Msaada wa India Utumike ipasavyo kuimarisha maendeleo ya teknohama, katika viwanda vyetu.

Zanzibar imepata faraja nyengine baada ya India kusema iko tayari kusaidia maeneo ya elimu, viwanda na Teknohama.

Faraja hii inatokana na ushawishi unaoendelea kufanywa na serikali kupitia makamo wakwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kwa washirika wa maendeleo, kuhakikisha Zanzibar nayo inapiga hatua muhimu za kimaendeleo katika sekta mbalimbali hasa ICT wakati huu dunia ikiachana na mfumo wa kale wa mawasiliano wa analogi na kuingia katika mfumo wa digital.

Taarifa za India kushawishika kufanya kazi na Zanzibar zimeleta matumaini makubwa na ni ishara tosha kwamba washirika wa maendeleo wako bega kwa bega na Zanzibar katika kusaidia kuinua uchumi wake.

Tunachukuwa fursa hii kuipongeza serikali ya India kwa dhihirisha udugu wake kwa Zanzibar na kukitumia kile walichonacho kwa faida ya ndugu zao ili nao wasiachwe nyuma.

Ni matarajio yetu kwamba, baada ya ujumbe wa Makamo wa Kwanza wa Rais kurejea nyumbani, wataalamu wake watakaa chini kuchambua mahitaji yetu halisi na kuyapeleka tena India kwa ajili yakufanyiwa kazi.

Aidha hii ni fusra adhimu kwetu ya kufufua viwanda vyetu pamoja na kuanzisha vyengine kama vya mboga mboga na matunda ambavyo vitatusaidia angalau kuingia katika ushindani wa soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambalo kama Zanzibar hatutajitutumua basi sisi tutakuwa wapokeaji tu wa bidhaa kutoka nchi nyengine wanachama huku sisi tukiwa hatusafirishi chochote.

Kwa kuwa malengo ya Zanzibar ni kuwa na kituo maarufu cha Teknohama katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, sekta ambayo hivi sasa imekuwa kichocheo kikubwa cha ajira na mafanikio katika sekta zote za maendeleo na uchumi, msaada huu wa India utakuwa umekuja wakati muafaka na sasa ni wajibu wa watendaji wa serikali kuhakikisha azma hio ya serikali inatekelezwa kikamilifu.

Tunaamini kwamba mbali ya Zanzibar kunufaika na misaada hio, pia kuna fursa nyingi za uwekezaji kwa wafanya biashara wa India katika visiwa vyetu vya Unguja na Pemba, ikiwemo sekta ya utalii, nishati na uvuvi hasa katika kisiwa cha pemba, ambacho bado kuna maeneo mengi yanahitaji kuwekeza kwa kuwa sasa kuna umeme wa uhakika.

Aidha hii ni fursa kwa wanafunzi wa Zanzibar kutumia ushirikiano uliopo kupeleka wanafunzi wetu India kwenda kujifunza elimu ya Teknohama kwa sababu India imepata sifa kubwa duniani kwa maendeleo ya ICT.

Wakati tunaendelea katika mfumo wa mawasiliano wa digital mwaka 2013, Zanzibar tunahitaji wataalamu ambao wataweza kumudu matakwa ya mfumo huu mpya ambao tunaamini utakuwa wa changamoto nyingi kwetu.

Huu si wakati tena wa kutumia fursa ya kwenda nje kama mapumziko, badala yake tutekeleze kwa vitendo yale tunayo jifunza.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s