Nafasi pekee ya kuleta mabadiliko Zanzibar

Mtazamo wetu ni kwamba Wazanzibari tutakuwa na nguvu na sauti licha ya udogo wetu ikiwa tutakuwa na mfumo shirikishi baada ya tenganishi na kwamba tunaweza kuyafikia, kwa umoja wetu, mengi ambayo hatukuweza kuyafikia kwa kugawanyika kwetu. Ni CUF pekee kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoweza kuyaleta haya. Maridhiano yetu na mafahamiano yetu juu ya malengo na dhamira zetu ni kuamini kwamba tunaweza kuingiza shauku na hamu mpya katika utungaji wa sera bora zenye nia ya kuleta mabadiliko ya haraka na ya maana yenye tija na neema kwa wananchi wote. Changamoto pekee itakayobaki itakuwa ni kusimamia na kufuatilia utekelezaji wake. Ni CUF kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa pekee inayoweza kuyaleta haya.

Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad

Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hammed

Jumapili ya Oktoba 31, 2010 tutapiga kura kwa mara nyengine tena kuchagua Serikali itakayotuongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Wengi wenu mtakao kuwa mnapiga kura siku hiyo, hamkuwahi kushuhudia kitu kingine zaidi ya serikali ya CCM.

Lakini hivi karibuni, nyote mmeshuhudia historia ya Zanzibar ikiandikwa upya pale vyama vya CUF na CCM vilipokubaliana kuongoza nchi kwa mtindo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo vyama vyote vitakavyopata ridhaa ya wananchi na kuingia katika Baraza la Wawakilishi vitakuwa na nafasi ya kushiriki katika uendeshaji wa Serikali.

Serikali ya aina hiyo inahitaji umakini mkubwa katika kuisimamia na kuiongoza ili iweze kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na yanayohitajika Zanzibar. Kuichagua CUF kuiongoza Serikali hiyo ni nafasi pekee ya mabadiliko ya kweli.

Mfumo wetu wa kisiasa unahitaji upepo mpya wa mabadiliko wenye nguvu ya kuisafisha jamii yetu na kuleta mawazo na fikra mpya, kuleta viongozi na watu walioungana na wenye dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya maana, na ambao wanathamini utu na heshima ya binaadamu,wanaofahamu maana hasa ya utumishi wa umma na uwajibikaji. Ni CUF pekee kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoweza kuyaleta haya.

Mtazamo wetu ni kwamba Wazanzibari tutakuwa na nguvu na sauti licha ya udogo wetu ikiwa tutakuwa na mfumo shirikishi baada ya tenganishi na kwamba tunaweza kuyafikia, kwa umoja wetu, mengi ambayo hatukuweza kuyafikia kwa kugawanyika kwetu. Ni CUF pekee kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoweza kuyaleta haya. Maridhiano yetu na mafahamiano yetu juu ya malengo na dhamira zetu ni kuamini kwamba tunaweza kuingiza shauku na hamu mpya katika utungaji wa sera bora zenye nia ya kuleta mabadiliko ya haraka na ya maana yenye tija na neema kwa wananchi wote. Changamoto pekee itakayobaki itakuwa ni kusimamia na kufuatilia utekelezaji wake. Ni CUF kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa pekee inayoweza kuyaleta haya.

Nchi yetu ina utajiri mkubwa. Ikiwa tutaziruhusu na kuziachia nguvu, vipaji na taaluma za watu wetu, na kuthamini na kuheshimu utajiri mkubwa wa mchanganyiko wa makabila na asili za watu wetu badala ya kuzitumia kuwagawa watu, basi kuna mambo mengi makubwa tunayoweza kuyafikia na kuushangaza ulimwengu. Ni CUF pekee kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoweza kuyaleta haya.

Katika kurasa hizi, tunakuelezeni kwa muhtasari tu baadhi ya yale mambo muhimu yanayowagusa Wazanzibari wenzetu na ambayo tunakusudia kuwatekelezea katika kipindi cha miaka mitano ijayo kupitia ridhaa yenu mtakayotukabidhi Oktoba 31, 2010. Ni CUF pekee kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoweza kuleta haya.

Nayaleta kwenu, kwa niaba ya wenzangu, muyapokee na muyakubali kwa kutupa kura zenu na imani zenu ili CUF iongoze Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayosimamia na kuyatekeleza haya kwa dhati. Hatuwaombi kingine chochote zaidi ya nafasi ya kuwatumikia.

Kwa kuyatekeleza haya tuliyoyaeleza humu ambayo tunayakubali na kuyayakinisha kwenu kwamba ni mkataba kati yetu na wapiga kura, tunakusudia kuijenga Zanzibar mpya.

Tunataka kuijenga Zanzibar mpya itakayofikia kule ambako Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, alitaka kila Mzanzibari afikie na kujinasibu nako, hayo yakiwa ndiyo malengo ya Uhuru waliokuwa wakiupigania wazee wetu hao. Katika Ilani ya Uchaguzi ya ASP ya mwaka 1961, Mzee Karume aliieleza vyema Zanzibar hiyo kwa maneno yafuatayo:

“UHURU ndio msingi wa siasa ya chama chetu. Unachanganya bila ya shaka kumalizika kwa Serikali ya Kikoloni na mwisho wa utawala wa nje. Kadhalika UHURU unakusanya ukunjufu kutokana na ujinga na haja zisizokwisha. UHURU wa kuwa na pato la kumwezesha mtu kuyatekeleza yaliyombidi, kustarehe na kuwa mtu, uhuru wa kuishi kama watu katika nchi yetu.

“Huu ndio UHURU ambao daima tukiutaka, huu ndio UHURU ambaodaima twaupigania, huu ndio UHURU ambao tumejitolea kuutumikia na siku zote tutautumikia kwa nguvu zetu zote na kwa uwezo wetu wote.

“Tunadhani kuwa kila mmoja wetu katika visiwa hivi aendelee mbele kwa mujibu wa uwezo wake, jambo ambalo ni gumu lakini kabisa si jambo lisilowezekana. Na iwapo wewe Kilillahi huyapingi haya tuliyoazimia na wewe mwenyewe ndiye uwezaye kujua, basi tafadhali karibu
uungane nasi twende pamoja na kuutia mkononi huu UHURU.”

Wazee wetu waliupigania na kuutia mkono UHURU huu. Sasa ni wajibu wetu sisi kuulinda na kuendeleza pale walipotuachia ili tuyafikie kweli malengo ya UHURU huo walioupigania kama alivyoyaeleza Marehemu Mzee Karume.

Naamini tukiyasimamia na kuyatekeleza vyema haya tuliyoyaeleza katika Ilani hii ambayo ni Dira ya Mabadiliko tunayowazadia Wazanzibari, basi tutaweza kuyafikia malengo hayo.

Tukiwa tumeungana, tunakupeni Wazanzibari nafasi pekee ya kuleta mabadiliko ya kweli.

Seif Sharif Hamad
10 Septemba, 2010

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s