Nyumba zachomwa moto Pemba

WATU wasiojulikana usiku wa kuamkia jana walichoma moto nyumba mbili
ikiwemo ya Sheha wa Shehia ya Kiuyu Minungwini katika Jimbo la Ole Mkoa
wa Kaskazini Pemba.

Mbali na nyumba hizo, pia watu hao wameweka mizinga mitatu ya nyuki
katika Kituo cha Uandikishaji wapiga kura cha Kambini Mchanga mdogo
katika Wilaya ya Wete usiku huo huo kwa lengo la kuzuia kazi za
uandikishaji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba,Yahya Hemed Bugi amethibitisha
kutokea kwa matukio hayo na kueleza kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo
linawasaka wahusika ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

“Kama nilivyosema kuwa kuna matukio hayo mawili kwa matatu, usiku wa
kuamkia leo(jana) nyumba ya Sheha wa Kiunyu Minungwini imechomwa moto na
kuteketea kabisa na nyumba ya mama mmoja pia imeteketea kwa moto”
amesema Kamanda Bugi.

Kamanda Bugi alimtaja mama aliyechomewa moto nyumba yake kuwa ni Salama
Ali Makame (38) Mkaazi wa Kijiji cha Kangagani katika Jimbo la Ole
ambalo kazi ya uandikishaji imeanza tangu juzi ambapo tukio hilo
lilitokea majira ya saa 7:00 usiku.

Alisema katika tukio hilo, wasamaria walijitokeza kumsaidia mwananchi
huyo ambapo kutokana na dhana duni za kuzimia moto, nyumba yake na mali
ziliteketea, ingawa kwa sasa Kamanda huyo alisema haijafahamika ni
hasara kiasi gani imepatikana.

Akizungumzia tukio la pili la Sheha kuchomewa moto, Kamanda Bugi alisema
tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo majirani wa nyumba
hiyo walianza kuona moshi ukifuka katika paa la Kiongozi wao na ndipo
walipoanza kuamshana, wakati Sheha huyo akiwa katika harakati za kujiokoa.

Katika tukio jingine, watu wasiojulikana wameweka mizinga mitatu ya
nyuki katika kituo cha uandikishaji kwa dhamira ya kuzuia wananchi na
wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi kukaribia kituo hicho, lakini ilipofika
majira ya asubuhi, wafanyakazi wa ZEC waliweza kufika huku wakichukua
tahadhari kubwa ya kuhofia kufumuka kwa nyuki hao.

Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman amesema,mara baada ya nyuki
hayo kuonekana, waliamua kutafuta wataalamu kuweza kuwatoa ili wasiweze
kusababisha matatizo kwa wananchi, shughuli hiyo ilikamilika saa 4:30
asubuhi.

“Hawa watu bwana sijui wanataka nini, kujiandikisha hawataki, wanaotaka
kujiandikisha wanawafanyia visa…hizi ni siasa za ajabu sana wanazofanya
kinyume kabisa na demokrasia sasa hawa nyuki wamewaweka ndio itawasaidia
nini.” Amesema mkuu huyo wa Wilaya.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo,Chama cha CUF kimekuwa ni Chama chenye
kukandamiza demokrasia kwa kuwa kimewahamasisha wafuasi wao wawazuie
wananchi wengine kwenda kujiandikisha.

Wakati wa asubuhi, watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa Chama cha CUF
walianza kujikusanya katika vituo vya uandikishaji, lakini ilipofika
wakati wa kuanza kuwaandikisha walikaa kitako huku wakizungumza masuala
mengine kama vile kuna shughuli ya harusi.

Watu hao waliwatupia maneno makali ya kebehi na dharau Wananchi wengine
walijitokeza kujiandikisha wakiwaita kuwa ni wasaliti.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s