CUF wawatuhumu CCM Igunga

CUF kimelitaka Jeshi la Polisi kumkamata na kumchukulia hatua kali, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana ya CCM Taifa (UVCCM), Martine Shigela kutokana na msafara wake kumshambulia kiongozi wa CUF. Akizungumza na waandishi wa habari Mjini hapa jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (bara), Julius Mtatiro, alisema kitendo cha msafara wa katibu huyo kushambulia mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CUF ni uchokozi usiokubalika.

”Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa chama chetu kutoka katika kijiji cha Iyogelo Tarafa ya Igurubi mjini hapa Salum Masanja (55) amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili kutokana na tukio hilo,”alisema Ntatiro. Habari zinasema Masanja alipigwa juzi majira ya saa tisa mchana nyumbani kwake katika Kijiji cha Iyogelo Kata ya Kining’inalo alipokuwa akipandisha bendera ya chake.

Akizungumza na Mwananchi hospitalini hapo, Masanja alisema alipigwa na watu wanne huku mmoja akimtambua baada ya kushuka kwenye gari moja jeupe lililokuwa kwenye msafara wa CCM. “Zilipita gari tatu nyeupe zikiwa zinapeperusha bendera za CCM, gari moja la nyuma lilisimama na watu wanne wakateremka na kunitaka kushusha benderea hiyo,”alisema Masanja.

Alisema baada ya kauli hiyo yeye alikataa ndipo walipompiga ngwala na kuanguka chini kisha kuanza kumshambulia kwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili na kumsababisha apoteze fahamu kwa muda wa saa mmoja. “Zilikuwa gari tatu zilizokuwa katika msafara wa CCM uliokuwa, ukiongozwa na Shigella, zilipofika karibu na mimi gari la nyuma lilisimama na watu hao kunifuata ndipo waliponiamuru nishushe bendera hiyo na kupandisha ya CCM,” alisema Masanja.

Alisema katika watu waliomshambulia alimtambua mtu mmoja aliyekuwa kiongozi wa msafara ambaye ni Katibu Mkuu wa UVCCM, Shigela.
Tamko la CUF
Chama cha CUF kimelaani tukio hilo na kulitaka Jeshi la Polisi kumkamata mara moja Shigela na kumchukulia hatua vinginevyo Igunga haitakalika. Mtatiro alionya kuwa CCM kama wafuasi wa CUF nao watajibu mapigo. Alisema CUF kwa sasa ni chama kisichopenda kuendekeza vurugu, lakini akasisitiza kuwa kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CCM ni uchokozi wa wawazi usikubalika.

“Martine Shigela anafahamika, na kama Polisi watashindwa kuchukua hatua sisi tutachukua hatua wenyewe, tuna uwezo huo na tukianza kuwapiga wafuasi wa CCM tutawashambulia jimbo zima,”alisema Mtatiro. “Sisi tumekaa kimya muda wote siyo hatuwezi kufanya vurugu, bali tunapambana kuona sheria, kanuni na taratibu zinafuata katika nchi hii, tunaliomba Jeshi la Polisi kuchukua hatua na kama halitachukua hatua sisi CUF tunafanya kazi hiyo wenyewe,”alisema Mtatiro.
Mtatiro alisistiza kuwa chama chao hakipo Igunga kwa ajili ya kufanya vurugu bali kampeni za kistaarabu za kutangaza sera zake na kutaka mbunge wao achaguliwe na wananchi Majira ya saa 4:00 asubuhi Mtatiro akiwa ameongozana na wajumbe mbalimbali wa CUF akiwamo Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama hicho Mkoa wa Tabora Magdalena Sakaya, walivamia Hodi za Hospitali ya Wilaya na kukuta majeruhi hiyo akiwa hajapatiwa tiba tangu kufikishwa kwake hosipitalini hapo juzi saa 12.00.

Kamishina Msaidizi wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Telesphory Anacleth, alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa tayari hatua za awali zimechukuliwa. Alisema mara baada ya kupata taarifa hizo Polisi walifika eneo la tukio juzi na kufanya mahojiano na Masanja pamoja na watu mbalimbali na kwamba jeshi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na tayari limeshafungua kesi ya shambulio la kudhuru mwili.

Mgombea acharuka
Baada ya kupata taarifa za kupigwa kwa kiongozi huyo, mgombea wa CUF, Leopold Mahona alizungumza kwa ukali na kusema atakuwa wa kwanza kuvuruga uchaguzi huo kama hatua hazitachuliwa dhidi ya wahusika.
Alisema yeye anagombea ubunge ili awatumikie wananchi na watu wanapowashambulia wanataka aje kumtumikia nani katika utumishi wake.
“Nimesikitishwa na tukio hilo, mimi nagombea ili niwatumikie wananchi ili waondokane na umasikini unaotukabiri, inapotokea CCM wanakwenda kuwapiga na kuwadhuru wanataka mimi niwatumikie wakinanani, ninachosema CCM waombe radhi kwa hili, la sivyo uchaguzi hautafanyika,”alisema Mahona alipokuwa akihutubia wakazi wa kata ya Nyandekwa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s