Maalim Seif atoa somo Pemba.

Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif hamad

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ameendeleza ziara zake kisiwani Pemba zenye lengo la kuimarisha Chama na kutoa maelezo kwa wananchi kuhusu mambo mbali mbali yanayohusiana na nchi.

Katika hilo ameyatembelea majimbo yote matano (5) ya Wilaya ya Wete (Jimbo la Mtambwe, Wete, Gando, Kojani na… Ole) na kuweza kuzungumza na viongozi na wananchi wa maeneo hayo. Mwisho wa ziara yake ilikua ni jana tarehe 5/12/2011 ambapo alifanya mkutano wa hadhara katika wilaya ya Micheweni na Mkoani.

Maalim Seif amezungumzia changamoto zilizoikabili serekali ya Zanzibar na mafanikio yaliyofikiwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Alisema mafanikio hayo hayakupatikana katika kipindi chote cha awamu tofauti zilizopita kuiongoza Zanziabar tangu kuanza kwa uchaguzi wa 19995.

Amesema amani iliyopo sasa ni hazina kubwa na inahitaji kutunzwa na kulindwa. Kuongezwa kwa mishahara sambamba na marupurupu yote ya nyongeza, vienua mgongo na pesa za likizo ambazo haijawai kupandishwa kama ilivyo sasa. kuongezwa bei kwa zao la karafuu pia alisema ni moja katika mafanikio ya serekali ya Umoja wa kitaifa.

Licha ya hayo lakini hakuacha kuuzungumzia mfumko wa bei za vyakula ambao umekua ukirejesha nyuma jitihada za serekali za kuwapunguzia ugumu wa maisha wananchi wake. Aidha amesema kupanda huko kwa bei kumesababishwa na hali tofauti zilizojitokeza; ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania (kuongezeka kwa gharama za ununuzi wa bidhaa kutoka nje) na kutokea mafuriko kwa nchi wazalishaji wakuu wa mchele jambo ambalo limepelekea wao badala ya kuuza sasa wananunua mchele kwa ajili ya watu wao.

Jambo hili limepelekea kuongezeka kwa mahitaji ya mchele duniani wakati uzalishaji umepungua. Mfano, nchi ya China ambao jumla yao ni watu bilioni 1 na milioni 5 (1.5 Billion), India ambao ni bilioni 1 na milioni 2 (1.2 Billion), mbali izo nchi nyengine za Asia ambao wote wanatumia mchele kama chakula chao kikuu. Jumla ya idadi hii inafikia nusu ya watu wote duniani wanaohitaji mchele kwa chakula cha kila siku; tukiwemo sisi Zanzibar.

Upandaji wa bei za vyakula, amesema Maalim Seif, umetokana pia na uvamizi wa meli unaofanywa na maharamia wa kisomali umechangia kwa kiasi kikubwa, kwani sasa wanaoagizia bidhaa inawalazim kusafirishia katika meli kubwa ambazo haziwezi kuvamiwa kiurahisi, na gharama zake ni kubwa zaidi.

Kwa upande wa sukari, nchi ya Brazil ambayo inazalisha sukari kwa wingi sasa imeamua kuzalisha Spirit kwa sababu kwao inawaigizia faida kubwa zaidi. Hata hivyo serekali haikuacha kuzungumza na wafanyabiashara wanaoingiza chakula na kukubaliana bei ya kuuza bidhaa zao kulingana na ghamara zao.

Katika ziara hizi, Makamo wa Kwanza wa Rais amekuwa akiwanasihi Wazanzibari kwa ujumla kujitokeza kwa wingi sana katika kutoa maoni yao kuhusu katiba. Amesema huu ndio wakati ambao Chama chake kilikuwa kinaupigania tangu kuasisiwa kwake hadi leo hii, akisisitiza kuwa hapa ndio pahala pake kwa Wazanzibari kuamua juu ya mustakbali mzima na muhimu kwa nchi yao.

Amewataka wananchi wajiskie huru, bila ya kushawishiwa katika kusema kile wanachokitaka.

___________________________________________________

Na Afisa Utafiti na Sera, CUF (Makao Makuu – Zanzibar)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s