Maalim Seif, Karume wakutana Ikulu

Thursday, 05 November 2009 17:06
Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar Bw. Amani Abeid Karume jana alikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Ikulu, mjini Zanzibar ambayo chama hicho cha upinzani kimesema ni ya ‘maelewano makubwa’.

Mazungumzo hayo, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Zanzibar, yaligusia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na ushirikiano kati ya wananchi wote.

Viongozi hao wamezingatia haja ya kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha Wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla, kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.

Viongozi hao walifafanua kuwa wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walihusisha umuhimu wa mchakato wa mazungumzo endelevu baina yao na vyama vyao kwa jumla.

Akizungumza na gazeti hili jioni jana, Msaidizi wa Maalim Seif, Bw. Ismail Jusa alisema mazungumzo yamekuwa ya mafanikio makubwa na wameahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta umoja na ushirikiano kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar.

Chanzo: http://www.btl.co.tz/

Advertisements

4 thoughts on “Maalim Seif, Karume wakutana Ikulu

 1. Tunafurahi viongozi wetu 2 kukutana kwa manufaa ya nchi yetu Zanzibar Mungu alete kheri zake Amin.

  But still I have doubt maalim una waamini CCM? Yasije yale yaleee ya kina Makamba wanakucheza shere na isiwe changa la macho.

  Hatuombi shari tunaomba kheri siku zote na tunakuona juhudi zako kuleta kheri kwa Wazanzibari na Tanzania kwa ujumla – but unawaamini hao?????

  • Bi Fatma Nasser,

   Shukrani kwa kuniunga mkono katika wakati huu mgumu na muhimu kwetu na kwa nchi yetu. Napenda kukuhakikishia kuwa hakuna chengine chochote ambacho mimi kama Maalim Seif nakiamini kuliko maslahi ya nchi yetu ya Zanzibar. Na kwa hilo hatuna la kupoteza. Tuwape wenzetu fursa ya kuthibitisha kwamba tunasimama pamoja kuitakia kheri nchi yetu, na kwa pamoja tutashinda. Hatutafeli kamwe!

   Maalim

 2. A/A KWANZA NAPENDA KUMSHKURU M/MUNGU NA BW MTUME(S.A.W).LA PILI NA PENDA KUWASHKURU MSH AMANI NA MALIM SEIF NA UONGOZI WOTE WA CUF KWA KUSHUKUA HATUA HII MZITO.HII YOTE NI KUNUSURU MAUWAJI NA MAFA WANANCHI TAYARI WALIKWISHA ONA ISHARA NA DALILI MBELENI.LAKINI TU WZANZIBAR WANAPENDA AMAN NA KUISHI KTK AMAN.KUPWA NI KAMA MSH AMANI ANAPENDA AMANI NA NUSURA YA VISIWA HIVI BASI NI KUFANYA SEREKALI YA MSETO KABLA YA USHAGUZI WA 2010 KWA VILE WAZANZIBAR WENGI WANAPENDA HILO NA LITAEPUSHA SHAKA YA KUGEUKIANA.

 3. ASSALAM ALAYKUM. KWANZA KABISA NAPENDA NICHUKUWE FURSA HII KWA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHMA KWA KUNIWEZESHA KUWEZA KUANDIKA BARUA HII NA INSHALLA MUNGU AKUJAALIE IKUINGIE VYEMA AKILINI MWAKO. MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD KIPENZI WA WAZANZIBARI WOTE WAPENDA AMANI NA UTULIVU. MAALIM MIMI NI KIJANA MDOGO WA UMRI WA MIAKA 27 ILA ALHAMDULILLAH NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA KICHWA KIZURI CHENYE AKILI ZA KUVUMBUWA MAMBO MBALI MBALI YA KIMAENDELEO. LAKINA KWANZA NIKUPE POLE NA HONGERA KWANI WEWE HATA KAMA HUJATANGAZWA KUWA RAIS LKN TEYARI ULIMWENGU UNAFAHAM KUWA WEWE NI MSHINDI WA MAISHA PAMOJA NA NAFSI. KWANI KATIKA MAISHA YETU WANADAM UKIWEZA KUISHINDA NAFSI YAKO BASI TAYARI WEWE NI KTK WATU MAJABARI NA WAJASIRI WA HALI YA JUU KABISA KABISA KABISA. MAALIM TUYAWACHE HAYO: NAKUMBUKA KATIKA MANENO YAKO AMBAYO MARA NYINGI ULIKUWA UNAYESEMA AU KWA MIMI NATHUBUTU KUSEMA KUWA ILIKUWA NDO NYIMBO YAKO MWENYEWO NA SIO JENGINE BALI NA SUALA ZIMA LINALOHUSU AJIRA KWA VIJANA WA WAZANZIBARI WOTE KWA UJUMLA BILA KUJALI ITIKADI ZAO. NA PIA MAALIM ULIKUWA UKIIMBA SANA SUALA LA KUWAUNGANISHA WAZANZIBARI WOTE KWA UJUMLA. NA ALHAMDULILLAH KWA HILO MUNGU KAKUUNGA MKONO PAMOJA NA WAZANZIBARI WOTE KWA UJUMLA NA NDO MANA WAKAKUCHAGUA KATIKA UCHAGUZI MKUU ULOPITA WA TAREHE 31 OCT 2010. SASA MAALIM KATIKA HILI SUALA YA AJIRA KWA VIJANA MIMI NAKUOMBA NIPITISHE MSAADA KWAKO KWA NIA SAFI KABISA. MIMI NAKUOMBA UNIPE RUHUSA NIWAORODHESHE VIJANA WOTE WA JIMBO LA BUBUBU BILA KUJALI VYAMA VYAO NA DINI ZAO. BAADA YA HAPO KINACHOENDELEA NITABUNI MIRADI MBALI MBALI AMBAYO ITATOSHELEZA KWA MUJIBU WA IDADI YA VIJANA HAO AMBAYO 99% YA VIJANA HAO. ILA SIISHII HAPO BALI ITABIDI UTUUNGE MKONO KWA KUTUTAFUTIA MISAADA YA NAMNA MOJA AMA NYENGINE NIKIMAANISHA NDANI YA NCHI NA NJE YA NCHI. MAALIM MIRADI IPO MINGI SANA TENA YENYE TIJA. NA WASHUGULIAJI ALHAMDULILAH TUPO TENA TUPO MAKINI KISAWA SAWA! NA HAPO MAALIM NDIPO MAALIM UTAKAPOPATA JAWABU LA ILE NYIMBO YAKO NYENGINE UNAYOIMBA KUWA “NITAHAKIKISHA NA SITAPUMZIKA MPAKA NIMUONE KILA KIJANA ANA KAZI YENYE TIJA. NA KILA MWANANCHI ATASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUIJENGA ZANZIBAR YETU MPYA INSHALLAH. SAWA SAWA??” MAALIM WANANCHI WA ZANZIBAR TUMEZIDI KUJENGA MAPENZI NA WEWE BAADA YA MAAMUZI MAZITO ULOYA CHUKUWA SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 01 NOV 2010 MAJIRA YA SAA 2 ZA USIKU. MUNGU AKUZIDISHIE UMRI NA MAPENZI YAKO KWA ZANZIBAR NA KWA WAZANZIBARI WOTE KWA UJUMLA. AAMIN. NI MIMI YASIR HASHOUL NASSOR. ASSALAM ALAYKUM:

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s