CUF yajipanga kushinikiza Jaji Makame ajiuzulu NEC

Na Salim Said na Hussein Kauli

MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema chama chake kinajiandaa kuchukua hatua kali za kisiasa ikiwa ni pamoja na kuitisha maandamano na mikutano ya hadhara kote nchini,kushinikiza kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame.

Lipumba aliliambia gazeti hili jana kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kauli za kejeli na dharau dhidi ya haki za msingi za Watanzania walizonyimwa, baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kikishirikiana na NEC, kununua shahada na kuziteketeza kinyemela, ili kupunguza idadi ya wapigakura.

“Hii ni kejeli na dharau dhidi ya haki za msingi za Watanzania. Unadiriki kuziita tiketi hai za Watanzania kupigakura kuwa ni takataka kwa kulinda maslahi yako na ya chama chako tawala,” alisema Profesa Lipumba kwa mshangao.

“Kama shahada hizo ni takataka zilizokusanywa na kuchomwa katika utaratibu wa wazi, kwa nini alipoulizwa na vyombo vya habari juzi, Jaji Makame alisema hana taarifa na uchomaji huo. Uchomaji gani wa wazi ambao hata Mwenyekiti wa NEC hana taarifa,” alihoji.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Rajabu Kiravu, amekitaka Chama cha Wananchi, kuacha kutunga mambo na kuyatangaza kwa jamii, kama njia ya kutafuta mtaji wa kisiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Kiravu alisema kitendo hicho ni cha kupotosha jamii na kuifanya ipoteze malengo yake.

Kiravua alisema kitendo hicho cha CUF, kimefanywa kwa lengo maalumu la kupotosha jamii ili ionekane kuwa NEC ina lengo la kuvurugha uchaguzi.

Kiravu aliunga mkono hoja ya Mwenyekiti wa tume, Jaji Makame, kwamba shahada zilizoteketezwa ni zile ambazo zilikusanywa wakati wa zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura ambazo hazihitajiki tena.

“Zoezi la kwanza la kuteketeza shahada zillizopatikana katika uboreshaji wa daftari la wapigakura, lilianza mwaka 2007 na kuishia mwaka 2008,”alisema Kiravu na kuongeza:

Alisema kuteketezwa kwa kadi hizo hakuwezi kuwa njama ya siri kwa sababu isingeweza kufanywa hadharani.

Akizungumzia madai ya CUF kuwa walikuta shahada za tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Kiravu, aliishutumu CUF kuwa huenda ilikwenda nazo.

“Sisi hatujaboresha daftari la wapigakura la Zanzibar, kwa hiyo wanaposema walikuta kadi za ZEC sisi tutaamini vipi, kwani walipovikuta mimi sikuwepo” alisema Kiravu.

Kutoakana na hayo Kiravu ameisihi CUF iache kapeni chafu kwani kuna mambo mengi ya maana inapasa kuyafanya.

“Kama wangekwenda mikoani wakaja wakatuambia tumekuta tatizo hili na hili lingekuwa jambo la maana sana kuliko kuihadaa jamii” aliongeza Kiravu na kuongeza.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s