Utiaji Saini wa Mkataba wa Muungano na Matokeo Yake {UHARAMU WA MUUNGANO}

Dr Harith Ghassany

“Hapana shaka yoyote kuwa Mkataba [wa Muungano] uliandaliwa kwa siri sana. Maofisa wawili [wa Kiingereza] Brown na Fifoot walihusika kwa karibu sana. Hakukuwa na mshauri wa kisheria kwa upande wa Zanzibar. Karume hakuliarifu Baraza la Mapinduzi. Jumbe alikuwa hajui.

Inawezekana Babu alikuwa anafahamu kuwa kulikuwa kuna kitu kinaendela, na inawezekana alishiriki katika mazungumzo ya kijumla, lakini hakutarajia kuwa Muungano utafanyika kwa haraka namna ile. Salim Rashid [Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi] aliuona Mkataba [wa Muungano] kwa mara ya kwanza pale ‘bahasha yenye Mkataba ulipowasili Ikulu kwa ajili ya kutiwa saini na Karume’.

Karume alimuelekeza Salim asimuonyeshe Dourado ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wa wakati huo. Salim alimuambia Karume kuwa Mkataba wa Muungano ulihitajia ushauri wa kisheria. Salim akapanga kumleta Nabudere, wakati huo alikuwa ni mwanasheria kijana kutoka Uganda ambaye Salim alionana naye London lakini Nabudere alipofika Zanzibar Mkataba wa Muungano ulikuwa tayari umo katika mchakato wa kusainiwa.
Katika mahojiano na muandishi [Issa Shivji], Nabudere alithibitisha kuwa wafuasi wa chama cha Umma, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walimuita ende Zanzibar. Alipofika Zanzibar, aliwekwa peke yake afanye kazi ndani ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Wakati huo, Mwanasheria Mkuu Dourado, alikuwa hayupo.

Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Mzee Abeid Amani Karume

Nabudere alipewa kopi ya Mkataba wa Muungano ambayo ilikuwa bado haijatiwa saini. Alitumia baadhi ya siku kuzipitia nyaraka husika za sheria za Zanzibar na makabrasha mengineyo. Baadae akenda Ikulu kuonana na Karume. Alimuarifu Karume kuwa kimsingi [Muungano] ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa. Utaifa wa Zanzibar utakabwa sana lakini uamuzi wa mwisho wa kisiasa anao yeye Karume.

Karume akasema yeye hana matatizo na Muungano kwa hiyo Nabudere akasema basi atakuwa hana mchango [wa kisheria]. Baadae Karume akashuka chini na Nabudere na kumuambia kuwa Nyerere amekuja kuonana nae. Nyerere alikuwa na Roland Brown. Jumla walikuwepo watu wane. Nabudere akajuulishwa na Nyerere.

Hakukuwa na mazungumzo khasa juu ya Mkataba wa Muungano. Baada ya kidogo, Nabudere akaondoka. Alipotoka nje ya Ikulu aliwaona baadhi ya wafuasi wa Umma waliokuwa wakiupinga Muungano. Nabudere alionana na Babu jioni ya siku ile. Inavyoonsha Babu aliwasili Zanzibar siku hiyo hiyo.

Nabudere alimueleza Babu kuhusu mkutano wake na Karume. Babu akasema kuwa yeye hana matatizo na Muungano. Nabudere akasafiri asubuhi ya siku ya pili au baada ya siku moja.
Nabudere hakuweza kuzikumbuka tarehe za kuwasili na kuondoka kwake Zanzibar. Na hakushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muungano, na wala hakushiriki katika mazungumzo yoyote yale ya Mkataba wa Muungano.

Inawezekana Nabudere alifika Zanzibar siku chache kabla ya Mkataba kutiwa saini. Inawezekana alikutana na Karume tarehe 22 au 23 [Januari], lakini kwa vyovyote hakushiriki katika mazungumzo juu ya Mkataba wa Muungano na wala hakutoa ushauri wowote ule wa kisheria.

Kwa hiyo kauli alioyoitowa Dourado miaka 20 baadae kuwa Zanzibar haikupata ‘ushauri wa kisheria au wa kikatiba kutoka kwa Mwanasheria wake Mkuu’ ni ya kweli.

