Seif: Nitaifumua ZEC

Saturday, 18 September 2010

Sadick Mtulya, Zanzibar

MGOMBEA wa kiti cha Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya CUF , Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kama atachaguliwa, atatumia miaka mitatu kuunda katiba mpya ya serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar.

Pia, amesema atabadilisha mfumo wa uteuzi wa makamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) ili kuifanya kuwa huru na inayojitegemea.

Maalim Seif aliyasema hayo jana, alipokuwa akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika katika Hoteli ya Bwawani mjini Unguja.

Mgombea huyo alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uongozi mwema na maridhiano yaliyofikiwa na vyama vya CCM na CUF, katika kumaliza migogoro ya kisiasa visiwani Zanzibar.

“Nikiingia madarakani, nitatumia muda wa miaka miwili hadi mitatu, kuhakikisha kuwa tutafanya mabadiliko ya katiba kwa kuunda katiba mpya ya Muungano na ya Zanzibar,” alisema Maalim Seif.

Alisema kwa upande wa Zanzibar, ubadilishwaji wa katiba utakuwa rahisi lakini kwa upande wa Muungano, atalazimika kwanza kukubaliana na upande wa serikali ya Muungano.

“Pamoja na kwamba mwelekeo wa CCM katika kubadili katiba ni mgumu, lakini tutawasilisha hoja ya maalumu kudai hilo,” alisema Maalim Seif.

Kuhusu kulinda Muungano, Maalim Seifa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alisema utalindwa na kuwa wa manufaa kama kutakuwa na serikali tatu zitakazotengeneza shirikisho.

“Muungano utaboreka kwa mazungumzo ya kina ya pande mbili yatakayosaidia kuundwa upya kwa Muungano na kuondoa kero zake ikiwa ni pamoja na kuangaliwa upya kwa mambo yote yalioongezwa baada ya muungano wa mwaka 1964,” alisema.

Kuhusu Zec, alisema atahakikisha kuwa inakuwa huru na kutengewa bajeti yake.

“Kwa sasa bajeti ya Zec, ipo chini ya Waziri kiongozi. Utaratibu huu utabadilishwa ili ijitegemee. Bajeti yao itapitishwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na itakwenda moja kwa moja katika idara hii,” alisema

Akizungumzia muundo wa Zec, alisema makamishina wake watapatikana kwa kuridhiwa na vyama vyote vya siasa.

“Kila chama kitawakilisha majina ya watu wake kwa Rais na kisha nitapendekeza majina ya makamishna hao na kuyarudisha kwa vyama, wakiridhia ndio watatangazwa,” alisema Maalim Seif.

SOURCE: MWANANCHI

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s