CUF kufunga barabara kushinikiza tume huru

Sunday, 27 September 2009 17:16
Elisante Kitulo na Godfrida Jola

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema wakati wa maandamano yake keshokutwa kitafunga baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam ili kushinikiza kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi na kutungwa kwa katiba mpya ambayo itapanua wigo kwa demokrasia nchini.

Akizungumza jana Dar es Salaam katika kongamano la wanachama wa CUF, Katibu Mkuu wa chama hicho, Seif Sharif Hamad alisema maandamano hayo yataanzia katika barabara ya Uhuru, Bibi Titi na Maktaba hadi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw John Tendwa.

Alisema kuwa maandamano hayo yatakuwa ya kihistoria yatakayodhirisha kuwa wananchi wamechoshwa na ubovu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ‘imekuwa kichaka cha chama tawala’.

“Katika maandamano yetu tunatoa wiki mbili kwa Bw.Tendwa kumaliza zozo hilo kama sivyo tutaandamana tena hadi Ofisi ya Waziri Mkuu na ikishindikina pia huko tutaandamana usiku na mchana hadi Ikulu kuhakikisha tunapata haki yetu ya msingi,” alisema Bw.Seif

Alisema kuwa lengo la maandamano hayo pia ni kutaka kuuonyesha Mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Madola (CTA) unaoanza leo mpaka Oktoba 4 mjini Arusha kutambua kuwa Tanzania hakuna demokrasia.

Akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa, alisema kuwa wananchi wanatakiwa kupewa haki ya kujiandikisha bila vikwazo na uhuru wa kuwachagua viongozi wanaowataka ili kuepusha migogoro ya kisiasa.

Kwa upande wa kasoro zilizojitokeza katika shughuli za uboreshaji wa daftari la wapiga kura alisema ni chuki za kupandikizwa na baadhi ya viongozi na kutaka kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi wa wawakilishi.

Naye Mkurugenzi Uenezi na Mahusiano ya Umma CUF Bi.Ashura Mustafa alisea, “Baada ya maandamano Dar es Salaam Septemba 30, Oktoba 1 tutajiunga na wenzetu Morogoro kushininikiza Tume huru ya Uchaguzi kuundwa na kutupatia majibu ya kuridhisha kwa kile tunachokidai,” alisema Bi.Mustafa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s