CUF na falsafa ya maisha mapya Igunga

SIASA ni moja ya eneo muhimu katika jamii yoyote ile, haina maana kuwa kila familia lazima awepo mwanasiasa lakini kila taifa lazima liwe na wanasiasa.

Siasa ndio kila kitu kwa kuwa, mambo mengi yanatokana na sera za vyama hivyo ambapo kwa kawaida siku zote hulenga kusukuma gurudumu la maisha mbele.

Chaguzi mbalimbali zimefanyika ndani na nje ya nchi ambapo wanasiasa hao wamekuwa wakujinadi kwa wananchi kuwafanyia mambo mengi mema. Leo macho na masikio ya Watanzania yanaelekezwa Tabora katika Wilaya ya Igunga baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bw. Rostam Aziz kung’atuka.

Kinyang’anyiri cha kugombea ubunge katika jimbo hilo kilianza Septemba 7, mwaka huu kwa vyama vinane kuchukua na kurudisha fomu za kugombea ubunge jimboni humo.

Bw. Rostam ambaye ametawala jimbo hilo kwa miaka 19 alitoa sababu za kujivua madaraka yake hayo kwa kile alichodai ‘siasa uchwara za CCM’ na kuamua kubaki kama mwanachama wa kawaida katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Vyama vinavyoshiriki katika uchaguzi huo ni pamoja na CUF, CCM, CHADEMA, DP, SAU, CHAUSTA, UMD, AFD.

Bw. Leopold Mahona (CUF) katika Uchaguzi Mkuu uliopita alishika nafasi ya pili kwa kupata kura kura 11,321 ambapo Bw. Rostam (CCM) aliongoza kwa kupata kura 28,000.

CUF ambacho chimbuko lake ni Wilaya ya Igunga kilianzishwa na mwenyekiti wa kwanza wa Bw. James Mapalala.

Bw. Mahona (29) anasema, ana uwezo wa kuwashirikisha wananchi katika kutatua matatizo mbalimbali yaliyopo katika jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kutumia vizuri maliasili zilizopo katika jimbo hilo.

Anasema, Igunga inayo misitu pori ya asili yenye mchanganyiko wa mimea ambayo hutengeneza gundi, kuzalisha asali kwa kusimamia bei ya kuwa juu na kutangaza wanyama, wadudu wa kuvutia waliopo katika Bonde la Wembele ambako kuna ndege, vyura, nyoka, samba, chui na tembo.

Anasema, ataanzisha uvunaji endelevu wa mimea asilia na kutafuta soko la ndani na nje la mimea hiyo na kuanzisha mikakati ya wananchi kulipwa fidia ya mali na mazao yao yanapoharibiwa na wanyamapori.

Madini

Anasema, katika sekta ya madini atahakikisha upendeleo wa wingi wa madini walionao wananchi wa Igunga unatumika ipasavyo kwa sababu ni mmoja ya majimbo yenye madini mengi ya dhahabu na madini mengine mengi ambayo hayapatikani sehemu nyingine nchini.

Jimbo la Igunga pia kuna madini ya almasi, chokaa, chumvi, mfinyanzi hivyo ataaanzisha vyama maalum vya wachimbaji wadogo waweze kukopa na kununua zana za kisasa za uchimbaji na kuleta watafiti kutafuta maeneo mengine yenye madini na kuhakikisha serikali haiwadhulumu wananchi maeneo yao ya uchimbaji kinyume cha sheria.

Kilimo

Anasema, katika Sekta ya Kilimo atafanya mapinduzi ya kwa kuendeleza wanachi katika kilimo cha umwagiliaji katika maeneo ya Kata ya Simbo, Kata ya Majengo, Kata ya Igumo Buhekela na Utuja na kuendeleza miradi ya kilimo cha mpunga, pamba, alizeti na kuhakikisha anafuta ushuru wa mazao na kusambaza zana za kilimo na pembejeo kwa wakulima.

