CUF wambebesha msalaba Msekwa

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtupia lawama Makamu Mwenyekiti wa CCM (bara), Bw. Pius Msekwa kuwa endapo damu itamwagika katika uchaguzi mkdogo wa
Jimbo la Igunga ndiye atakuwa amesababisha.

Meneja Kampeni wa chama hicho Jimbo la Igunga, Bw. Antony Kayange akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Bw. Leopold Mahona katika kijiji cha Ncheli, Kata Sungwizi, alisema kitendo cha Bw. Msekwa kutangaza kuwa CCM itashinda katika jimbo hilo anataka damu imwagike.

Bw. Mayange alisema CCM haina chake kwa sababu imekuwa ikitaka
wananchi wa Igunga wachague mbunge wa chama hicho lakini akichaguliwa haonekani tena mpaka uchaguzi mwingine uje, huku akiacha wananchi wakiendelea kuteseka kwa shida zilizokithiri.

Bw. Pius Msekwa alikaririwa akitamba kwenye vyombo vya habari kuwa pamoja ya matukio ya hapa na pale yanayofanywa na vyama vya upinzani, bado CCM itashinda katika uchaguzi wa mbunge utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu.

Kampeni za chama hicho zilizofanyika juzi katika Tarafa ya Simbo
alikozaliwa na kusoma Bw. Mahona, watu waliohudhuria kumsikiliza walimtaka asiige tabia za wabunge waliopita wa CCM pindi wanapochaguliwa hukimbilia Dar es Salaam wao wakibaki yatima na hawana sehemu ya kupeleka matatizo yao.

“Nimedhamiria kuokoa maisha ya ndugu zangu wa Igunga, ndiyo maana mwaka jana nilibaki peke yangu nikiomba kura zenu kwa baiskeli. Kati ya wagombea 13 waliochukua fomu za Ubunge nikapambana na mbunge aliyejiuzulu CCM hivi karibuni, Bw. Rostam Aziz na nikashinda vishawishi vyake vya kutaka nijitoe nikang’angana hadi mwisho nikashika nafasi ya pili nikipata kura 11,000,” alisema Bw. Mahona.

Kampeni za CUF zilitarajiwa kuendelea jana katika vijiji 96 vya Jimbo la Igunga ambalo wananchi wake wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ya safi ya kunywa na kunywesha mifugo yao.

“Huyu Pius Msekwa anatangaza CCM itachukua jimbo hili yaani wasukuma na wanyamwezi wote hatuwezi kudanganywa kama walivyozoea kufanya wanavyotaka,” alisema Bw. Mahona.

Mikakati ya kampeni

Akizungumzian kampeni za uchaguzi wa Igunga, Naibu katibu Mkuu wa CUF (Bara), Bw. Julius Mtatiro alisema wamejipanga vizuri na kuongeza timu kufikia 6 na kufanya mikutano 36 kwa siku katika kata 26 za Igunga.

Alisema baada wabunge sita wa Zanzibar kuwasili wengine 10 wanatarajia kuwasili leo, wengine 15 Alhamisi, na Ijumaa
wataongezeka watano na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Bw. Mtatiro alisema timu hiyo inaongeza mikutano kufikia 45 kwa siku na kutamba kuwa chama chake kiko tayari kupiga kampeni ya chini kwa chini, juu kwa juu na miguu kwa miguu.

Alisema vyama vingine vikileta helkopta moja, CUF nayo inafanya hivyo hivyo, vikileta tatu na hata kumi nacho kitafanya hivyo mpaka jimbo hilo libaki kwa chama hicho

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s