Maridhiano yampatia nishani ya Ushujaa Maalim Seif

Maalim Seif akipokea nishani kutoka kwa Mzee wa Chama Cha Mapinduzi, Hassan Nassor Moyo Gombani Chake Chake Pemba kutokana na ushujaa wake wa kuasisi na kufanikisha maridhiano yaliyofikiwa miaka miwili iliyopita iitwayo Shujaa wa Zanzibar.

Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amepewa tunzo iitwayo ‘Shujaa wa Zanzibar kutokana na mchango wake mkubwa wa kuasisi Maridhiano yaliofikiwa Novemba 5 2009 huko Ikulu mjini Zanzibar kati yake na Rais wa Zanzibar wa wakati huo Amani Abeid Karume.

 Nishani hiyo imetolewa na wasanii wa Swahili Center Zanzibar, Maalim Seif alikabidhiwa nishani hiyo na Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi, Mzee Hassan Nassor Moyo ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa mstari wa mbele katika kuyasukuma maridhiano hayo.

Kusudio la nishani hiyo ilikuwa ni kuonesha ‘appreciation’ kwa niaba ya wasanii wa Zanzibar ambao wamefurahishwa na hali ya maelewano yaliyopo Zanzibar sasa na hivyo kuwa na matumaini makubwa ya maendeleo ya sekta yao ya Sanaa za Utamaduni. 

Nishani aliyotunukiwa imepewa utambulisho wa “Shujaa wa Zanzibar”. Aidha ilitegemea kutolewa zawadi hizo mbili kwa watu waliofanikisha kwa kisi kikubwa ambapo zawadi kama hiyo ilipangwa kupewa Dr. Karume katika sherehe hiyo iliyofanyika Gombani na kuhudhuriwa na mamia wananchi mbali mbali lakini kutokana na Dr Karume kudharurika imepangwa nishani yake kupew asiku nyengine.

Katika hatua nyengine Mzee Hassan Nassor Moyo ameishari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumfukuza kazi kiongozi yeyote atakae pinga suala la maridhiano yaliofikiwa hapa Zanzibar baina ya vyama vya CCM na CUF na kuwepo kwa amani ya kudumu.

Alisema kuwa kwa vile Zanzibar imepita katika misukosuko mingi ya kisiasa na kusababisha mauwaji miongoni mwa wananchi na viongozi huku hasama na chuki zikiwa zimetanda kwa miaka kadhaa hadi kupatikana kwa amani na utulivu hivi sasa hakuna budi kuungwa mkono na kila mtu na iwapo akijitokeza kiongozi akipinga au kubeza juhudi hizo za maridhiano afukuzwe kazi.

Moyo alitoa tamko hilo jana huko Uwanja wa Michezo Gombani Chake chake Pemba mbele ya Makamu wa Kwanza rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kwenye hafla ya ufungaji wa tamasha la 100% Zanzibari baada ya ya kumaliza kambi yake kwa muda wa miezi miwili.

Alieleza kuwa tokea Zanzibar ijitumbukize kwenye mfumo wa vyama vingi nchi imekosa amani na utulivu hadi kufikia wananchi wenyewe kwa wenyewe kutosaidiana mambo ya kheri kama vile mazishini, harusini jambo lilikuwa likichnagiwa kwa kiasi kikubwa na siasa za chuki na hasama zilizojikita kwa miaka kadhaa ambapo wazanzibari walisahau silka na mila zao za udugu na kuishi pamoja.
‘’Leo hii tunamshukuru Mwenyeenzi Mungu tunaishi vyema na kwa salama na amani na tunafanyiana mambo yetu kama asili yetu sasa akitokezea kiongozi anataka kuturejesha tunakotoka mfukuzeni maana huyo hatufai’’.alisisitiza Mzee Moyo ambaye ni Mzee wa Chama Cha Mapinduzi.

Mzee Moyo alisema pamoja kuheshimu na kuyaenzi maridhiano ya Zanzibar, amewaomba wananchi wa Zanzibar kuendelea kuwathamini na kuwaheshimu waasisi wa mwafaka huo Maalim Seif Sharif Hamad na rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume.

Mapema akizungumza kwenye hafla hiyo Balozi wa Norway nchini Tanzania Ingunn Klepsvik amepongeza hatua ya kufikia mwafaka hasa kutokana na kutosimamiwa na mataifa ya nje lakini yameweza kuleta sura halisi ya umoja na mshikamano na kuziomba nchi nyengine kuiga mfano wa maridhiano ya Zanzibar ambayo yameafikiwa na wazanzibari wenyewe.

Balozi huyo alieleza kuwa sio mataifa mengi duniani ambayo yana ujasiri wa kukubaliana wenyewe kwa wenyewe hasa baada ya kutengana kwa muda mrefu na kutokezea mapigano na uhasama kama ilivyotokea kwa Zanzibar.

Nae Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kukabidhiwa nishani ya ushujaa kwa kuipeleka nchi kwenye amani ya kudumu amesema hadi sasa hajajitokeza mtu yoyote kupinga maridhiano hayo hadharani na kuwaomba wazanzibari kuyaunga mkono maridhiano hayo ili amani ya kudumu iendelee kuwepo daima.

Aliongeza kuwa inawezekana wapo wanaopinga maridhiano hayo lakini wamekuwa wakiumia ndani ya moyo wao na hawawezi kujitokeza kwa vile hakuna atakaemuunga mkono kwani wazanzibari asilimia kubwa wamekubaliana na mfumo wa serikali ya umoja kutokana na kuchoshwa na uhasama na chuki zilizokuwepo awali zilizosababishwa na mfumo wa kisiasa.

Hata hivyo Maalim Seif aliongeza kuwa nishani aliokabidhiwa na wasanii wa Zanzibar sio ya kwake pekee bali ameipokea kwa niaba ya Wazanzibari wote kwa vile katika hilo washindi ni wanzibari wenyewe ambao wameunga mkono kuwepo kwa maridhiano baada ya kupiga kura ya ndio ya kutaka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s