PRESS CONFERENCE (MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI).

Pahala: Ukumbi wa mkutano C.U.F Vuga.
Tarehe: 30/09/2011
Wakati: saa 3:30 asubuhi.
Mada kuu:
1) Pole kwa wazanzibari wote na watanzania kwa ujumla waliopatwa na msiba wa kuzama kwa meli ya MV Spice Islanders.
2) Shukrani kwa vyombo vya habari kwa jinsi walivyotoa ushirikiano katika kutoa taarifa za meli iliyozama.
3) Shukurani kwa taasisi na wananchi waliojitolea kikamilifu katika uwokozi wa majeruhi na utafutaji wa maiti, aidha na wale waliojitolea kukosha na kuzika maiti hao.
4) Shukrani za dhati pia kwa wale waliochangia na wanaoendelea kuuchangia Mfuko wa Maafa kwa ajili ya wahanga wa ajali hiyo.
5) Suala zima la kuboresha Daftari la la Kudumu la wapiga kura, na utolewaji wa ZAN-ID.
6) Ahadi ya Serekali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) juu ya suala zima la kupandisha mishahara ya wafanyakazi kwa asilimia 20.
7) Ushauri kwa Serekali (GNU).

Ni ukweli usiofichika kwamba suala la kuzama kwa meli ya MV Spice Islanders limepoteza maisha ya wananchi wengi na kuacha vizuka na mayatima wengi ambao ni ulezi kwa serekali.
Chama Cha Wananchi CUF hakina lengo la kuendelea kuwatonesha wananchi juu ya huzuni na majonzi kwa kuwapoteza wananchi wenzetu, bali tumeona kuna kila haja ya kuendelea kuwapa pole kwa huzuni zilizotawala katika nyoyo zetu, kwa sababu msiba huu si tu wakitaifa, bali pia umetupa huzuni sana sisi kama Chama Cha siasa chenye ushirikiano na kukubalika sana na wananchi wa Zanzibar; hususan katika kisiwa cha Pemba.
Tunaahidi kuwa pamoja; bega kwa bega na familia zilizopatwa na msiba huu kwa hali na mali.
Pia tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa vyombo vya habari vya binafsi na serekali kwa ushirikiano wao na kujitolea kwao katika kutoa taarifa za ajali ya kuzama kwa meli. Hata hivyo tunapenda kulishauri Baraza la Habari la Zanzibar kutoa uhuru wa kutoa taarifa kwa vyombo vyengine wakati jamii inapohitaji taarifa hizo kwa haraka na uwazi zaidi.
Aidha Chama Cha Wananchi CUF inatoa shukrani za dhati kwa taasisi pamoja na wananchi waliojitolea kikamilifu katika uwokozi wa majeruhi, utaftaji wa maiti, kuwakosha na kuwazika maiti hao. Wananchi waliona wazi kwamba kila mtu kwa nafasi yake alijitolea kwa njia moja au nyengine ili kuhakikisha anayanusuru maisha ya wananchi wenzake.
Pia tunapenda kutoa shukrani za dhati na pongezi kwa wananchi, mashirika na asasi za kijamii kwa mchango wao katika Mfuko wa Maafa ambao una lengo la kuwafariji waliokumbwa na janga hili.
Kwa kweli inatia moyo sana na inaonesha jinsi wananchi wetu wanahurumiana. Na hii inaashiria kuwa nchi yetu imeshaondoka katika zama za kuhasimiana na kutokuhurumiana.
Kwa upande wa suala la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura, na utolewaji wa Zan-ID; hatuna budi kuijuulisha serekali kuwa watendaji wake katika kada hii ya utowaji vitambulisho, pamoja na masheha wa shehia bado wanaonekana kuwaekea vikwazo visivyo vya msingi na kuwakatalia kabisa wananchi wenye haki ya kuwa na ZAN-ID. Tunamuomba waziri husika azungumze na watendaji wake, kwasababu hii ni haki ya kila mzanzibari mwenye sifa, na sio mzanzibari wa upande flani.
Aidha tunapenda kuikumbusha serekali ya Umoja wa Kitaifa juu ya ahadi yao ya kuwaongezea nyongeza ya mishahara watendaji wa serekali kwa asilimia 25. Tunawakumbusha watekeleze ahadi zao kwa sababu gharama za maisha bado ni kubwa mno, na kima cha mshahara kiliopo hakitoshelezi haja.
USHAURI KWA SEREKALI:
a) Tume iliyotangazwa kuchunguza ajali ya MV Spice Islander iapishwe haraka na ipewe uhuru wa kufanya kazi yake kwa uwazi na uadilifu.
b) Mfuko wa maafa usije kuchezewa ili wananchi wajenge imani na serekali yao.
c) Kufanywe uhakiki wa wazi juu ya uzima na ubora kwa vyombo vya baharini na nchi kavu.

HAKI SAWA KWA WOTE.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s