiana kuunda serikali. Sio jambo la ajabu kabisa. Hivi hawa jamaa zetu wakitaka sisi kule Zanzibar tuendelee kuuwana kila siku? Alihoji.

Amewata wananchi wa vijiji hivyo kukiunga mkono Chama Cha CUF ili kiweze kuwaletea maendeleo ya haraka kwa kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili ikiwa ni pamoja na kuangalia maslahi ya wakulima wa zao la korosho na ufuta kama ilivyofanywa kwa wakulima wa zao la Karafuu visiwani Zanzibar ambao wakipandishiwa bei kutoka shilingi 3000 hadi 15,000 kwa kilo.

_______________________________________________________________

Habari na Hassan Hamad. Picha na Salmin Said (OMKR)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s