UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA: Seif aibua shutuma nzito

Friday, 07 August 2009 16:01

*Ahusisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano
*Ataka Jumuiya ya Kimataifa iingile kati
*Ahusisha pia vigogo wanaowania madaraka

Aziza Masoud na Aisha Kitupula

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka Serikali kutojihusisha na vurugu pamoja na kupunguza wananchi wenye sifa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura visiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Maalim Seif, alidai kuna taarifa za uhakika kutoka vyanzo vya kuaminika ambazo zinasema Serikali ya Muungano ndiyo inayoendesha mikakati ya kuvuruga Daftari la Wapiga Kura.

“Serikali kupitia viongozi wakuu na vyombo vilivyo chini yake, wamejiingiza katika kuvuruga Daftari la Wapiga Kura kwani haiwezekani asilimia 70 ya Wazanzibari wawe juu ya umri wa miaka 18,” alisema Maalim Seif.

Alisema mipango hiyo ina nguvu kutokana na kuungwa mkono na kuratibiwa na viongozi wa CCM wanaotaka kugombea uongozi wa ngazi za juu visiwani humo.

Aidha, alisema mkakati huo umefanikiwa kwani mpaka sasa Wazanzibari 11,012 wamepunguzwa kwenye Daftari katika tathmini iliyofanyika katika majimbo ya Konde, Mgogoni na Micheweni Pemba na 6,000 katika Jimbo la Magogoni Unguja.

“Tulizoea kuiona Serikali ya Muungano ikishiriki katika kuvuruga chaguzi za Zanzibar kwa kumimina vikosi vya ulinzi na usalama na silaha nzito za kivita kuja kuwatisha na kuwadhibiti Wazanzibari ili wasitekeleze haki yao ya kuwaweka madarakani watu wanaowataka kwa njia ya kidemokrasia,” alidai Maalim Seif.

Alisema kuwa dhamira ya Rais Jakaya Kikwete ya kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar ambayo aliisema wakati akilihutubia Bunge mwaka 2005 haikuwa ya kweli bali ililenga kujenga mazingira ya ushindi kwa CCM.

“Huu ni uporaji wa haki ya Wazanzibari kuchagua viongozi wanaowataka uliopangwa kutekelezwa na Serikali ya Muungano , uhalifu huu hauwezi kukubalika na Wazanzibari,”alidai Maalim Seif

Kutokana na hali hiyo alitoa mwito kwa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati mipango hiyo mibovu ili kuinusuru Zanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s