Wairan kujenga hospitali za kisasa Zanzibar

Moja kujengwa Wete Pemba na nyengine Mjini Magharibi Unguja.
• Maalim Seif ashuhudia utiaji saini Dubai.

 

Waziri wa afya wa Zanzibar Mh Juma Duni haji (kushoto) akitia saini makubaliano ya ujenzi wa hospitali mbili za kisasa zitakazo jengwa Zanzibar na jumuiya ya Mwezi Mwekundu ya Iran, makubaliano hayo yalitiwa saini mjini Dubai Falme za Kiarabu. Katikati waliosimama ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na maafisa wa jumuiya hiyo.

Juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuinuwa huduma yza afya kwa wananchi, ikiwemo kuwapunguzia gharama za kwenda kutibiwa nje ya nchi zimeanza kuonesha dalili za mafanikio baada ya Serikali kutiliana saini makubaliano ya ujenzi wa hospitali mbili zqa kisasa zitakazojengwa katika mji wa Wete Pemba na mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Hospitali hizo zitajengwa na jumuiya ya Mwezi Mwekundu ya Iran (Iran red Crescent Society) mara baada jumuia hio kukamilisha utafiti wa mahitaji ya afya ya wananchi wa Zanzibar unaotarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
Hatua hio inafikiwa baada ya serikali ya Zanzibar kutiliana saini makubalianoya mradihuo huko Dubai, Falme za kiarabu wiki iliopita, ambapo Waziri wa afya na Ustawi wa Jamii, Mh Juma Duni Haji alitiliana saini hio kwa niaba ya Zanzibar, huku Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif hamad akishuhudia tukio la utiaji saini makubaliano hayo.
Waziri wa Afya , Juma Duni amesemachini ya makubaliano hayo, jumuia hiyo itajenga hospitali za kisasa zitakazotoa mahitaji yote, ambapo Zanzibar jukumu lake litakuwa ni kuipatia sehemu zitakazo jengwa hospitali hizo katika mkoa wa Mjini Magharibi na huko Wete kwa upande wa Pemba.
“serikali ya Zanzibar haitatoa fedha yoyote kwa ujenzi huo, isipokuwa maeneo ya kujengwa hospitali hizo, baada ya hatua ile ya utiaji saini watafanya utafiti wa mahitaji halisi ya kiafya ya Wazanzibari ambao utakuwa umekamilika ufikapo mwezi Disemba mwaka huu ba ujenzi utaanza”, alisema Waziri Duni.
Alieleza kuwa utafiti huo pia utajumuisha mahitaji ya uajiri kwa madaktari watakao hitajika katika hospitali hizo, pamoja na taratibu za kuwapatia vibali vya kufanyia kazi kwa madaktari wageni watakao hitajika kuja kuwahudumia wagonjwa.
Duni alisema kuwa, jumuia hiyo ya Mwezi Mwekundu ya Iran ni ya hisani (charitable society) ambayo tayari imejenga miradi mikubwa ya hospitali katika miji mbali mbali, ikiwemo Dubai na huduma inazozitoa zimesifiwa juu ya ubora wake na hata unafuu katika upatikanaji wake kwa wananchi wenye vipato vya chini.
Alieleza kuwa walipokuwa Dubai walitembelea moja ya hospitali zinazoendeshwa na jumuiya hiyo, ambayo inatoa huduma zote muhimu katika kiwango cha hali ya juu na wagonjwa wengi wamekuwa wakienda kupata huduma kwa unafuu.
Waziri Duni alisema hospitali hizo zitakapoanza kutoa huduma Zanzibar, itakuwa ni hatua kubwa ya mafaikio kwa Wananchi wa Ungujana Pemba kupata matibabu, kwa sababu haadi sasa huduma zinazopatikana nchini hazijatosheleza na kuna Wananchi wengi wanaopewa rufaa kwenda kutibiwa nje ya nchi, jambo ambalo sio wananchi wote wanaoweza kumudu gharama zake.
Alisema faraja kubwa zaidi itakuwa kwa wananchi wa kisiwa cha Pemba, ambao hata kesi ndogo za matibabu mara kadhaa hutakiwa kwenda Unguja katika hospitali ya Mnazimmoja, jambo ambalo pia alisema ni mzigo kwao kutokana na hali za maisha za wananchi wengi bado ni duni.
“Hospitali itakayo jengwa kule Wete Pemba ina umuhimu mkubwa zaidi ikizingatiwa kwamba, hata kesi za kawaida wao hutakiwa kuja Uguja na kutumia gharama nyingi za usafiri na matibabu yenyewe”, alisema.
Ijumaa iliyopita, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali inachukuwa juhudi kubwa kuhakikisha huduma za kisasa na za kiwango cha juu za matibabu zinapatikana Zanzibar kwa nia ya kuwaondolea usumbufu na gharama kubwa wanazopata wananchi pamoja na serikali, pale wanapotakiwa kwenda kufanyiwa matibabu zaidi nchi za nje.
Akizungumza na madaktarri kutoka hospitali ya MIOT ya India walipomtembelea ofisini kwake, alisema bado Zanzibar inahitaji wataalamu waliobobea zaidi katika sekta mbali mbali,ikiwemo ya Afya kufanikisha azma ya kuwapatia wananchi wa visiwa vya Zanzibar huduma za matibabu za urahisi na uhakika.
Maalim Seif alisema hadi sasa kesi za wagonjwa wanaotakiwa kupatiwa matibabu ni nyingi, ikiwemo watoto wadogo wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo, ambao hutakiwakwenda kufanyiwa upasuaji nchini India wakifuatana na jamaa pamoja na mhuduma wa Afya, ambapo Serikali na Wananchi watapata nafuu kubwa iwapo huduma kama hizo zitakapokuwa zinapatikana hapa hapa Zanzibar.
Mbalina nchi za nje, baadhi ya wagonjwa hapa Zanzibar hutakiwa kwenda kupata matibabu zaid katika hospitali za Tanzania Bara, pale huduma husika zinapokosekana katika hospitali za Zanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s