Msiwabeze Wabunge wenu-Maalim Seif.

Mbunge wa jimbo la Mgogoni, Kombo Khamis akimkabidhi funguo za gari mbili, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo, makabidhiano hao yaliofanyika huko Micheweni Pemba

Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) katika majimbo ya Micheweni, Mgogoni na Tumbe, Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba wametoa magari sita kwa wananchi wa majimbo hayo yatakayotumika kusaidia shughuli za kijamii na maendeleo katika maeneo yao.

Magari hayo yenye thamani za zaidi ya shilingi milioni 90 yamekabidhiwa kwa viongozi wa mamjimbo hayo na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharifa Hamad katika sherehe maalum ya makabidhiano zilizofanyika katika eneo la Micheweni kisiwani Pemba.
Wabunge waliotoa magari hayo ni Haji Khatib Kai wa jimbo la Micheweni aliyetoa magari mawili kwa ajili ya jimbo lake, Kombo Khamis Kombo wa jimbo la Mgogoni aliyetoa magari mawili pamoja na Mbunge Tumbe, Rashid Ali Abdallah ambaye pia alitoa magari mawili kwa ajili ya matumizi ya jimbo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kukabidhi gari hizo kwa viongozi wa majimbo, Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad aliwapongeza viongozi hao kwa kukamilisha ahadi walizotoa kwa wananchi katika maeneo yao.
Alieleza kuwa hatua ya Wabunge hao kutekeleza ahadi ni ya kiungwana na viongozi wengine wa chama hicho, wakiwemo Wabunge na Wawakilishi hawanabudi kufuata nyayo hizo, kwasababu unapoahidi na badala yake usitekeleze unakuwa na sifa za mtu mnafiki.
Alieleza kwamba kama Wabunge hao wameweza kutekeleza ahadi kubwa kama hizo katika kipindi cha mwaka mmoja, basi matarajio yake wataweza kutimiza ahadi zote walizoahidi kwa wananchi wakati walipowaomba wawachague kuwaongoza.

Aliwataka wananchi wa majimbo hayo kushukuru na kuwaunga mkono viongozi hao, kwa hatua hiyo kubwa ya kununua magari kwa ajili ya matumizi ya wananchi, wakielewa kuwa tabia ya kushukuru ndiyo ya kiungwa na ya kibinaadamu, pale mtu anapofanyiwa jambo la kheri na lenye maslahi kwake.
“Nakuombeni wananchi wa Micheweni, Mgogoni na Tumbe muwashukuru Wabunge na Wawakilishi wenu kwa kutekeleza ahadi, kama huwezi kumshukuru binaadamu mwenzake huwezi kumshukuru hata Mwenyezi Mungu”, alisema Maalim Seif.

Maalim Seif aliwataka wananchi hao wawapuuze watu wanaowaponda Wabunge wao kwa madai hawajafanya kitu, kwa kile alichosema madai hayo sio kweli na mambo wanayoyafanya ni makubwa na wananchi wenyewe wanayashuhudia. Wakizungumza baada ya makabidhiano hayo, Wabunge hao walisema magari hayo ni miongoni mwa ahadi nyingi walizokwisha tekeleza katika kipindi cha mwaka mmoja tangu wachaguliwe, na kuahidi wataendelea kuwatumikia wananchi na kuhakikisha shida zinazowakabili zinapatiwa ufumbuzi.

Mbunge wa Tumbe, Rashid Ali Abadallah alisema baada ya wao kutoa magari hayo, hakuna sababu kwa watendaji wa chama hicho kushindwa kufuatilia kazi za chama na na shida za wananchi kwa kisingizio cha kukosa usafiri au mafuta.
Aidha, alisema kwamba hatarajii kusikia malalamiko kutoka kwa akinamama wajawazito kwamba hawana gari za kuwapeleka hospitali wanapohitaji kujifungua.

Aliwahimiza kutumia usafiri kwenda hospitalini na kuachana na tabia ya kujifungulia majumbani, kwasababu ni hatari kwa maisha ya akinamama na watoto wanaozaliwa.
Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif pia katika mkutano huo, aliwaeleza wananchi wa Micheweni juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya saba katika kuimarisha maisha ya wananchi wote wa Unguja na Pemba, ambao idadi kubwa wanafanya shughuli za kilimo, kazi za maofisini, uvuvi na ufugaji.

Kuhusu kilimo cha mwani ambapo Micheweni kuna idadi kubwa ya wananchi wanaofanya kazi hiyo, Maalim Seif alisema matarajio ya serikali wafanyabiashara wanaonunua zao hilo watapandisha bei, kwa vile uwezekano huo upo kwa mujibu wa bei wanayouzia katika soko la kimataifa.

Maalim Seif alisema serikali tayari imewakumbusha wafanyabiashara hao mara kadhaa, ili wapandishe bei angalau wanunue kilo kwa shilindi 1000 kutoka bei ya sasa ya shilingi 400, ili bei hiyo iende sambamba na kazi kubwa anayopata mkulima katika uzalishaji mwani hadi kuuza.

Lakini alionya iwapo wataendelea kuwapunja wakulima, serikali haitasita kulitaka Shirika la Biashara la Taifa ZSTC kununua mwani kutoka kwa wakulima, kama inavyofanya kwa zao la karafuu.

________________________________________________________________
Habari na Khamis Haji,

Picha na Salmin Said (OMKR)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s