Pia anasema, wilaya hiyo ina utajiri mkubwa wa mifugo ya ng’ombe na mbuzi hivyo amedhamiria kubadilisha matatizo ya wananchi wa Igunga kwa sababu ni mzaliwa wa Kata ya Simbo aliyesoma shule ya msingi , Sekondari katika Wilaya ya Igunga akitokea katika familia ya Kisukuma.

Bw. Mahona anasema, atainua ubora wa mifugo kwa kuongeza idadi ya madaktari wa mifugo, idadi ya majosho, ukubwa wa maeneo ya malisho na idadi ya manywesheo, kusimamia chanjo na ruzuku za dawa za kuogeshea mifugo ili wafugaji wapate ahueni.

Kugeuza ufugaji kuwa ajira rasmi na kuboresha masoko yenye bei nzuri ya mifugo ambako ngo’mbe watapimwa kwa kilo badala ya kutazamwa kwa macho na kukadiria bei hivyo kuwanufaisha walanguzi huku wakiwaacha wafugaji wakibaki pale pale kiuchumi.

Anasema, atakahikisha anashirikiana na wananchi kuanzisha mchakato wa uchimbaji wa visima virefu vyenye kutoa maji ya kudumu katika vijiji vyote 96 vya Jimbo la Igunga na kuanzisha programu ya uvunaji maji ya mvua hasa mashuleni, zahanati, hospitali na kuboresha vyanzo mvya maji vilivyopo Wilaya ya Igunga.

Mgombea huyo anasema, atahakikisha anawaboreshea wananchi wa Igunga mfuko wa afya ya jamii na kuongeza vituo vya afya kutoka vinne vya sasa hadi vinane ifikapo mwaka 2015 na kununua magari angalau matatu ya kubebea wagonjwa ili kuondoa adha iliyopo sasa na kusimamia zahanati zote ziwe na wauguzi na kuhakikisha madawa yanapatikana ya kutosha.

Pia anaahidi kusimamia mabilioni ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya Barabara za Igunga ili zisiingie mifukoni mwa wajanja na kuhakikisha barabara zinatengenezwa ipasavyo na kupitika mwaka mzima likiwepo Ujenzi wa Daraja la Mbutu ambalo Rais Mstaafu Bw. Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete waliahidi kuyajenga lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika.

Katika suala la mawasiliano anasema, huduma za mawasiliano ya simu bado ni za kusuasua ambako wananchi wanapata mawasiliano baada ya kutegesha simu zao katika milima au juu ya miti na katika miaka miwili vijiji vyote vitapata mawasiliano ya simu za mkononi.

Hivyo, atahakikisha michango ya mara kwa mara inakomeshwa na kuanzisha mitaji ya ajira binafsi ya mtu mmoja mmoja, vikundi vya kijamii vya vijana, wazee akinamama kwa kuanzisha SACCOS moja katika Tarafa nne za Igunga ambako kila mwezi atatoa asilimia 15 ya mshahara wake wa bunge kuimarisha SACCOS hizo.

Bw. Mahona ni mkazi wa Wilaya ya Igunga anasema, akichaguliwa atahakikisha anatumia ilani ya Nishati, Madini na kushirikisha Jamii (NIKIJA) ikiwa na maana ya kutumia rasimali zilizomo jimboni kukomboa maisha ya wananchi wa Igunga.

Bw. Mahona alizaliwa mwaka 1992 katika Kijiji cha Simbo la kusoma Shule ya Msingi Simbo kutoka mwaka 1997 hadi mwaka 2001 na baadaye kuendelea na sekondari katika Shule ya Umoja alikohitimu kitado cha nne mwaka 2001 alipochaguliwa kuendelea kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Uchama.

Alichaguliwa kusomea shahada ya utawala, biashara na uongozi na kuhitimu na aliwahi kuwa mtafiti wa Shirika la World Vision Mkoa wa Shinyanga mwaka 2005 akitokea Shule ya Sekondari Tirav ambako nalifundisha kwa miaka miwili.

Akiwa shuleni hapo pia aliwahi kufanya kazi kama Ofisa Ugavi na Ununuzi wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Tirav na kufanya kazi kama hiyo katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mwaka 2007.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s