Zanzibar: Tusipoziba ufa tutajenga ukuta

Na Nizar Visram

HAKUNA anayeweza kukataa kuwa Zanzibar inaelekea kubaya, kuwa hali ya visiwani inatia wasiwasi. Zoezi linaloendelea la kujiandikisha katika daftari la wapigakura limetawaliwa na mabomu, risasi, helikopta, uchomaji moto, mapigano, ukamataji wa raia na vitisho vya kuua.

Hapo awali tuliambiwa Pemba ndiko kwenye vurugu. Tukasikia na Unguja nako katika kisiwa cha Tumbatu polisi wanamimina mabomu ya machozi kutoka helikopta. Tunaambiwa polisi inashindwa kuwatawanya wananchi kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na ndipo risasi za moto zinafyatuliwa.

Vilio vya akinamama na watoto kutokana na hofu ya milio ya risasi na nyumba kuungua moto ni sehemu ya patashika lililoendelea katika uandikishaji katika jimbo la Tumbatu.

Askari polisi (FFU) na kikosi cha KMKM huacha eneo la uandikishaji na kuelekeza mabomu yao kwenye makazi ya wananchi na kusababisha baadhi yao kupoteza fahamu na wengine kupanda maboti na kukimbia. Mkazi mmoja wa Tumbatu mtu mzima alikimbizwa kituo cha afya baada ya kupoteza fahamu.

Akina mama wakiwa wamewabeba watoto wao migongoni pamoja na wazee wanaonekana kukimbilia vichakani ili kuokoa maisha yao kutokana na hofu ya mabomu na risasi za moto.

Tunaambiwa kundi la wafuasi wa CUF na CCM wanarushiana mawe, wanatwangana makonde na kupambana kwa silaha za kienyeji na kusababisha baadhi yao kujeruhiwa. Mwanamke mmoja aliyejeruhiwa na jiwe alikimbizwa hospitali.

Huko Pemba nako baadhi ya wakaazi tunaambiwa wamelazimika kuyakimbia makazi yao na kuhamia porini kwa vile polisi wanawavamia majumbani mwao usiku wa manane. Tunaambiwa katika kamata kamata hiyo polisi wanavamia nyumba za baadhi ya viongozi wa “chama kimoja cha siasa.”

Wakati wote huo magari ya polisi yaliyokuwa na vitambaa vyekundu na magari ya msalaba mwekundu yamekuwa yakiranda mitaani.

Yote haya yanafanyika wakati wa kuandikisha wapigakura. Uchaguzi wenyewe bado. Hata kampeni bado. Hii ni hatua ya mwanzo tu ya kuandikishwa kwa wapiga kura. Tufikirie kitakachotokea siku za usoni, hasa tukizingatia historia ya kisiasa visiwani Zanzibar.

Rais Jakaya Kikwete alikubali kuwa kuna mpasuko huko Zanzibar. Akaahidi kuwa atafanya kila juhudi kutafuta suluhisho. Akaanzisha mazungumzo ya Mwafaka. Wakati wa kutiliana saini ulipowadia chama chake ‘kikaruka kimanga.’

Vurugu hii ya sasa huko visiwani isingetokea kama Mwafaka ungetekelezwa. Hata hivyo kuna haja ya Rais Kikwete kuingilia kati na kutatua matatizo. Haya si mambo ya ndani kwani jeshi la polisi linalotumiwa huko Zanzibar ni la Muungano.

Wanaojiandikisha wanafanya hivyo ili wachague Wabunge na Rais wa Muungano.

Iweje sasa tatizo hilo aachiwe Rais Amani Karume peke yake? Yeye alipobanwa na wafadhili kama kawaida yao mara moja akawaalika Ikulu Zanzibar na akatoa amri kuwa vitambulisho vya ukaazi vitolewe bila ya usumbufu. Wafadhili wakanywa chai na kisha kuendelea kumwaga mabilioni.

Wanaotegemea kuwa wafadhili wataingilia kati wanajidanganya.

Hawakufanya hivyo tangu 1995 kwa sababu wao wanaangalia maslahi yao ya kitaifa. Wataingilia kati pale tu maslahi yao yatakapohatarishwa. Si Kenya, si Zimbabwe wala si Zanzibar

Sasa tunaona Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Polisi (IGP) wanatembelea Zanzibar na kukutana na makamanda wa polisi. Kisha wanatoa onyo kuwa polisi itajizatiti kuzuia vurugu.

Atakayevuruga amani atakiona kilichomtoa kanga manyoya!

Yaani tatizo la kisiasa linatatuliwa kipolisi. Watu wanataka kujua kwa nini kitambulisho cha Uzanzibari kiwe ni sifa ya uandikishaji wa wapigakura? Cheti cha kuzaliwa hakitoshi? Na hicho kitambulisho kwanini iwe balaa kukipata? Watu wanataka kujua kwa nini daftari la wapiga kura liwe siri?

Haya ni maswala ambayo hayawezi kujibiwa na IGP. Ilitakiwa Rais Kikwete aingilie kati na kuonana na wadau wote huko Zanzibar. Ilitakiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itimize wajibu wake na kuisaidia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Badala yake NEC inajivua lawama kutokana na matatizo yanayojitokeza Zanzibar na kuitupia mzigo huo ZEC.

Katika baadhi ya vituo hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza kuandikisha. Hata ZEC yenyewe imesema hairidhishwi na zoezi hilo kutokana na kasi ndogo ya uandikishaji. Imesema zoezi hilo katika Mikoa ya Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba, “halikutoa mafanikio” yaliyotarajiwa. Lakini CCM eti inaipongeza ZEC kwa “kazi nzuri.” Huo siyo utatuzi wa kisiasa tunaozungumzia.

