CUF yamjia juu Lowassa

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema hakuna sababu ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, kukaripia vyombo vya
habari na madai ya kuwaonea huruma Watanzania na kuwalaumu wenzake wakati na yeye ni sehemu ya matatizo yao.

Pia CUF imesema Bw. Lowassa hana sababu ya kulaumu umaskini wa Watanzania bali ashauriane na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wenzake namna gani waache maslahi binafsi na kutetea Mtanzania mnyonge anayeteseka kwa matendo yao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi na Bunge wa CUF, Bw. Shaweji Mketo, ilieleza kuwa chama hicho kinamtaka Bw. Lowassa kutafakari utendaji wake kabla ya kujiuzulu uwaziri Mkuu.

Taarifa hiyo ya CUF iliseleza kuwa, Bw. Lowassa anajifanya kuwa na uchungu na matatizo yanayowakabili Watanzania wakati yanasababishwa na chama chake naye ni mhusika, hivyo dawa ni kukaa pamoja kuangalia jinsi ya kuyatatua.

Ilieleza kuwa Bw.Lowasa alikuwa kwenye serikali ya sasa kabla ya kujiuzulu na kwamba hadi sasa ni kiongozi muhimu ndani ya CCM kama mjumbe wa vikao vya juu vya chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Monduli hivyo matatizo ya Watanzania wanayowapata hivi sasa na yeye ni mmoja wapo kati ya watu waliochangia.

Chama hicho pia kilihoji sababu ya viongozi wa CCM ambao hawapo madarakani kwa sasa kujitokeza kukosoa mambo mbalimbali na kutoa mfano wa siku ya maadhimisho ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

“Mfano amesikika mkongwe wa CCM, Bw. Kingunge Ngombale-Mwiru alipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mwalimu Nyerere akiikaripia CCM akiitaka ifuate misingi ya azimio la Arusha na mfumo wa CCM aliyoiacha mwalimu Nyerere,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya CUF.

Taarifa hiyo ilisema CCM inajitahidi kuitumia Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kama njia ya kuonesha kwamba wanavijana makini kama vile Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Bw.Ole Millya, aliyewarubuni Watanzania kuhusu uhalisia wa chama hicho.

Ilieleza kuwa tatizo la CCM ni mfumo wa chama hicho unaotengeneza viongozi wanaopatikana kwa fedha na kwa kuzingatia maslahi ya mtu na mtu ama mtandao kwa mtandao na kwamba haiwezi kujirekebisha na kuwa chama cha kuwasaidia Watanzania kuvuka kutoka kwenye umasikini.

“CCM ilizaliwa, ikakua, imezeeka na sasa inaelekea kufa, kwa hiyo CUF inawataadharisha Watanzania kwamba wasije wakadanganyika na vituko vya kauli zinazotolewa na baadhi ya wana CCM kwa lengo la kuhakikisha inabaki madarakani,”ilieleza taarifa hiyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s