INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAAJIUN

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF- Chama Cha Wananchi)
Kurugenzi ya Haki za Binadamu, Habari na Uenezi.
Office of the Secretary General
P.O. BOX 3637, Zanzibar, Tanzania
E-mail: cufhabari@yahoo.couk
Weblog:http:hakinaumma.worldpress.com

Our Ref: CUF/HQ/KR/U/01/011/31 Date: 18/10/2011.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Maulid Hamad Maulid, wakati wa uhai wake

Chama cha Wananchi, CUF, kimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mwandishi Mwandamizi wa Habari nchini, Bw. Maulid Hamad Maulid.

Chama cha Wananchi, CUF, kinaamini kuwa kifo ni haki ya kila kiumbe-hai duniani, na kwamba hakuna atakayeweza kukiepuka, pale muda wake ukifika wa kuondoka duniani, na hivyo ndivyo ilivyokwishajiri kwa ndugu yetu Maulid, na pia kwamba hiyo ni KUDRA YA MWENYEZI MUNGU.

Ni dhahiri kwamba taarifa hizi zimewagusa wengi kuanzia familia yake, taasisi alizoweza kuzitumikiwa zikiwemo za vyombo mbali mbali vya habari, michezo, vyama, jamii na umma kwa ujumla.

Maulid alikuwa sehemu muhimu ya jamii katika harakati za habari, mwandishi hodari na mahiri mwenye kujali uzalendo, mstahamilivu, na aliyeweza kushikamana bega kwa bega na wanahabari wengine pamoja na wananchi katika kuhamasisha maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Chama cha Wananchi, CUF, kinaungana na taasisi zote zilizoguswa na kifo cha Bw. Maulid, pamoja na wananchi kwa ujumla, katika kuyakumbuka yale mema ya Mjenzi huyo mashuhuri wa Taifa, hasa wakati huu wa msiba.

“Chama Cha Wananchi, CUF, kinatoa Mkono wa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Marafiki, na Taasisi, Pamoja ka Wananchi Wote, Kutokana ka Kifo Cha Mwanahabari Huyo Mwandamizi”.

Chama cha Wananchi, CUF, kinamuombea Marehemu Maulid Hamad Maulid, MAKAZI mema huko AKHERA –AMIN!

HAKI SAWA KWA WOTE.

………………………………
Salim Bimani,
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari na Uenezi.

Headquaters: P.O.Box 3637, Zanzibar, Tanzania. Tel.: 024 22 37446 Fax.: 024 22 37445
Main Office: PO. Box 10979, Dar-es-Salaam, Tanzania. Tel. 022 861009 Fax.: 022 861010

Headquaters: P.O.Box 3637, Zanzibar, Tanzania. Tel.: 024 22 37446 Fax.: 024 22 37445
Main Office: PO. Box 10979, Dar-es-Salaam, Tanzania. Tel. 022 861009 Fax.: 022 861010

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s