KESI ZA UCHAGUZI MKUU:CUF yaanguka, Chadema, CCM wakwama

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki, alisema asingeweza kuzungumzia tukio hilo kwa sababu alikuwa safarini Dar es Salaam.Awali, akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa moja na nusu, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Seleman Kihiyo, alisema mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha madai yake, hivyo ameamua kutupilia mbali ombi lake la kutaka kutengua matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana na kumpatia ushindi Murji.

Miongoni mwa hoja ambazo mlalamikaji aliwasilisha Mahakamani hapo ni madai kuwa, walinyimwa haki ya kuhesabu kura, kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo na baadhi ya fomu za matokeo kutosomeka vizuri.

Jaji Kihiyo alisema madai hayo yote yameshindwa kuthibitika mbele ya mahakama, hivyo ameamua kulitupilia mbali shauri hilo na kuamuru mlalamikaji kumlipa mlalamikiwa gharama zote za uendeshaji kesi na kwamba, anaweza kukata rufaa iwapo hajaridhishwa na uamuzi huo.

Umati wa watu ulihudhuria mahakamani hapo, kusikiliza kesi hiyo yenye mashahidi watatu, wawili wakiwa wa upande wa mlalamikaji na mmoja upande wa mlalamikiwa. Hata hivyo, hawakupata fursa nzuri ya kusikiliza hukumu hiyo kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya vipaza sauti vilivyofungwa nje.
Wakati hayo yakiendelea mkoani Mtwara, kesi namba 12/2010 ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Jimbo la Ilemela jana ilishindwa kuanza kusikilizwa baada ya mashahidi wawili kushindwa kufika mahakamani.

Wakili wa Mbunge Highness Kiwia (Chadema), Tundu Lisu, alisema jana baada ya kuahirishwa kesi hiyo kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na kukosekana kwa mashahidi wa upande wa walalamikaji.

Alisema kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Oktoba 21, mwaka huu.
Msajili wa Mahakama Isaya Arufani, alieleza kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi Ijumaa itakapoanza kusikilizwa na Jaji Gadi Mjemas.Katika kesi hiyo, walalamikaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi ni wakazi watatu wa Ilemela, Yusuf Lupilya, Nuru Nsubugu na Beatus Madenge.

Washitakiwa ni Kiwia, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Willson Kabwe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Katika matokeo hayo yanayopingwa mahakamani, Kiwia alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 31,269 dhidi ya mpinzani wake, Anthony Diallo wa CCM aliyepata kura 26,270.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s