Kikwete asifiwa kuheshimu hadhi ya Z’bar

—Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) akihutubia mkutano wa wanakijiji cha Mchangani Jimbo la Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja

WAKATI Tanzania inajiandaa kutunga Katiba mpya, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema umoja na sauti moja ndio silaha pekee ya kuwawezesha Wazanzibari kulinda maslahi ya Zanzibar ndani ya serikali ya Muungano.

Alisema kukosekana kwa msimamo huo kutawakosesha kutumia vema fursa muhimu ya kujadili na kutetea kwa umakini mahitaji ya Zanzibar katika Katiba mpya, tume ya kuratibu maoni itakapoanza kazi hiyo rasmi baada ya kuundwa na Rais Jakaya Kikwete.

Maalim Seif alitoa changamoto hiyo katika kijiji cha Mchangani, jimbo la Donge, wakari wa ziara ya kutembelea matawi ya CUF katika wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kusini Unguja jana.

Alisema anaamini tume itakayoundwa na Rais Kikwete kwa kushauriana na kukubaqliana na Rais wa Zanzibar, itazingatia maoni yao juu ya aina ya Muungano wanaoutaka kwa maslahi ya Zanzibar na wananchi wa visiwa hivyo.
“Baada ya tume ya kuratibu maoni kuundwa, kazi yetu itakuwa kusema tunachotaka na tusichotaka, hakuna kuburuzwa tena, hii fursa tuitumie vizuri, tusahau tofauti za itikadi za kisiasa, tuseme kwa sauti moja kwa faida ya Zanzibar ,” alisema na kusisitiza:
“Tunataka Muungano wenye maslahi kwa Zanzibar , yakiwemo ya kuingia katika masuala ya kimataifa, tukiwa na hadi ya nchi.”

Alisema mfumo wa Muungano uliopo umeminya fursa ya Zanzibar kuingia katika masuala ya kimataifa kwa kisingizio kuwa ni nchi ndogo kijiografia kulinganisha na upande wa Tanzania bara.

Alisema mtazamo huo umechangia Muungano kuwa na kero nyingi kuliko mafanikio na kwamba udogo kijiografia sio kigezo cha Muungano kuikosesha Zanzibar nafasi ya kuingia katika masuala ya kimataifa.

“ Seychelles ina watu laki moja, lakini nafasi yake katika Umoja wa Mataifa inalindwa kama ilivyo kwa nafasi ya China yenye watu bilioni moja,” alisema.
Hata hivyo, Maalim Seif alisema anampongeza Rais Kikwete kwa kutambua hilo na wakati mwingine kulitolea maelezo huko Tanzania bara.

“Nampongeza Rais Kikwete kwa kuwaambia Watanganyika kuiona Zanzibar kama wanavyoiona Tanganyika ,” alisema Maalim Seif.
Juu ya mchakato unaoendelea wa kupata Katiba mpya, Maalim Seif aliswahakikishia Wanzibari kuwa muswada unaosubiri kusainiwa na Rais Kikwete umebeba mambo yote yanayosimamia mahitaji ya Zanzibar .

Aliongeza kuwa kinachotakiwa kwa upande wao ni ushiriki na kutumia uhuru wao katika kutoa maoni juu ya Katiba mpya wanavyotaka iandikwe na kujadili mambo wanayotaka na ambayo hawataki katika Muungano.

___________________________________________
Habari na Charles Mwankenja

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s