CUF chakana kuwachomoa wanaoandikishwa kwa kura

14th September 2009

Chama cha Wananchi (CUF), kimekanusha madai ya kwamba wanachama wake ndio waliohusika kuwachomoa wananchi waliokwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura visiwani Zanzibar.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Salum Bimani, amesema wananchi wenyewe ndio waliofanya hivyo baada ya wengi wao kukosa vitambulisho vya ukaazi.

“Hakuna uandikishaji hapa… wananchi ndio wanawatoa wenzao wanaowasaliti kwa kwenda kuandikishwa kwa sababu wengi wao hawana vitambulisho vya ukaazi,”akasema Bw. Bimani.

Jumamosi asubuhi, zoezi hilo lilitawaliwa na vurugu katika vituo vingi vya kuandikisha wapiga kura kwa madai kuwa watu wengi hawana vitambulisho vya ukaazi.

Mbunge wa jimbo la Ole, Bakari Shamis Faki, amesema kuwa anaamini vurugu hizo zimetokana na vijana na wazee wengi katika jimbo lake kukosa vitambulisho vya ukaazi.

Akasema katika jimbo lake hilo, karibu watu 3,000 hawana vitambulisho vya ukaazi, jambo ambalo limewafanya wakose haki ya kujiandikisha katika daftari hilo.

Akaitaka Serikali kuhakikisha inalimaliza tatizo la ukosefu wa vitambulisho kwanza ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa haki.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Dadi Faki Dadi, amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwazuia wenzao kujiandikisha katika daftari hilo.

Hata hivyo, licha ya kuwasihi bado vitendo vya kuwachomoa wanaojiandikisha liliendelea na kufanya zoezi hilo kusimama.

CHANZO: ALASIRI

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s