Mtanzania zinduka, mabadiliko yanawezekana

Ufisadi na rushwa zinaendelea kuimarika nchini na CCM imegawika mapande mapande. Watanzania tutajuta ikiwa tutaruhusu wizi wa kura na kuipa fursa CCM kuendelea kutawala. CCM haina dira ya kuongoza nchi na kusimamia utawala bora. Imeshindwa kutumia utajiri mkubwa tulionao wa raslimali na maliasili ya Taifa kwa manufaa ya wananchi wote na badala yake leo Tanzania imegeuka kuwa omba omba na Matonya wa kimataifa.

mwenyekiti wa CUF taifa, Professa Ibrahim Harouna Lipumba

Mwenyekiti wa CUF taifa, Prof. Ibrahim Harouna Lipumba

Kwa mara nyingine tena ifikapo Oktoba 2010 wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tutapiga kura kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani wa nchi yetu. Huu utakuwa ni Uchaguzi Mkuu wa nne kufanyika nchini chini ya mfumo wa vyama vingi.

Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wakati nchi yetu ikiwa njia panda. Watanzania wamechoshwa na hadaa na ngulai za CCM. Umaskini unaongezeka, ajira zimetoweka, ufisadi na rushwa vimekithiri. Ahadi ya CCM ya mwaka 2005 ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania” imeishia kuwa Maisha bomu kwa kila Mtanzania. Serikali ya CCM imeshindwa kuboresha maisha ya Mtanzania.

Hali ya maisha imezidi kuwa ngumu. Mwaka 2005 kilo moja ya sukari iliuzwa shilingi 500/- lakini hivi sasa inauzwa shilingi 1800/- na vijijini ni zaidi ya shilingi 2000/-, mchele ulikuwa unauzwa kilo moja shilingi 450/- lakini hivi sasa unafika shilingi 1700/-, kilo moja ya sembe ikiuzwa shilingi 250/- lakini hivi sasa ni shilingi 900/-, Wafanyakazi wanapodai kuongezewa mishahara kwa sababu ya kupanda kwa gharama za maisha wana sababu za msingi kabisa kufanya hivyo kutokana na hali halisi ya kupanda kwa gharama za maisha.

Ufisadi na rushwa zinaendelea kuimarika nchini na CCM imegawika mapande mapande. Watanzania tutajuta ikiwa tutaruhusu wizi wa kura na kuipa fursa CCM kuendelea kutawala. CCM haina dira ya kuongoza nchi na kusimamia utawala bora. Imeshindwa kutumia utajiri mkubwa tulionao wa raslimali na maliasili ya Taifa kwa manufaa ya wananchi wote na badala yake leo Tanzania imegeuka kuwa omba omba na Matonya wa kimataifa.

Watanzania wameweka matumaini yao kwa Chama cha CUF na misingi yake ya sera ya kuleta “Haki sawa kwa wananchi wote” na “Kujenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa wote.” Chama chetu kimekuwa ni Chama kikuu cha upinzani nchini kwa muda mrefu sasa na wananchi wanaendelea kuteseka kwa kuona matatizo yao yakizidi kuongezeka bila kuchukuliwa kwa hatua za msingi kushughulikia matatizo yao. Hali hii inawafanya wananchi wengi hasa vijana na wanawake kuwa katika shauku kubwa ya kuona utawala wa nchi yetu unabadilishwa kwa amani kupitia karatasi za kura.

CUF kwa kutambua nafasi yake katika kuyaongoza Mabadiliko yanayohitajika, kikiwa siyo tu chama kikuu cha upinzani hapa nchini bali pia kutokana na mjengeko wake wa kuwa kweli ni chama cha kitaifa chenye kukubalika na chenye mtandao mpana katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano, imezindua DIRA YA MABADILIKO – VISION FOR CHANGE. Dira ya Mabadiliko ndiyo msingi wa ILANI yetu ya uchaguzi. Vision for Change chini ya Serikali ya CUF itatujengea Tanzania Mpya inayojali haki sawa kwa wananchi wote na itakayojenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa wote.

Mambo muhimu yaliyobebwa na Dira ya Mabadiliko ni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kutokomeza njaa na kuhakikisha lishe bora kwa wajawazito na watoto, kutoa huduma bora ya afya na kudhibiti vifo vya wajawazito na watoto, kuwahudumia wazee waliolitumikia Taifa letu, kuwasaidia walemavu na kuwawezesha kupata elimu na ajira, kusimamia elimu bora na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano;, kusimamia maendeleo ya kiuchumi nchini; usimamizi makini katika sekta ya kilimo na maendeleo ya viwanda; kuimarisha miundo mbinu na kuhamasisha uwekezaji; na usimamizi wa Rasilimali za Taifa na Nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.

Bado nina moyo ule ule niliokuwa nao mara tatu nyuma nilipoomba kuitumikia nchi yetu. Bado CUF ina dhamira ile ile ya kuibadilisha nchi hii kuwa mahala bora pa kuishi kwa kila Mtanzania. Nguvu ya kutuwezesha kutimiza azma na dhamira zetu njema imo mikononi mwako, ewe mpiga kura wa Tanzania. Fanya uamuzi wa busara ifikapo Oktoba 31 mwaka huu kwa kuchagua Dira ya Mabadiliko. Kwa kuichagua CUF. Kwa kumchagua Lipumba.

Ibrahim Haruna Lipumba
Agosti 26, 2010
Dar es Salaam

Kwa kuisoma Manifesto nzima, bonyeza hapa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s