Lipumba: Siamini kama haya ni maamuzi ya NEC

Wednesday, 17 February 2010 06:27
Na Dunstan Bahai

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema hakiamini kama Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) inaweza kupingana na maamuzi yaliyokwisha amuliwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu serikali ya mseto.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na gazeti hili.

“Ninaamini wajumbe wa NEC ya CCM ni makini sana, siamini kama wanaweza kutoa maamuzi yanayopingana na yale yaliyokwishaamuliwa na Baraza la Wawakilishi,” alisema huku akionyesha wasiwasi mkubwa.

Baraza la Wawaklishi Zanzibar katika vikao vyake vya hivi karibuni wajumbe walikubaliana kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ingawa taarifa zilizoandikwa na vyombo vya habari jana vilieleza kuwa NEC imepitisha uamuzi huo lakini baada ya kura za maoni zitakazopigwa baada ya Uchaguzi Mkuu.

Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, si Kamati, Halmashauri Kuu ya CCM wala kikao chochote kinachoweza kutoa maamuzi tofauti na yale ya Baraza la Wawakilishi kuhusu hoja ya kuwepo kwa serikali shirikishi.

Alisema hawezi kuwa na kauli yoyote juu ya maamuzi hayo yanayodaiwa kutolewa na NEC kwa kile alichoeleza kuwa hana ushahidi nacho.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s