Mswaada mpya wa mabadiliko ya katiba mtego kwa Zanzibar.

vijana wakiwa katika maandamano

Mswada mpya wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao utafikishwa bungeni hivi karibuni kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa kuwa sheria bado unaonekana kubeba vifungu vya mitego dhidi ya upande wa Zanzibar, ili kutoa mwanya kwa watanganyika kupenyezi maslahi yao katika katiba hiyo.

Miongoni mwa maeneo yanayoonekana kuwa ni mitego ni yakiwemo haya yafuatayo.
1. Ibara ya 9 (2) Katika kutekeleza masharti ya kifungu kidogo cha (1) Tume itazingatia misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii, na kwa mantiki hiyo kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo
a) Kuwepo kwa Janhuri ya muungano
b) Uwepo wa serikali bunge na mahakama (mpaka kifungu cha h)

Tukiangalia ibara hii utaona kwamba kilichowekwa hapa hapa ni kile kile kilichokuwemo katika mswada wa awali uliochana huko Zanzibar. Kifungu hichi kina lengo lile lile la kuwazuia wale ambao wanahitaji kutoa maoni yao kama wanapenda kuendelea kua na muungano au laa wasiweze kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa kifungu hicho maoni yanayolenga kuukataa muungano wenyewe hayatazingatiwa katika hansard za makishna wa Tume. Wazanzibari walikosa kuulizwa huko nyuma kama wanautaka muungano huu au laa wanauhitaji uendelee au laa. Hivyo basi hii ndio nafasi pekee ya kuwapa wazanzibari na watanganyika kujadili na kuwamua kama wangependa kuendelea kuwa na muungano wao huo au laa.

2. Ibara ya 13 (6) Sekreterieti (ya Tume) itakuwa na idadi ya watumishi wa umma kwa kadri itakavyohitajika kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu na mamlaka ya Tume.
Sekretarieti ya Tume ndio itakokaa kitako na kuyafanyia mahesabu na tathmini maoni ya wananchi na kuyatafsiri, kwa mfano ni asilimia ngapi ya wazanzibari wamedai kutoendelea kwa muungano, asilimia ngapi wamedai serikali 3, serikali 2 nk.

Mahesabu hayo ndio yatakayotumika kuiandika katiba kwa kuwa ndio jumla ya maoni ya wananchi. Kwa kuwa ibara hii haikueleza kuwepo kwa uwiano sawa wa wajumbe wa sekretarieti kati ya Tanganyika na Zanzibar upo uwezekano wa kuwapiga changa la macho wazanzibari na kuchakachua na mahesabu ya maoni kutolewa yalio kinyume na uhalisia.

3. Ibara ya 20 (3) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (2) idadi ya wajumbe wa bunge la katiba kutoka Tanzania Zanzibar watakaopatikana kwa mujibu wa aya ya (a) hadi (e) haitapungua theluthi moja ya wajumbe wote wa bunge la katiba.

Lile dai muhimu la wazanzibari kwamba bunge la katiba lilwe na idadi sawa ya wajumbe wa bunge la katiba limepuuzwa tena. Idadi ya Wajumbe wa bunge la katiba kwa mujibu wa mswada mpya haitalingana baina ya Tanganyika na Zanzibar. Bunge la katiba ndilo litakalokuwa na mamlaka ya kuijadili rasimu ya katiba iliyoandikwa na tume na mwisho kupiga kura kuipitisha au kutokuipitisha.

Kwa hivyo michango ya mijadala kutoka Zanzibar itakuwa michache na hivyo kufunikwa na michango mingi ya watanganyika. Pia sheria hii imelipa uwezo bunge la katiba kuendelea kutumia kanuni za bunge la kawaida kufanya maamuzi kanuni ambazo zinalalamikiwa kuikandamiza Zanzibar kwa muda mrefu.

4. Ibara ya 24 (3) Uchaguzi wa spika na naibu spika utaendeshwa kwa kura ya siri na mshindi atachaguliwa kutokana na wingi wa kura.
Kwa kuwa idadi ya wajumbe wa bunge la katiba kutoka Zanzibar ni theluthi moja tu ya wajumbe wote wote wa bunge la katiba ni hakika spika atachaguliwa kutoka upande wa Tanganyika ili kul;inda maslahi ya Tanganyika.

Ukweli hapa imekusudiwa Zanzibar ichukue nafasi ya Naibu spika. Hakuna utaratibu unaowezekana kumpata spika kwa haki bila ya wajumbe wa bunge kuwa sawa baina ya Tanganyika na Zanzibar.

5. Ibara ya 32 (2) inatoa uhalali wa matokeo ya ushindi wa kura ya maoni kwa asilimia zaidi ya 50 ya kura zote. Hichi niwango kidogo na ni rahisi kukichakachua. Kiwango muafaka cha ushindi ni angalau asilimia 65.

6. Kwa kuwa kura ya maoni kuhalalisha katiba mpya itapigwa tofauti baina ya Tanganyika na Zanzibar, Pia sheria hii iko kimya haisemi ni nini kitafuatia pale upande mmoja wa jamhuri ya muungano itakaposhinda kura ya HAPANA na upande wa pili ikashinda kura ya NDIO.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s