Siasa za helikopta ni za kitoto-CUF

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema siasa za sasa za kutumia helikopta ni za kitoto na zina lengo la kuhamisha Watanzania kutoka katika kujadili hoja za msingi za maisha yao na kuingia
katika kujadili nani anatumia helikopta.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Zanzibar Ismail Jussa Ladhu, alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari kufafanua hoja alizodai zimepotoshwa na gazeti moja la kila wiki na
kuongeza kuwa baada ya CUF kuleta helikopta, wananchi sasa wameanza kubadilika na kuanza kujadili hoja za maji, afya, elimu na nyingine.

“Helikopta inatumika kama toy (mwanasesere) kutokana na kutoelimika kwa Watanzania na umasikini wao, inawatoa Watanzania katika kujadili hoja zinazogusa maisha yao, inawaingiza
katika mambo ya kitoto,” alisema Jussa na kuomba radhi kwa kuzungumzia ukweli katika namna hiyo.

Kwa mujibu wa Jussa, mwanzoni wakati Chadema imeanzisha matumizi ya helikopta katika uchaguzi, walidhani kuwa ni chombo cha kurahisisha usafiri na kusaidia kufika maeneo
mbalimbali ya nchi.

Tofauti na dhana hiyo, Jussa alisema walishangaa kuona chombo hicho kikitumika katika uchaguzi mdogo ndio wakagundua kuwa lengo lake halikuwa kurahisisha usafiri, bali siasa
hizo za kitoto.

Aliilaumu CCM kwa madai kuwa ndiyo iliyowafikisha Watanzania katika hatua hiyo ya kutojadili mambo ya msingi ya maisha yao na kuanza kujadili nani anatumia helikopta ndio
maana na yenyewe ikaingia katika matumizi ya chombo hicho.

Jussa alifafanua kuwa CUF na wao wameamua kutumia helikopta katika uchaguzi wa Igunga na itaendelea kuitumia katika uchaguzi mwingine wowote utakaokuja ili kuweka uwanja sawa wa siasa.

Kutokana na kufanikiwa kuweka uwanja huo wa siasa sawa Igunga, Jussa alisema kwa sasa wananchi wameanza kuelewa baada ya kuzoea helikopta hizo na kubadilika na sasa wanajadili mustakabali wa maisha yao na Chadema kimeanza kupata wasiwasi baada ya CUF kuanza kutumia chombo hicho.

Alidai kuwa katika wasiwasi huo, Mratibu wa kampeni za Chadema, Mwikabe Mwita alinukuliwa na gazeti moja la kila wiki akisema kuwa CUF kimechoka katika kampeni hizo na hata Naibu Katibu Mkuu wake Tanzania Bara, Julius Mtatiro amekimbia Igunga na kurudi Dar es Salaam baada ya kuona anapoteza muda.

Jussa alisema kila mtu anajua kuwa Mtatiro yupo Igunga, anashiriki katika kampeni na hata jana alipishana na waandishi wakiingia katika mkutano wa CUF na yeye akienda katika shughuli za kampeni.

Naye Mwita alivyoulizwa na gazeti hili, alikiri kusema maneno hayo na kuongeza kuwa ana taarifa za uhakika kuwa Mtatiro alikwenda Dar es Salaam kushughulikia helikopta ya CUF na
amesharudi kwa sasa.

Katika hatua nyingine, Jussa aliviasa vyombo vya habari kuacha kushabikia siasa hizo za kitoto na kutolea mfano wa mhariri mmoja ambaye alikataa kumtaja jina wala chombo
chake aliyempigia simu akiuliza iwapo ni kweli helikopta ya CUF ilipotea eneo ilikokuwa ikienda.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s