CUF yatamka

Mkurugenzi wa habari,mahusiano ya umma na haki za binadam, Mh Salim Bimani wakati akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Vuga.

Chama cha Wananchi CUF kimeridhia muundo wa tume ambayo imeteuliwa na Rais wa Zanzibar kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa ajali ya meli ya MV Spice Islanders iliyotokea tarehe 10 usiku katika mkondo wa Nungwi ikwa njiani kuelea kisiwani Pemba.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa haki za binadamu, sheria, habari na mahusiano ya Umma wa Chama hicho Mheshimiwa Salim A. Bimani alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Vuga siku ya tarehe 30 septemba mwaka huu.
Mbali na shukurani hizo, mheshimiwa Bimani pia amesema kwamba chama cha CUF kinatoa mkono wa pole kwa wafiwa na kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu.
Akielezea kuhusu kuundwa kwa tume hio, amesema kwamba chama cha CUF kimepata wasiwasi mkubwa wa kiutendaji wa tume hio kutokana na kimya kirefu tokea kuundwa kwake, na kutojulikana mahala ilpo ofisi ya tume hiyo ili wananchi wapate fursa ya kupeleka maoni yao sambamba na kupata taarifa rasmi ya kipi kinachoendelea na inafanya kazi kwa utaratibu upi ili ile imani ya wananchi kwa Serikali juu ya kuundwa tume hiyo iendelee kuwepo kuwaeleza hakuna budi ikaanza kuwaeleza wananchi hatua gani wamechukuwa hadi sasa.
Wananchi wanahamu kubwa ya kutoa madukuduku yao, haina budi tume hii kuweka vituo katika maeneo mengine ambapo watapeleka maoni yao.
Aidha, amesema kwamba, tume hio hadi sasa haijawahi kuzungumza na waandishi wa habari ambao watawapasha wananchi kwa kile kinachoendelea, kwa hivyo kwa niaba ya chama chake (CUF) ameitaka tume hio ifanye hivyo kwa lengo la wananchi wapate kujua kinachoendelea.
Pongezi
Akitoa pongezi zake kwa wale wote ambao wamechangia mfuko wa maafa wakiwemo watanzania na wengine kutoka nje, kwa michango yao ili kuwasaidia wale wote ambao wamepoteza ndugu pamoja na wazee wao ili kujikwamua kimaisha kwa njia moja au nyengine.
Pia amewashukuru wakaazi waNungwi na vitongoji vyake kwa kujitolea kikamilifu kusaidia shuguli za uokozi.
Tahadhari
Akitoa tahadhari, Mheshimiwa Bimani ametoa tahadhari juu ya fedha zinazokusanywa na kamati ya maafa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wale walioathirika kutokaana na ajali hio kwa njia moja au nyengine kufanya hivyo na fedha ambazo itapatikana zitumike kwa malengo yaliokusudiwa na si vyenginevyo. Wako mayatima wengi ambao wamepoteza wazazi wao na wanataka na wanahitaji huduma kama vile masomo chakula n.k
Pia amesema kuwa itolewe takwimu halisi ya idadi ya watu ambao wamefariki na wote ambao walikuwemo ili iweze kujulikana.
Kuhusu mamlaka ya bandari, Mheshimiwa bimani ameitaka mamlaka hio kujifunza kwa lile ambalo limetokea kuwa nitahadhari kwa jengine kwakufanya ukaguzi kwa vyombo vyote kabla ya kuruhusiwa kupakia abiria, na ameitaka Serikali kununuwa helkopta mbili moja kwa kisiwa cha Unguja na nyengine kwa kisiwa cha Pemba, ambazo zitasaidia kwa ajili ya shughuli za uokozi mara tu pale ajali itakapotokezea.
Vitambulisho vya Uzanzibari ukaazi
Akizungumzia suala la vitambulisho vya ukaazi (Zanzibar ID), Mheshimiwa Bimani ameitoa wito kwa tume husika kufanya majukumu yake pasi na upendeleo kwani hadi sasa kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajapatiwa vitambulisho hivyo na inaonekana dhahiri kwamba wale wanaonyimwa haki ya kupata vitambulisho hivyo ni wale ambao wanaonekana ni wafuasi wa chama cha CUF, huku ni kwenda kinyume na ahadi za Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Utawala bora Dr Mwinyi Haji Makame aliyoitowa katika baraza la wawakilishi.
“Ipo idadi kubwa ya wazanzibari ambao hadi sasa hawajapatiwa vitambulisho hivyo, kama mkoa wa kaskazini, katika jimbo la Nungwikuna watu wapatao 606, Chaani watu 434, Tumbatu 629, Matemwe 423, Mkwajuni 282, Bumbwini 324 pia kuna Jimbo la Donge na Kitope idadi halisi haijafahamika.ambapo hadi sasa hawajapatiwa vitambulisho.
Imeonekana watu hao hata wakifuata utaratibu unaotakiwa inakuwa ni vigumu kupata haki yao hio ambayo ni ya msingi kwao kwani kukosa kwao vitambulisho hivyo ndio hukosa huduma zote katika nchi hii ikkwemo suala la ajira, usafiri kutokana na utaratibu ambao umewekwa.
Mkurugenzi wa vitambulisho hivyo ndugu Mohammed Juma Ame akishirikiana na watendaji wengine ameonekana kuwa ni kikwazo kikubwa kupatikana kwa ID hizo, hivyo tunamuomba Rais amuwajibishe kwani anaweza kuipeleka nchi pahala pabaya , kwani itafika wakati ambapo watu hawatokubali tena kuikosa haki yao hiyo” alisema.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s