Matatizo haya hayakuibuka ghafla. Yalibainika mapema. Julai mwaka huu tuliambiwa kuwa huko Zanzibar kumekuwao malalamiko kwamba kuna wananchi wananyimwa haki yao ya kujiandikisha. alalamiko haya yalifika hata bungeni ambako baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar walilalamika kwamba watawala wa Zanzibar kuanzia sheha hadi wakuu wa wilaya wamejenga utaratibu mgumu kwa baadhi ya watu kupata vitambulisho vya ukaazi.

Zanzibar imekuwa na migogoro ya kisiasa hata kabla ya uhuru wa 1963 na Mapinduzi ya 1964 na kuendelea baada ya uchaguzi wa 1995, 2000 na 2005.

Kama mara hii tena uandikishwaji utatawaliwa na vurugu ni dhahiri kuwa visiwa hivyo vinaelekea kubaya.

Chanzo: Mwananchi la 30 Septemba 2009

Advertisements

One thought on “Zanzibar: Tusipoziba ufa tutajenga ukuta

 1. Ahsante Visram. Tanzania inaishi kii Ali Nacha nakudhani siku zote watakaa ndani ya miaka 5 wafanye watakavyo ikifika uchaguzi kuelewa fika hawatachaguliwa na hapo tena kila mbinu za Ghilba kuchukuliwa pamoja na kutumia nguvu za Dola.
  Prediction yangu mie ya waziwazi nikusema Tanzania itakuja kuwa Angola, Liberia, Sierealeone watu watachoka nakusema sasa liwe lakuwa.

  Zanzibar ni udhalimu na uharamia ndio unaoendlea na Marekani na wenzake ikiwa Uiengereza na Serikali za Magharibi kwakhofu zao za kipumbavu wao watayaachia haya, lakini watakuja juta pale mambo yakararuka na kubakia uchi. Seif Shariffu na CUF wameshawaweza lakini hiyo sio kumaliza dhuluma, kutatokea kina Lakama, Fodi Sanko au kina Alshabab nakuanza vurugu la kwelikweli. Angalieni Mabomu yanavyoripuka Pakistan na Afghanistan hayo yametokea wapi? Hayatoweza kufika Bara na Zanzibar, hayatoweza kuripuliwa na wale watakaokuja kusema sasa bora kufa kuliko kuishi.

  Mwalimu Nyerere watu humkumbuka kwa lile linalomvuta mie Nyerere namkumbuka alivyowatoa shoti Kikwete na Lowasa hakika Kikwete bado hajawa kiongozi, ikiwa Elvis Presley sawa au Amita Bachan kuvaa leo Jacket, kisha hati. Nchi hii ipo kwenye Msukosuko awakumbuke kina Samora, Amica Cabral, Mzee Seke Toure awache bobish. Kidagaa hakitooza mikononi mwa yoyote yule isipokuwa ni yeye na mtandao na kina Yussuk Kamba hapana Makamba. Wapi Mangula na Makamba ni dhahiri uwezo wake hata wakufikiri ni mduchu na ndio maana mara Dowans, IPTL huu, waaa, wuuu. Kwa Ban Kin Moon anakuja na maeneno ya kichale juu ya Zanzibar anaingia Tanzania anasema mengine.

  Nawatahadharisha wa Bara na Zanzibar yatakuja kuwa koliko ya India na Srilanka oneeni ukweli na Uharamia wa CCM-Zanzibar sio kuiba kura bali hata kuwakataa Raia zake, jamani mtakuja kulia kilio cha Mbwakoko.

  Leo Zanzibar inakuwa na waziri Hamza asiojua Historia anachojua ni kusema ovyo. Anaijua USA na Zanzibar? Anamjua Caluci? Anamjua Don Peterson? Yupo kuropokwa na kuonyesha kuwa yeye sio aliokuwa mshoni wa Janjaweed sasa ni kiongozi. Wapi Zanzibar itakwenda pale kwenye brains za babu, Twala, Athumani Sahrif, Ali Muhsin kutokuweko leo kuburuzana na kina Hamza.

  Tujuwe Westerners program yao imeshadumu miaka 40 kuelekea 50 kuifisidi Zanzibar kama ya Philipines lakini ya baada ya hapo kuanzi kwenda 50 tukiwa hai basi vumbi lake halitoshikika kwa wazanzibari kuitaka haki yao ya kwelikweli na kuondokana na ukoloni wa kibara ambao wapo tayari kuwachia watawala wa zanzibar wajifanyie kila la unyama lakini waendelee kubakia kwenye madarak, na kusikia kauli za kina Membe na kina Wangazija koko kina Saidi Mwema sijui kama anajua jamaa zake wa Zanzibar wanaambiwa kuwa sio makwao hapa, nmwambia ajue na yeye siku yake haiko mbali na salamu tutazifikisha kwa Mtikila. Saa hatutoweza kuirudisha nyuma (lenini) lakini Mapinduzi ni mabadiliko na yatatokea Zanzibar na Tanganyika ni wakati tu ndio ni muamuzi.

  wazanzibari enedeleeni kupiganuia haki na kina Sefu achaneni nao, kila mtu kwasasa afikirie ukombozi, Mwamsho, Hizbul Tahriri, viajana wa kijiweni, upanga kila kikundi kipigane kwa mbinu zake na mwisho mie nitasema tuataeleka kwa kina Alshabab na hapo ndipo watajuwa wakuu wa bara wamefanikisha.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s