Pia ni kweli kuwa Karume hakupewa ushauri wowote ule wa kisheria, na inawezekana sana kama ilivoonekana mara nyingi, kuwa alikuwa hajali kuhusu sheria au mambo ya kisheria katika uendeshaji nchi au mambo mengineyo.

Jumbe aliuona Mkataba wa Muungano kwa mara ya kwanza baada ya mawaziri wa Zanzibar kurudi kutoka Dar es Salaam ambako walikwenda kushuhudia kuidhinishwa kwa Mkataba wa Muungano ndani ya bunge la Tanganyika.

Jumbe anasema alimuambia Karume kuwa kulikuwa kuna kitu hakipo barabara. ‘Vipi sisi tunayo serikali lakini Tanganyika haina!’ Jumbe alifanya kama kusema tu. Kama ilivyo kawaida yake, Karume akapuuza: Tutarekebisha baadae.

Prof. Issa Shivji

Kama hawana serikali [ya Tanganyika] si shauri yao wenyewe!
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini Zanzibar tarehe 22 Aprili 1964…Tamko rasmi la safari ya Nyerere kwenda Zanzibar ambayo ilikuwa ni ya mara ya kwanza kutokea kufanyika mapinduzi, ilielezewa kuwa ilikuwa ni ”safari ya heshima.” Safari hiyo ilidumu kwa masaa mawili tu.

Nyerere alikwenda na Ronald Brown na Fiffot. Picha ya utiaji saini [Mkataba wa Muungano] ipo mpaka leo, na inamuonyesha Abdulaziz Twala, Kasim Hanga na Ali Mwinyigogo kutoka upande wa Zanzibar na Oscar Kambona, Job Lusinde na Bhoke Munanka kutoka upande wa Tanganyika.”

Kuuidhinisha Mkataba wa Muungano
Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.

Mkataba wa Muungano ni mkataba wa kimataifa ambao ulitiwa saini na viongozi wawili wa nchi mbili. Katika mfumo wa kisheria wa kawaida ambao unafuatwa na Zanzibar na Tanganyika, mikataba ya kitaifa inahitajia kuidhinishwa na mabaraza ya kisheria ili kuipa nguvu za kisheria.

Kifungu viii cha Mkataba [wa Muungano] kinasema wazi kuwa Mkataba wa Muungano ‘lazima uidhinishwe kisheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na pamoja na Baraza la Mawaziri liidhinishe na liipe nguvu za kisheria Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar’.

Ni muhimu kuwa kifungu hichi hakizungumzi tu juu ya uidhinishaji wa Mkataba wa Muungano bali kinalazimisha sharti juu ya mabaraza mawili kutoka Tanganyika na Zanzibar kuudhinisha na kuupa nguvu kwa ajili ya serikali za nchi zote mbili.

Hilo ndilo khasa lililofanywa na Bunge la Tanganyika. Tarehe 25 Aprili 1964 (ambayo ilikuwa ni siku ya Jumamosi), Rais wa Tanganyika, Julius Nyerere, aliliita bunge kwa ajili ya kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Wajumbe wengi wa Baraza la Mapinduzi walikuwepo wakati Bunge la Tanganyika lilipokuwa likijadili muswada wa sheria mpya wa kuuidhinisha kisheria Mkataba wa Muungano.

Aliusisitiza uhusiano mrefu wa kihistoria baina ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, ambao umeufanya muungano baina yao uwe kama ni kitu cha kawaida.

Pia alitilia nguvu hamu ya watu wa Afrika kuujenga Umoja wa Afrika. Alilitilia mkazo suala la kuundwa kwa shirikisho la Afrika Mashariki na kuwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar hautoziathiri [kwa vibaya] juhudi zao katika kuelekea kwenye Umoja wa Waafrika. Kurasa 82-83.

Wakati mchakato wa kuuidhinisha [Mkataba wa Muungano] kwa upande wa Tanganyika ulifuatwa hatua kwa hatua na ulifuata taratibu kama zinavatakiwa na sheria ya Mkataba wa Muungano, hayo hayawezi kusemwa kuwa yalifuatwa kwa upande wa Zanzibar. Ukurasa 85.

