Maalim Seif: Nitafuta michango ya elimu

Na Hassan Shaaban, Zanzibar

MGOMBEA urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), ametangaza kufuta michango yote katika sekta ya elimu mara atakapochaguliwa kuwa Rais, ili kuwawezesha maskini kunufaika na elimu.

Akizindua kampeni katika viwanja vya Kibandamaiti, Maalim Seif alisema michango katika sekta ya elimu imekuwa ikiwanyima fursa wananchi wanyonge kupata haki ya elimu.

Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ilitangaza elimu kuwa bila ya malipo, lakini wananchi wanatoza michango mingi na kusababisha wanyonge kutokuimudu.

Alisema elimu ndiyo injini katika kupambana na umaskini na iwapo wananchi watapata elimu nzuri mpango wa kuondoa umaskini utaweza kufanikiwa.

Alisema mbali ya tatizo la michango, mazingira ya kusomea Zanzibar sio mazuri kwa vile darasa moja linabeba wanafunzi wapato 80.

Alisema hali hiyo, imekuwa ikiwapa wakati mgumu walimu kufundisha kwa ufanisi na malengo ya CUF, darasa moja linatakiwa lisizidi wanafunzi 35.

Alisema serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, chini ya uongozi wake italeta mabadiliko makubwa katika sekta hiyo, ikiwemo kumwezesha kila mwanafunzi kuwa na kompyuta yake.

Alisema wakati huu ambapo dunia iko katika mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia wanafunzi lazima wajue kutumia kompyuta ili waende sambamba na wakati uliopo.

Alisema serikali ya umoja wa kitaifa itaandika misingi ya utawala bora, ikiwemo kuweka mazingira mazuri kwa watumishi wake na kusimamia kwa karibu suala la uwajibikaji kazini.

“Viongozi wa juu itakuwa hakuna kulala chini ya serikali ya umoja wa kitaifa iwapo mtanipa ridhaa ya kuongoza,” alisema mgombea huyo katika mkutano ambao ulihudhuriwa na mamia ya wanachama na wafuasi wa chama hicho.

Maalim Seif, aliwaahidi wananchi atahakikisha hoja ya serikali tatu ndani ya mfumo wa Muungano, inapewa muhimu na pande mbili za Muungano kwa nia njema na kuimarisha Muungano wenyewe.

Hata hivyo, alisema atatetea hadhi ya Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano, kwa vile utaratibu huo ndio msingi wa makubaliano ya Muungano huo wa mwaka 1964.

Alisema kuondolewa kwa wadhifa wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais hakuleti sura nzuri na kumpunguzia hadhi yake.

Kuhusu kuimarisha utawala bora, atahakikisha Wazanzibari wote wanapatiwa vitambulisho vya Uzanzibari pamoja na hati za kusafiria, kwa vile ni haki yao.

SOURCE: TANZANIA DAIMA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s