Maandamano kuunga mkono Seif, Karume

Friday, 13 November 2009 08:33
Mwajuma Juma, Zanzibar na Rabia Bakari, Dar

SIKU chache baada ya wafuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF) kutaka kumshambulia Katibu Mkuu wao, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kukubali kumtambua Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, jumuiya za chama hicho zimetangaza kuunga mkono hatua inayoashiria muafaka mpya.

Wakati Jumuiya ya Wanawake wa chama hicho (UWCUF) Zanzibar imeandaa maandamano ya kuunga mkono mazungumzo hayo, ile ya vijana imempongeza Maalim Seif kwa hatua hiyo.

Maandamano ya wanawake hao yamepangwa kufanyika Jumapili na kupokewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Machano Khamis Ali, yakiwa na ujumbe wa kuwaeleza wafuasi hao faida ya muafaka huo.

Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma Bw. Salim Bimani aliwaambia waandishi wa habari jana, matayarisho yote yameshakamilika na mzungumzaji mkubwa atakuwa Maalim Seif Sharif Hamad.

“Lengo kubwa ni kuunga mkono mazungumzo ya viongozi ambayo yamesaidia CUF kuondosha mpasuko wa kisiasa siku nyingi na sasa Wazanzibari wameamua kuungana na kusahau tofauti zao,” alisisitiza Bw. Bimani.

Alisema mbali na maandamano hayo viongozi wa kitaifa wameanza kufanya ziara za kutembelea majimbo na kukutana na wanachama ili waweze kuwafahamisha sababu zilizofanya Baraza Kuu la Uongozi wa CUF kumtambua Rais Karume.

Maandamano hayo yataanzia Uwanja wa Komba Wapya, kupitia Mikunguni na kumalizikia Viwanja vya Kibandamaiti.

Wakati hayo yakiripotiwa Zanzibar, jijini Dar es Salaam, Sekretarieti ya Vijana wa CUF imetoa pongezi kwa Bw. Hamad kwa hatua aliyofikia.

Mwenyekiti wa Sekretarieti hiyo, Bw. Mohamed Babua alisema kuwa hiyo ni njia muafaka ya kufikia suluhisho la amani visiwani humo.

“Kitendo cha kukutana kwa Maalim Seif na Rais Karume na hatimaye CUF kuitambua serikali ya Rais Karume ni ishara njema ya kulimaliza tatizo la Zanzibar,” alisema Bw. Babu.

Aliongeza kuwa matatizo ya kisiasa visiwani Zanzibar yamefikia katika hali mbaya sana na ni viongozi pekee wanaotakiwa kuchukua hatua madhubuti za kumaliza tatizo hilo.

“Watu wamekuwa wakipigwa mara kwa mara, kujeruhiwa vibaya, kukamatwa na kukoseshwa haki yao ya msingi ya kuandikishwa kupiga kura. Vijana wa chama cha CUF tunaamini matatizo haya na mengine yatamalizika kutokana na kitendo cha CUF kuitambua serikali ya Rais Karume na tunatoa wito kwa wanachama wote kwa ujumla kutoa nafasi kwa viongozi wetu wafikishe mwisho hatua waliyoanza ili kumaliza kabisa mtafaruku wa kisiasa Zanzibar,” alisema.

Novemba 5 mwaka huu, Rais Karume alikutana na Maalim Seif kuzungumzia mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar ambayo pende zote mbili zilisema ni ya mafanikio makubwa.

Chanzo: Copied from Zanzinet.net

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s