Maridhiano ya Wazanzibari: Ufafanuzi wa taarifa za magazeti

MARIDHIANO YA WAZANZIBARI: UFAFANUZI 24 Januari 2010

Kutokana na kuwepo kwa wimbi la upotoshaji wa habari zinazohusu Maridhiano ya Wazanzibari katika vyombo mbali mbali vya habari, Kurugenzi ya Uenezi na Mahusiano na Umma ya Chama cha Wananchi (CUF) imeamua kutoa ufafanuzi ufuatao kwa makusudi ya kuweka rekodi sawa:

1. Suala la Maridhiano haya ni la Wazanzibari wote kwa ujumla wao. Lolote zuri linalohusiana nayo ni kwa maslahi ya Wazanzibari wote; na sio kwa CUF tu au CCM tu. Vile vile kama litafeli au kufelishwa kwa makusudi, basi hasara yake itakuwa ni kwa Wazanzibari wote; na sio kwa CUF tu au CCM tu. Kwa sababu hiyo, ndiyo maana CUF kama Chama, haina lolote la kusherehekea au kulilia peke yake; kwani furaha au kilio cha Maridhiano haya ni kwa Wazanzibari na Watanzania wote kwa pamoja. CUF haijapanga sherehe wala kujiundia Baraza la Mawaziri; kwani hivyo ni vitu vidogo mbele ya maslahi ya nchi, ambayo CUF inasimamia

2. Aina ya uandishi inayoshuhudiwa sasa katika vyombo vyetu vya habari inaashiria kwamba, aidha vyombo hivi havijaelewa malengo halisi ya Wazanzibari na au vinafanya kusudi kuzidhoofisha juhudi za Wazanzibari kujiandikia historia mpya. Huko ni kupotoka na ni kupotosha maadili ya uandishi wa habari, ambao unatakiwa sana kuzingatia maslahi ya umma. Maslahi ya Zanzibar ni makubwa na ya muda mrefu kuliko chochote na hilo ni vyema likafahamika hivyo

3. CUF inaendelea kusimamia kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Kikwete, juu ya Maridhiano hayo, ambayo ilitamka kwamba ni wajibu wa kila mmoja kuyaunga mkono na kumdharau yule anayeyabeza.

Pamoja na salamu za Chama.

Imetolewa na:
Salim Bimani
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma, CUF
Simu: +255 777 414 112
Zanzibar

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s