Bangalore iko tayari kuisaidia Zanzibar

  • Kuharakisha maendeleo ya elimu, viwanda na ITC

Waziri Kiongozi wa serikali ya Karnataka nchini India, DV sadananda Gowda, amesema serikali yake iko tayari kutiliana saini na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya makubaliano ya mashirikiano katika Nyanja za elimu, viwanda na teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT).

Sadananda amemueleza makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif sharif hamad anayeongoza ujumbe wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar unaotembelea India huko Bangalore kuwa Karnataka imepiga hatua kubwa katika maeneo hayo na Zanzibar inaweza kunufaika chini ya makubaliano maalum.

Aidha, aliwataka wataalam wa sekta hizo tatu wafanye mazugumzo na ujumbe wa Zanzibar ili wajue mahitaji halisi ya Zanzibar, ambapo ujumbe huo wa Zanzibar katika mazugumzo na wataalam hao umeahidi kutumia fursa ya makubaliano hayo kupeleka watendaji wake na kujifunza mafanikio hayo katika mji mkuu wa Karnataka huko Bangalore.

Mapema, Maalim Seifakizungumza na waziri kiongozi huyo alisema malengo ya Zanzibar ni kuwa kituo maarufu cha teknolojia ya habari na mawasiliano katika eneo la Afrika ya Mashariki na Kati, sekta ambayo hivi sasa imekuwa kichocheo kikubwa cha ajira na mafanikio katika sekta zote za maendeleona uchumi.

Alisema mbali na Zanzibar kunufaika na utaalamu wa fani hizo kutoka Bangalore, lakini pia kuna fursa nyingi za uekezaji kwa wafanya biashara wa India katika visiwa vya Unguja na Pemba na wataweza kuichukuwa fursa ya kufunguliwa milago hiyo ya mashirikiano  kufungua vitega uchumi.

Maalim Seif alieleza  kwamba malengo ya Zanzibar kufanya ziara ya kujifunza katika miji ya India ni kupata utaalamu ambao baadae utapelekwa kwa wananchi wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji na wafanya biashara wadogo, kwa nia ya kuwawezesha kufanya shughuli zao kitaalamu na kwa mafanikio makubwa zaidi.

“Malengo ya serikali ya Zanzibar ni kupata ujuzi na uzoefu wa shughuli za kiuchumi, elimu na maendeleo kwa ujula na baadae ujuzi huu utapelekwa kwa wananchi moja kwa moja wakiwemo wazalishaji na vijana wanaomaliza mafunzo katika vyuo mbali mbali kwa nia ya kuinua maisha yao”, alisema maalim Seif.

Nae waziri wa elimu ya msingi na sekondari wa serikali ya Karnataka, Vishweshwar Hedge kageri amesema kuna fursa kwa Zanzibar kutumia ushirikiano uliopo kupeleka wanafunzi kujifunza elimu ya Teknolojia ya habari kwa sababu jimbo hilo limepata sifa kubwa duniani kote katika Nyanja hiyo pamoja na elimu kwa ujumla.

Alisema baadhi ya miji ikiwemo marekani imeamua kufanya tafiti mbal imbali katika sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano (IT&C) katika mji wa Bangalore kutokana na sifa uliyoipata kimataifa na kasi ya ukuaji wa teknolojia hiyo siku hadi siku.

Akizungumzia biashara, Katibu msaidizi wa shirikisho la wafanya biashara wadogo na wakati wa Karnataka, Dorothy Salkadanha amesema wanapendelea kutoa mafunzo kwa wazalishaji wanawake wa Zanzibar na kuomba kupewa maelezo ya kina juu ya harakati za wazalishaji hao wa Zanzibar.

Alieleza kwamba wanawake wa India wanaonesha ushindani mkubwa katika kazi za biashara na wanaweza kutoa ujuzi wao kwa wanawake wa Zanzibar na kuwawezesha kukuza biashara zao kwa faida yao na nchi yao.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s