Moyo awakoromea wanaovuruga maridhiano.

Mzee Hassan Nassor Moyo

Mzee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hassan Nassor Moyo, ameishauru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutowaonea haya viongozi ndani ya serikali wanaopinga maridhianona umoja wa Wazanzibari na wawatimue maramoja serikalini, ili Zanzibar iendelee kubaki katika amani na utulivu.
Mzee Moyo alisema kwamba haikuwa kazi rahisi kuleta maridhiano na hatimaye amani na utulivu unaodumu hadi sasa Wazanzibari wana adhimisha mwaka mmoja wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo katika mfumo wa Umoja wa Kitaifa baada ya kupita katika miaka mingi ya chuki uhasama.
Alisema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya maridhiano ya mwaka mmoja wa serikali ya umoja wa kitaifa, yaliyofanyika katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, amabapo wasanii walitoa bururdani na kuwatunuku nishani ya kudumisha amani, Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad , na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume.

Alieleza kwamba vizazi vya sasa Zanzibar havitakiwi kuona mivutano na ugomvi kama ilvyokuwa ikijitokeza Zanzibaar kabala na baada ya Mapinduzi na tokea kuja kwa mfumo wa vyama vingi, na hivyo viongozi wanaotaka kuirejesha nyuma Zanzibar hawafai na watimuliwe Serikalini kwa nia ya kuhakikisha Wazanzibari wnaendelea kubaki katika hali ya ushirikiano.

“Umoja na maelewano tuliyonayo Wazanzibari si jambo la kufanyiwa mzaha, nakwambieni viongozi tuliokukabidhini madaraka ya kulinda amani ya Zanzibar, viongozi wanao pinga maelewano haya msiwavumilie waondoeni”, alisema mzee Moyo.

Mzee wa Chama Cha Mapinduzi, Hassan Nassor Moyo akimkabidhi tunzo ya nishani Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika hafla hiyo, alisema inawezekana wapo watu wanaopinga umoja na maelewano ya Wazanzibari, lakini hadi sasa hawajajittokeza hadharani na wanaumia ndani ya mioyo yao.

Maalim Seif alisema wakitokea watu kama hao , serikali haiwezi kuwavumilia kwa vile wananchi wa Zanzibar hawako tayari kurudi nyuma kwenye uhasama, baada ya kupata neema kubwa ya maelewano na kuanza kushuhudia dalili njema za mafanikio.

“Hatukubali kurejeshwa nyuma tulikotoka,, akitokea mtu anapinga maridhiano yetu Wazanzibari hawawezi kukubali na tutamshughulikia, kwa sababu katika kipindi kifupi cha maelewano na serikali ya Umoja wa Kitaifa tumeanza kuona mafanikio makubwa”, alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema kazi kubwa na muhimu iliyofanywa na mzee Moyo na baadhi ya viongozi kutoka CCM na CUF na hatimaye kuzaliwa maridhiano ya kisiasa Novemba 2009 ni ya kupigiwa mfano na lazima waingie katika historia.

Aliwataja baadhi ya viongozi kutoka vyama hivyo ambao walibeba jukumu la kufanikisha mazungumzo ya awali hadi Maalim Seif kukutana na rais Mstaafu karume na baadaye Maridhiano kupokelewa na Wazanzibari wote kuwa ni Ismail Jussa, Salum Bimani, Abubakar Khamis Bakary, Mansour Yussuf Himid, Edi Riyami, ambao waliongozwa na Mzee Moyo kufanikisha kazi hio muhimu.
Alisema kutokana na kazi hio iliozaa Zanzibar mpya baada ya kushindika miafaka kadhaa tokea baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, hivi sasa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limesema limerikodi hatua zote za kuleta maelewano na kuzitumia kama njia za kuziwezesha nchi nyengine zenye mizozo kuleta maelewano.

Naye balozi wa Norway nchini Tanzania , Igunn Klepsvik alisema nchi yake inaunga mkono maridhiano ya Wazanzibari ambayo yametoa njia kwa Zanzibar kuweza kupata maendeleo na kuinua hali za maisha ya Wananchi.

Alisema Norway imeamua kufadhili maadhimisho ya maridhiano ya Zanzibar kwa njia ya miziki na burudani, kwa vile sanaa hizo ndio njia muhimuya kutoa sauti moja inayo wafikia wengi na kuwasilisha ujumbe wa amani, umoja na mshikamano.

Katika hafla hiyo wasanii wa taarab kutoka Unguja na Pemba walitoa burudani na baadaye kumtunuku nishani, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamadambayo alikabidhiwa na mzee Hassan Nassor Moyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s