Jumbe na Salim Rashid [Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi] wote wawili hawakubali kuwa kuliwahi kufanywa mkutano wa Baraza la Mapinduzi kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Kwa mujibu wa kiapo aliochoapa Salim Rashid Mahakama Kuu ya Zanzibar, katika kesi ya Rashid Salum Adiy na watu 9 wengine dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu 4 wengine (Nambari 20 ya 2005), ameshuhudia [Salim] kuwa hajawahi kuulizwa na wala hakuwahi kuitisha kikao cha Baraza la Mapinduzi kuudhinisha Mkataba wa Muungano. Hajawahi kuulizwa na hakuwahi kumpa taarifa mwandishi yoyote kuiandika sheria ya kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Ukurasa 89.
“Katika kipindi chote cha utawala wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere, uhakika wa kisheria wa Muungano ulinyimwa jukwaa. Ikionekana ni usaliti kujadili au hata kuutaja Mkataba wa Muungano wa 1964.

Hayati Mwalim julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa vile Mwalimu Nyerere alivimiliki vyombo rasmi vya habari na kwa sababu kulikuwa hakuna vyombo huru, maovu yake makubwa ya uvunjaji wa Katiba hayakuweza kuripotiwa.” Profesa Hamza M. Njozi kwenye dibaji ya kitabu cha Rais Mstaafu Mzee Aboud Jumbe, The Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union 30 Turbulent years ambacho kilichapishwa mwaka 1994 na Al Khayria Press Ltd na kuenezwa na Amana Publishers.

Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Jumuiya ya Mataifa (United Nations)
Kutoka Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru, Ukurasa 334.
“Ukweli unabakiya kuwa Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar haukuwahi kusajiliwa katika Seketeriet ya Umoja wa Mataifa [UN].

Kwa mujibu wa Andrei Kolomoets wa Ofisii ya Mambo ya Kisheria ya Umoja wa Mataifa “Kama ulisajiliwa basi kungelikuwepo rekodi katika Data Base na shahada ya usajili ingelikuwepo. Nimecheki, haipo.”

Kamisheni ya Katiba na Bunge la Katiba
Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.

Itakumbukwa kuwa Mkataba wa Muungano uliagiza kuchaguliwa kwa kamisheni ya katiba na kufuatiliwa na bunge la katika ndani ya mwaka mmoja kutokea siku ya kutiwa saini Mkataba wa Muungano ili katiba ya Muungano ipatikane.

Haikufanyika na wakati wa kuyatekeleza hayo ukaakhirishwa moja kwa moja. Kisheria ilifanywa hivyo pale bunge la Muungano lilipopitisha Sheria ya Bunge inayoitwa Sheria ya
Bunge la Muungano, 1965 (Nambari 18)…Kwa hiyo kimyakimya, kisirisiri, bunge la Muungano limeubadilisha Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano.

Inaweza kuhojiwa kama (a) upande mmoja wa bunge la Muungano una mamlaka ya kuubalilisha Mkataba wa Muungano ambao ni mkataba wa kimataifa na (b) kuibadilisha sheria ya Zanzibar ambayo inasemekana kuwa ilipitishwa na Baraza la Mapinduzi kuudhinisha Mkataba wa Muungano.

Inaweza ikahojiwa, na kwa njia safi na ilio wazi zaidi, kuwa njia nzuri ingelikuwa kwa viongozi watendaji wawili, Karume na Nyerere, na Nyerere kwa uwezo wake kama ni mkuu wa ‘Tanganyika’, angelipatana upya kuhusu Mkataba wa Muungano.

Lakini kisiasa njia hiyo ingelikuwa ni msiba kwa sababu ingeliuunja muungano hapo hapo. Ukurasa 163-164.
Kama unamjuwa adui yako na unajijuwa wewe mwenyewe, utakuwa huna wasiwasi wa matokeo ya vita hata viwe mia. Lakini kama unajijuwa wewe mwenyewe lakini humjui adui yako, basi kwa kila vita utakavyoshinda basi pia utashindwa. Na kama humjui adui yako na hujijui wewe mwenyewe basi utashindwa katika kila vita – Sun Tzu.

_____________________________________________________________

Kutoka Kwa Dr. Harith Ghassany ”Facebook”

Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union, pp. 79-81.

Advertisements

One thought on “Utiaji Saini wa Mkataba wa Muungano na Matokeo Yake {UHARAMU WA MUUNGANO}

  1. Mimi, siamini kabisa kama, eti watu kama: Jumbe, Hassan Nassor Moyo na wengine wengi ambao walikuwepo katika serkali ya mwanzo ya mapinduzi Zanzibar, kuwa eti walikuwa hawajui muungano umefanyikaje..

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s